jah kimbute akiongoza kundi lake la roots and kulture enzi hizo. mwenye nyeupe na bakora mkononi na mvi kishwani ni david manju ambaye sasa ni fundi hodari wa nguo za kiafrika. hivi sasa bendi hii imekula pozi na jah k anafanya biashara na ukulima huko tanga (leo nimeambiwa yuko dar kikazi) na wanamuziki wengine wametapakaa kwenye bendi mbalimbali. roots and kulture itakumbukwa kwa umahiri wake wa kupiga muziki wa reggae..
.
Home
Unlabelled
roots
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Do nakumbuka vibao kama KITUMBUA CHANGU UPANDE MMOJA KIMEUNGUA..
ReplyDeleteEti ni kweli kaka Michuzi kwamba Manju alikuwa anatishia sana katika fani kiasi kwamba Jah Kimbute akawa anaona wivu, hasa ugomvi ulianza walipokwenda Jamaica, na Manju akaonekana nyota zaidi ya Kimbute. Pia eti ndo chanzo cha bendi kusambaratika?
Manju kwa sasa ni Mbunifu wa mitindo mahiri sana nchini, nadhani kwa mtazamo wangu, he is the best so far, ingawa rafiki yangu Hasanali akinisikia ataninyima tenda za designing. haha haha