sekondari ya tambaza ilivyo leo na miti yake ya krisimasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. du kaka Michuzi umenikumbusha mbaaaali sana, kweli tunazeeka , tumebakiza mvi tu, nimesoma hapo 1995-1997, nikitazama hayo mazingira nakumbuka " those good old times" hapo kwenye hilo gari nafikiri ndo tulikuwa tunasimama asubuhi "mstarini"..du kweli miaka inaenda..Asante sana kaka kwa picha za shule yangu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi yaani hii y tambaza umenikumbusha mbali sana!yaani baada ya miaka kibao uhgahibuni leo ndio naiona tena Tambaza..shukrani kwa hizo picha za Wu-tamba!

    ReplyDelete
  3. Michuzi umenikumbusha mbali sana. Hii shule yangu bomba sana. Air Tambaza Corporation (ATC) ilikuwa inaondoka shuleni saa mbili na nusu. Lakini kutoroka kwetu shule tulikuwa tunaenda Tanganyika library kujisomea au pale American library. Shule ikipanda sana tunaenda kufanya ujasiriamali enzi zile kutafuta raba za kichina toka kwenye meli na kuzilangua kwa wapenda raba mtoni tunapata pesa za kuwazengua mabinti wa Zanaki Secondary. Siku ya mtihani wa taifa tuna "ubamiza" vile vile kwa kupata "A" kwasababu tulikuwa tunaenda maktaba kusoma. Ndio maana napenda kuwasilisha kuwa vijana waliosoma Tambaza hasa "O" enzi miaka za themanini na kurudi nyuma wametawanyika duniani nzima wakifanya kazi kama Madakitari, Engineers, Managers na nyadhifa mbali mbali. Kwasababu walifahamu kujituma tokea zamani na kufanya creative competition balancing education and entrepreneurship. Sio sikuhizi mtoto wa akademi hata kwenda shule na ufagio wa chelewa anaona ni mateso. Tambaza ya zamani chini ya Marehemu "Kalulu" Karumuna ilikuwa bomba !. We were ahead of our time.

    ReplyDelete
  4. Machizi wangu hapo juu umenikumbusha mbali kichizi, enzi za Mkuu Kalulu, kisha akaja Mushi naye akatolewa sijui aliyefata.... enzi za kina mwl. Dafa, Mandara, Mtunza maabara Hassan, na wengineo wengi -heshima mbele.. duuh, poa sana michuzi, na asante kwa picha..

    Masela wangu, hivi Azania bado wanawachukua Jangwani siku hizi au mambo yalishabadilika tena?...

    SteveD.

    ReplyDelete
  5. Tambaza ilikuwa miaka ya Head Master Felix Kalumuna na kabla ya hapo.

    alipoingia yule Mchagga toka Forodhani shule ikaharibika kabisa. alitaka kuleta ukuda wake wa Forodhani.

    Mwinyi,Sarungi,na Mrema, ndiyo waliamua kuivunja Tambaza.

    vijana wa tambaza waliunga mkono mgomo wa waalimu na system ikaona itakuwa soo.

    ReplyDelete
  6. That's right buddy , i wish pay tribute to all pilot of ATC as it was then known. Im from class 1981, currently in houston, texas. wish you all merry x-mas and happy new year.
    Tony.

    ReplyDelete
  7. MwanaTambaza mie nilimaliza mwaka 1980 hapo Tambaza. Wanatambaza kuna blog ya wanatambaza http://tambaza.blogspot.com/

    ReplyDelete
  8. Misupu asante sana kwa picha ..ya shule yangu..umenikumbusha mbali mnooo, yani napaona kabisaa mstarinii...namkumbuka bi mkoraa vizuri sanaa.Pia wu-tambaaa......na zaidi ule wimbo wa:

    Tambaza tambaza nakupenda sanaa
    mandhari yana ni vutia...
    leongo letu sisi shuleni tanambaza..ni TAZAMA MBALI ZAIDII...KATIKA MAISHA TWA TAZAMA MBALI.....SILAHA YETU NI ELIMUU,,'JUHUDI ,UNGWANA..PIA NA AKILI...NI KIREFU CHA NENO JUA...KUKUZA ELIMU NDIO LENGO LETU..MUNGU IBARIKI TAMBAZA.

    MISUPI ..PLEASE BRING MORE PICS ZA TAMBAZA..UMENIKUMBUSHA MBALI MNOOO....NIMEFURAHI MNOOO MISUPUU KUMBE SAA NYINGINE HUWA UNA AKILI..

    ReplyDelete
  9. Huo ni mti wa krismasi michuzi au? Mbona huku haujulikani kabisa au ni mimi tu...maana huku krismasi ina miti yake ambayo huwa ni ya kijani kilichokolea na huwa ni inaota style ya ashock tree but inakuwa ni mifupi sasa ukisema hiyo nix-mas sikuelewi kabisa...!! Au imebatizwa na wala vumbi maana hawachelewi kuvipa vitu majina...

