wadau,
wataalamu wanaposema kwamba theluji mlima kilimanjaro inakauka sio kwamba wanapenda kuosha vinywa bali wanaelewa wanasema nini. hii ni picha iliyopigwa wiki iliyopita na ukisoma na posti ya hapo chini utajua kwamba hali si nzuri na huenda theluji ikapotea kabisa sehemu hiyo tukabakiwa na liji-chuguu tu..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. NAJUA WENGI WANASHANGAZWA NA GLOBAL WARMING NA HIYO THELUJI INAYEYUKA KUTOKANA NA "LAVA" ILIYOPO NDANI YA HILO SHIMO KULIPUKA NA KUKARIBIA KUTOKA NJE.
    KUNA UWEZEKANO LAVA IKALIPUKA SIKU YOYOTE HIVI KARIBUNI. HUU NI WAKATI MUAFAKA KWA WANA-SAYANSI KUCHUNGUZA KWA MAKINI NA KUJUA LAVA YA KILIMANJARO ITALIPUKA LINI NA WAKATI GANI ILI KUWAANDAA WAKAZI WALIO KARIBU NA ENEO HILO KUANZA KUFUNGASHA VIRAGO.
    MENGINE ZAIDI NITWALETEA BAADAYE HASA KUHUSU DALILI ZA KULIPUKA KWA MILIMA YENYE LAVA KAMA HUU WA KILIMANJARO, UDZUNGWA NA MENGINE HAPA DUNIANI KAMA SIYO ULIMWENGUNI.

    ReplyDelete
  2. I think we should all turn back to stone age, that would be a perfect situation in reversing this global warming phenomena.

    Once the quest and lust for materials things, still persist, I don't think will get anywhere, we can stall the global warming but the reality is we wont be able to stop it.

    It is my hope at least stone age, is not reality BUT, detesting materials would be ideal combination of stalling this madness.

    I think we should start with you Michuzi, no more flying around, stay put in Dar. we should start commuting using bicycles, donkeys and other earth friendly cars.

    lol,

    That was a joke, but Seriously, I believe this is a serious issue, we should take it as such,

    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  3. Bwana Michuzi, isikuchanganye hiyo theluji kwisha. Muda huu ni wakati wa joto kwa mazingira ya East Africa. Kwa hiyo joto ni kali sana na si ajabu barafu kuyeyuka.

    Usisikilize maneno ya wanaojiita wataalam.Hao watalaaumu wengi hawkuwepo Africa miaka iliyopita. Ndo maana wanawachanganya hata local scientists.

    NI kwamba muda huu ni wakati wa joto kali Africa ya mashariki na kati. Si ajabu kwa barafu kuyeyuka. Jaribu tena kupiga picha mwezi wa tano wa sita mwakani na uilete hapa hapa kwenye blog. Nadhani utashangaa.

    Ingawaje issue ya global warming ipo, laKINI SI isssue kubwa sana kwa maeneo yetu ya Africa Mashariki. Wasitake kuwakimbiza watalii. Hakuna kitu kama barafu au theluji kuyeyuka hapa.

    ReplyDelete
  4. We anon wa Dec 22, 9.15, wacha kucheza madogoli, hivi unafikiri ni wataalamu wa nje tu ambao wanasema theluji ya Kilimanjaro inayeyuka? Hata hapa kwetu wataalamu wamekuwa wakifanya utafiti kuhusu mlima Kilimanjaro kwa muda sasa na ni kweli theluji inapungua.

    Hivi unavyosema joto la msimu una uhakika kweli, umekwisha panda mlima au kukaa mahali popote ambako ni high altitude/milimani juu ukaona joto lake. Kwa altitude ya Kilimanjaro panda huko juu ukiwa umevaa vesti ili upime hilo joto linaloyeyusha mlima.

    Jamani hebu tuwe tunasoma vijarida na mambo mbali2 yahusuyo mustakabali wetu. Hii global warming kweli ipo na kasi yake imekuwa kubwa. Kwa anayesema madhara yake hayapo East Africa naona huyu anaishi Ulaya, hali ya hewa imekuwa ikibadilika badilika kama kinyonga, ukame wa muda mrefu, mvua kubwa zenye kuleta mafuriko, njaa (kutokana na ukame na mafuriko), na kupanda kwa kina cha bahari. Nani ambaye hajayashuhudia haya?

    Wataalamu wanasema ifikapo 2015 theluji itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa, watu wamebishana huko Bali na waandishi wala hawakujisumbua kutuelezea nini kinaendelea na nini mustakabali wetu na nini matokeo ya huo mkutano wa Bali kwa lugha nyepesi ili tujue wakubwa wameamua nini katika suala zima la upunguzaji wa hewa chafu inayoathiri mazingira.

    ReplyDelete
  5. WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WANAPASWA KUJADILI TAARIFA KAMA HII ITAKUWA NA EFFECT GANI KWA IDADI YA WATALII TOKA JAPANI WATAKAOKUJA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO.

    KAMA NI POSITIVE EFFECT (say wanataka kuja kuona hiyo barafu) BASI WATOE TAMKO LITAKALOHIMIZA WAO KUJA.

    NA KAMA NI NEGATIVE EFFECT BASI WATOE TAMKO KWENYE HAYO HAYO MAGAZETI AU WEBSITE YAO KUWEKA MAMBO SAWA.

