balozi wa redds 2006 joketi akitangaza namna shindano la kumsaka balozi wa redds mwaka huu litavyokuwa leo katika ukumbi wa hoteli ya beach comber ambako warembo hao wamepiga kambi. toka shoto ni wabunifu wa mitindo kevin mosha na ally rhemtullah, joketi, meneja wa redds mpeli nsekela na miss tz 2006 wema sepetu.

mshindi wa tuzo ya mitindo ya balozi wa redds 2007 atanyakua mkwanja wa milioni 2 unusu na alawansi ya laki 2 kila mwezi kwa mwaka mzima. vigezo 10 vya mshindi ni kwamba anatakiwa awe:

1. mchangamfu, mwenye ucheshi na mvuto
2. uwezo wa lugha za kiinglishi na kiswahili
3. mwepesi kuelewa, kufikiria na kuchambua mambo
4. utulivu wa kujiamini bila jazba
5. hekima, busara na tabia njema
6. miondoko ya kimaonyesho ya mitindo ya nguo
7. ufahamu na uelewa wa mambo ya mitindo ya kitaifa na kimataifa
8. ufahamu na uelewa wa kinywaji cha redds
9. awe na mvuto katika picha
10. bashasha, mchangamfu, mwenye mlahaka na mkabala mwema

futi kamba: awe na urefu wa walau futi 5 na inchi 8, kiuno inchi 26-28, kifua inchi 32-34 na hipsi inchi 36-37



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Vigezo Vyote Hivyo Vimemdondokea Miss Tanga Na Hakuna Ubishi Katika Hilo!

    Izz Wa

    ReplyDelete
  2. Hee!! MPELI NSEKELA!! Ugonile kaka! Twambombo!! Siku nyingi sana enzi za Mbeya. Haya kazi njema

    ReplyDelete
  3. mbona mmsesahau kusema kuwa lazima pa awe ni mywaji mzuri wa redds.

    ReplyDelete
  4. kazi kweli kweli huyo mwenyewe aliyetoa hivi vigezo anavyo vyote ye mwenyewe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...