mwandaaji wa filamu ya supa modo nassir mohamed akinadi posta ya uzinduzi wa filamu hiyo itayozinduliwa rasmi leo pale landmark plaza ubungo ambako twanga international, darda king, jaffarai na wasanii wengine kibao watatumbuiza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2007

    Kifo cha Amina Chifupa chaivuruga familia yake

    na Shabani Matutu


    KIFO cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Amina Chifupa (CCM), kinaonekana kuichanganya familia yake ambayo sasa imebadili mwelekeo wake wa awali, na kuanza kulihusisha tukio hilo na sababu za kishirikina.
    Wiki tatu baada ya familia hiyo kukihusisha kifo hicho na maradhi, ikisema alipoteza maisha kwa kisukari na homa kali, jana baba mzazi wa mbunge huyo, Mzee Hamisi Gabriel Chifupa, aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam taarifa tofauti na za kushangaza.

    Mzee huyo, kada wa muda mrefu wa CCM alisema kuwa, baada ya Amina kuanza kuugua, familia ilipata ofa kutoka sehemu kadhaa kumpeleka mbunge huyo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

    Aliwataja waliotaka kumpeleka Amina nje ya nchi kwa matibabu kuwa ni Ofisi ya Bunge pamoja na Kampuni ya Mohamed Enterprises.

    “Nilikataa ofa hizo zote baada ya kujua kuwa ugonjwa unaomsumbua marehemu kuwa ni wa Kiswahili, tukaona si vyema kumpeleka nje na badala yake tukaamua kumpeleka kwa waswahili ili atibiwe… kama anaumwa ugonjwa wa Kiswahili kwanini tumpeleke Ulaya?” alisema Chifupa na kuhoji.

    Akielezea matukio kabla ya kifo cha binti yake, Chifupa alisema kuwa, Mei 8 mwaka huu, alikutana na binti yake nyumbani kwake Mikocheni, alipokwenda kumtaarifu kuwa alikuwa na ziara ya kikazi mkoani Mtwara.

    Hata hivyo, wakati huo hali yake kiafya ilikuwa imeshaanza kuzorota, aliamua kumzuia asiende ziara hiyo, lakini binti huyo aligoma na hatimaye akaamua kuondoka Mei 6, kwa kuwaomba wamsindikize sambamba na mdogo wake.

    Alisema wakiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, walikutana na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Mark Mwandosya, akiwa katika chumba cha wageni mashuhuri (VIP) na Amina alizungumza naye kabla ya waziri huyo kuondoka.

    Chifupa alisema baada ya muda, Amina alimuita mhudumu wa chumba hicho na kumuomba amrudishie mzigo wake kwa sababu alikuwa ameahirisha safari yake.

    Alisema baada ya Amina kuahirisha safari, walirejea nyumbani kwao Mikocheni, lakini hali ya binti yake ilianza kubadilika huku akisema maneno makali akitaja majina ya baadhi ya viongozi na kudai kuwa wao ndio walimsababishia matatizo hayo yote.

    “Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, tulimuita daktari ili amuhudumie, daktari alimpatia dawa, lakini hali yake haikuwa nzuri, ndipo tukagundua kuwa yale yalikuwa mambo ya Kiswahili… tukaamua kumpeleka kutibiwa Kiswahili kwani alikuwa hali chakula katika kipindi chake chote cha kuugua,” alisema Chifupa.

    Baada ya kumtibu kwa waganga wa kienyeji, hali ilizidi kuwa mbaya na mwisho waliamua kumpeleka hospitali ambapo aligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha sukari mwilini kilichofikia kipimo cha 400 ambacho kilikuwa hakishuki na wakaamua kumhamishia Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.

    Alisema hata wakati alipokuwa hospitalini hapo, Amina bado aliendelea kutamka majina ya viongozi ambao alikuwa akiyatamka awali, na aliendelea kufanya hivyo hadi mauti yanamkuta Juni 26 mwaka huu, majira ya saa 2:45.

    Hata hivyo, Chifupa hakuwa tayari kuyataja majina ya viongozi ambao binti yake alikuwa akiwataja wakati wa kuugua kwake, lakini alisema yapo baadhi ya majina ambayo tayari yameshaandikwa magazetini.

    Jambo lingine lililoisababisha familia ya Chifupa kukihusisha kifo hiki na mambo ya kishirikina, anasema ni ndoto aliyoiota siku tatu baada ya kifo cha mbunge huyo.

    Alisema katika ndoto hiyo, alitokewa na bibi wa marehemu Amina, Tulionana Mnyalape, ambaye alimuuliza mjukuu wake yupo wapi.

    Alipomjibu kuwa alikuwa kwa Mungu, bibi huyo alisema kuwa Amina hakutaka kwenda huko mapema, ila binadamu ndio waliompeleka kabla ya wakati wake.

    Pia mdogo wake, Bakari Chifupa, alimuota Amina akimwambia kwamba waishi kwa amani, wapendane na wamuombee na wawaheshimu wakubwa na pia amueleze bibi yake mzaa mama yake kuwa amekwenda hapo kijijini kuishi naye.

    Kuhusu kuhusishwa kwake na vita dhidi ya dawa za kulevya, alisema kuwa iwapo kifo cha mwanawe kimehusika na wauzaji wa dawa hizo, vita hiyo itakuwa haijazima, bali itakuwa imetiwa petroli.

    Wakati huo huo, Chifupa alisema kuwa familia yake imeanzisha mfuko wa kumuenzi marehemu Amina, ambao unajulikana kama ‘Amina Chifupa Foundation’ nia ikiwa ni kulienzi jina la marehemu Amina kwa yote aliyokuwa akiyafanya enzi za uhai wake kama vile kupiga vita dawa za kulevya na kusaidia wasiojiweza.