    ReplyDelete
  6. Michuzi mimi naona huo mlima inaweze kana ni global warming lakini volcanic mountains inatabia ya ku erupt kila baada ya miaka kadhaa na process ya mlipuko huanza ndani ya mlima pole pole hivyo wataalam wajulishwe kwani huo mlima huenda ukaripuka any time na kusababisha maafa ya ndugu zetu.

    ReplyDelete
  7. Hapo kuna hali mbili zilizochangia kupungua kwa theluji juu ya huu mlima
    1- Nikweli kuna swala la global warming lakini data zinaonyesha theluji itakwisha ikifika mwaka 2015
    2-Huu ni msimu wa joto kwa hiyo theluji lazima ipungue juu ya mlima

    NINI KIFANYIKE
    Ukataji wa miti ni moja ya sababu, mji wa moshi sasa hivi umekuwa na joto sana tofauti na zamani, watu wamekata sana miti na misitu ya hifadhi ikiwemo kilimanjaro kila siku inachomwa moto

    Sasa ukichanganya na global warming hali inakuwa mbaya sana, jamani naomba kila mtu ajitolee kupanda miti ili kuokoa kizazi kijacho, msimu huu mimi nimepanda miti 1000. Kama kuna mtu atahitaji kupata utaalamu wa bure kuhusu upandaji wa miti tuwasiliane (rhxoqsa@hotmail.com)

    ReplyDelete
  8. We Annon Sunday 23 2:12 usiwe na papara wala usidhanie kila kiandikwacho kwenye majarida ni habari.

    Unatakiwa ufikirie kwanza. Hii dunia imepita katika hatua nyingi sana. Moja ya hatua hizo ni Wakati wa Baridi sana na baadaye ikaja joto sana. Hapo kukatokea extinction na speciation za organisms depending na adaptability. Jinsi ulivyo sasa hivi ni kutokana na kwamba babu zako walipita katika hatua nyingi sana ambazo waliweza pambana nazo. Baadhi yao walikufa. Waliobakia ndo sisi hapa.

    Kwa hoyo issue ya Global warming usiinmgali kupitia mabishano ya Bali na mabadiliko ya hali ya hewa unayoyaona East Africa kwa sasa. Wewe angalia historia ya Dunia climatewise.

    Hata hapa bongo, angalia mwaka 62, 72, 82 na sasa hivi. Kama unakumbuka, 72 ndo Mwalimu Nyerere alipotangaza kilimo na kuhamisha watu kwenda vijiji na vijiji vingi vikaundwa muda huo. lengo lilikuwa ni kupambana na UKAME uliokumba Africa, ikiwemo bongo. Bahati mbaya sana watu wa wakati huo hawakuwa wanaelewa kinachoendelea. Pia issues za China au Marekani ku-produce green house gases hazikuwepo. Je, hii nayo utaiitaje?

    Kwa kifupi, hali halisi ya Kilimanjaro na pia hali ya hewa Africa Mashariki kubadilikabadirika, ni normal cycles za kidunia kama zilivyo cycles za mwanadamu na pia ya mwanamkee kila mwezi ambayo iko tofauti kila mwezi!.

    Msiogopeshwe wala kutishwa. Ndo maana Wataaaalumu wa NASA wamekaa kimya. Hata Marekani haiko na wasi wasi. Tatizo ni wale wanaodakika mambo. Ukiwemo wewe annnon.

    ReplyDelete
  9. Mbishi wa Dec 23, 8.28PM. Kasome ripoti ya kina Yanda na wenziwe pamoja na ripoti ya Al Gore (hivi ni Mmarekani huyu?). Hivi alipewa Tuzo ya nini vile, nimeshasahu aliandika kuhusu haya mabadiliko ya hali ya hewa au? Tena usilete suala la vijiji vya ujamaa vya Nyerere vilivyowatoa watu kwenye mashamba yao yaliyokuwa tayari yana chakula na kuwapeleka kwenye umaskini ambao tuko nao hadi hii leo. Mpaka leo watu wamepewa majina ya kuwa ni wavivu. watalimaje wakati kwenda kulifuata shamba liliko ni mwendo wa masaa mawili akifika shamba yu hoi wakati kabla ya vijiji alikuwa akiamka asubuhi anaamkia shambani.

    Global warming ipo, mpaka mkija stuka watu wameshapanga mikakati zamani ya kupambana na hali hiyo sie bado tuko tunabishana kuwa ipo au haipo wakati wenzetu wanajipanga na adaptation measures. Kalaghabaho mmezoea zimamoto!!

    ReplyDelete
  10. Can someone please explain the Global Cooling Scare we had in 1973? A lot was said but not such thing came to pass. The earth was apparently supposed to have cooled to a point where every living organism would have died. Global Warming as it may true that it is taking place mankind has no way to stop it. It is just another way of westerners to control mankind kind through economy and science. Al Gore has not debated anyone credible; his points have been refuted time after time again.

    The universe has gone through 7 ice ages. Many of them took place 1000’s of years ago. During the ice ages we had less industries as we have at the moment then how did all this take place….mhhh. Al Gore left office with $ 10 million and now he is worth over $ 100 through the carbon offset he is selling.

    Friends not everything that the Whiteman says has to be taken literally. I am a Tanzanian who has lived in America for the past decade and I am ashamed to see my people buying this lie day after day. There is a high price to be paid through this illiteracy, loss of jobs because companies are not meeting the carbon offsets requirements. More taxes to fight carbon dioxide.

    More carbon we have more synthesis takes place thus more tree and more oxygen.
    AL GORE is a LIAR….

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...