    Kwa mujibu wa Chifupa, Mwenyekiti wa mfuko huo ni diwani wa Njombe, ambaye ni mjomba wake, Augostino Mbanga, ambapo pia gari la marehemu Amina litatumika katika shughuli za mfuko huo na kuanzia sasa litakabidhiwa kwa viongozi hao wa mfuko.

    Aidha, alisema kuwa baadhi ya wajumbe wa mfuko huo watatoka kwenye kamati ya kampeni ya ubunge ya marehemu Amina na kamati ya mazishi yake.

    Alitoa wito kwa mtu mwenye nia ya kuchangia mfuko huo, afanye hivyo kupitia akaunti katika benki ya CRDB tawi la Kijitonyama yenye namba 01J1014153400.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2007

    kwako michuzi na watanzania woooote, napendekeza siku ya marudiano yetu na msubiji picha kubwa ya mh marehem Amina iongozane na timu yetu itakayoanza kama cameroon ilivyo fanay kwa marc vivian foe maana amina alikuwapo kule msubiji wakati tukicheza na nao amina alikwa stars kwa vitendo ni ombi kwa wadau wote mnasemaje?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2007

    Nilidhani hapa ni comments za Nassir na juhudi zake ya movie. CONGRATS Nassir....you've done it.
    Tunahitaji watu kama nyinyi kueleza story za kibongo - pia Mr. Siagi....CONGRATS!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2007

    Hawa wangempeleka mwanao kutibiwa. Haya mambo ya kufikiria ushirikina basi tena siwezi kusema lakini mbona ushirikina haupo kwenye nchi zilizoendelea? Ina maana voodoo ni la watu weusi tu?

    Wangejaribu kote kote kuliko kutegemea imani tu. Na kusubiri mpaka mwanao keshazidiwa ndio wnamkimbiza hospitalini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2007

    jamani uuuuuuuuuwi siamini ninayosoma huyu mzee na wanaohusika wanatakiwa kufunguliwa mashtaka yakuuwa bila kukusudia iwe fundisho kwa wengine jamani kisukari kikipanda dalili zake nini?? kama siyo kuchanganyikiwa au kupagawa?na hiyo sukari ya 400 ni kwa kipimo gani? au arobaini? naaomba tutumie huu mwanya kuwaelimisha watu niwangapi wanakufa kama amina kwa ugonjwa mdogo kama kisukari??/
    naogopa naogopa kabisa madaktari na manesi ukumbi kwenu pls pls michuzi publish this one mungu bariki africa. Dos

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 13, 2007

    kaka michu,huyu nassir kuna kitu amewaboa watanzania,mbona sehemu ya comment zake kuna habari za Amina Chufupa?Inakuaje hakubaliki hivyo?Haya ngoja mi nianze kwingine

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 13, 2007

    hivi nyinyi WABONGO Mbona!!!!!!!!!!
    Hapa ni kupost comments za Nassir and his achievements.....SIJUI huyu changu doa Chifupa discusssion yake inaingiaje hapa???

    Na wewe Bwana Michuzi kwanini usi edit basi peleka hizo comments za Chifupa to its rightful place......MBONA HIVYO!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2007

    Michudhi,wa ughaibuni tukitaka kuchangia huo mfuko wa Amina tufanyaje?swali tuu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2007

    Haya Jamani haya mambo ya Amina Chifupa yataisha lini? Amekufa ndio amekufa na Mungu aiweke Roho yake mahala pema peponi.
    Mie nilifikiri Maada ilikuwa juu ya Movie ya Supa Model na chini yangekuwa ni maoni juu ya hayo, Lakini Michuzi na wewe ni kama hukagui comments bwana. Soma kabla hujapost. Habari za babake Amina Chifupa ungezipa nafasi yake na watu wa comment accordingly.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2007

    we anon wa july13 9;13 huna adabu hata kabla hujazaliwa na mamayo wewe , chunga mdomo wako mchafu pumbaffff.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2007

    SAMAHANI WADAU, HUYU DADA ALIE SUKA RASTA NA NINAHISI NI MEAN 'CHARTER'(MUHUSIKA MKUU )KAFANANA SANA NA DADA MMOJA AITWAE AICHI KUTOIE JE SIYO YEYE???

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2007

    Annoy usiwalaumu madactari kwa kuua bila kukusudia. Tatizo walimpeleka kwanza kwa waganga wakienyeji kwanza. Kumpeleka ikawa too late. labda ni kisukari kweli lakini umeshasikia wazazi wamesema walikataa offer zote wakijua ni mambo ya kiswahili.

    La muhimu ni kuielimisha taifa sana tu. Miaka hii nado tunapoteza wengi kwa mawazo hayo.
    dalili moja ya kisukari ni kuwewesuka na dalili ya maleria ni kuwa kama kichaa vile. sasa hizi dalili zinafanana pia na mambo ya ushiikina.

    We have a long way to go..

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 17, 2007

    sisemi madaktarindo wauaji , nasema babake mzazi ndo muuaji kwa kutompeleka hospt mapema. hakuna ushirikina duniani nakama upo ni juu hatujui sababu ya ugonjwa niko nafanya na vichaa ambayo ingekuwa bongo tungesema ni kipapai lakini hapa yana diagnosis yake . elimu muhimu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 18, 2007

    Amina Chifupa tunakukumbuka.. halafu wewe mwenye muvi watu wanalipia matangazo humu ndani, mpaka uambiwe ??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...