    ReplyDelete
  10. you almost made me cry!!!!them goooood all days samaki wa kukaanga na ugali. stay focus everybody

    ReplyDelete
  11. Mimi naikumbuka Tambaza ile ya 1998-2000 intake hiyo ndio ilikuwa na kina John Mnyika, Amina Chifupa, Pamela Bomani [wote hawa form five yao 99], Saidi Yakubu wa BBC, Vero wa ECA, Goddy Kirumbi, Amri Shindo [CRDB], na Eric Winston Massanja ha Headmaster wetu Mchizi Kaaya.

    Ndio mwaka tulikuwa na WU TAMBA.

    Elia Yobu ''protocol'' upo wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  12. Duh Longi taimu kichizi, we mwanatambaza umeniua sana, unakumbuka ATC ha ha Father K unamkumbuka? Nangurukuku Samiti unakumbuka? samiti ya madarasa ya fom thrii na foo. Anyway sina mengi wacha nichukue zangu ATC kuna mechi na Azania Leo, halafu maktaba miting pointi na videmu vya zanaki.

    ReplyDelete
  13. jaman cjui niseme nini maana nimekumbuka mbali sana...i wish i cud turnback the hands of time...yani i had fun ndani ya Tambaza from 2000-2002...tukiwa na kichaa wetu kaaya(head master)..am so happy to see this school again..na hapo palipopaki gari ndio assembly yetu..wanatambaza woe nawapa holla popote walipo.

    ReplyDelete
  14. Michuchu umenikumbusha mbali sana!
    Mie nimesoma hapo 1979-1982.
    Nimesoma darasa moja na "PAPA MSOFE" a.k.a Geofrey Marijani Msofe.
    Namkumbuka Mzee Yusufu alikuwa mpishi wa shule akitupikia Viazi na nyama, tukila baada ya kutoka shule kwa wale wanaobaki kusoma.
    The Jacksons, Super Mnyanyuo, Shimo Group na Thae Bee Gees mko wapi?

    ReplyDelete
  15. Aisee umewakuna sana jamaa wa Tambaza,

    sasa ili ku-equalize mambo toa basi na ya Azania enzi hizo hakukua na mademu wala nini, ilikua kisela mchana tunakamua Chipsi dume na juice kwa Mkemia.

    Enzi hizo Master alikua Mzee Kwayu na Second wake Mkongo.
    Nidhamu alisimama Mchwa a.k.a Mzee wa Vibao vya ghafla wakati academic alikua mzee mwenyewe Christian.

    Namkumbuka a.k.a FUVU mwalimu wangu wa Namba form two bila kumsahau Mwl Mugituti alinifundisha Commerce.

    Hiyo ilikua ni miaka ya 1996
    Alikuwepo Tokyo na Suruali zake za Dukan enzi hizo kwenye History, hakua mtaalam sana na ndio maana somo lake la history sikulipenda mpaka leo.

    Aisee nakumbuka nilitesa sana namba anzi zangu za O-level mpaka class walikubali, ingawa masomo mengine niliburuzwa.

    Aisee Misupu tuwekee bwana ya Azania na sie tujikumbushie

    ReplyDelete
  16. MwanaTambaza2 hapo juu nawakubuka hao wote. Mimi nimesoma Tambaza "O" Level miaka ya themanini. Nakumbuka enzi zile nikienda kidato cha kwanza lazima uwe na kile kitabu kinaitwa "Learning Through Language". Lakini lazima unakijaladia kwasababu hutaki ma-binti wa Zanaki Secondary wakione ukiwa umepanda basi la UDA. Tulikuwa tunashindana kusoma Novel za James H. Chase and others. Na kubadilishana miziki mipya kutoka mtoni palivyokuwa panaitwa wakati ule... enzi zile ukiwa na Tape ya "Chrome" alafu iwe na miziki mipya ulikuwa unaonekana wa maana sana lakini unaangalia wajanja wasibadilishe mkanda wakiiazima. Na Namkumbuka mwalimu wangu wa English Mr. Khan.. alikuwa noniino yule. Waalimu wengine ni akina Mwaipopo (hesabu), Mchwampaka (History). Ms. Juma (Biology, alikiwa anapendeza sana darasani). Kiwinga (kiswahili, kada wa chama kipya yule, I mean CCM).. I can go on and on. Enzi hizo ukishika kile kitabu cha Biology kinaitwa Modern Biology ukijikita Tanganyika Library, shule inapanda. Sikuhizi vijana mpaka wapigwe "tuition"/coached ili wafauli masomo. Siwezi kuacha kuzungumzia Tambaza bila kutaja "Duka Shop" lilivyotutunza. Tukicheza kandanda na Kinondoni(muslim)Secondary ujue sikuhiyo kosovo litakalo zuka sio la kawaida. Weekend tunafanya picnic "Ngazi" moja, wasio jua Ngazi moja It is nice natural ocean cave karibu na ilipojengwa SeaCliff. Anyway, the bottom line we had a lot of fun and got a very good education at the same time. I am in touch with a lot of my classmates from my "O" level days at Tambaza most of them are doing so well from Business men now Tanzania and South Africa, Practising Medical Doctors in Europe, Engineers in America, Institution leaders in TZ. I am very pround of the experience I garnered at Tambaza "O" level Secondary School. Lakini watu mtaani walikuwa wanatuita watukutu. But looking back, all I can say is that we were way ahead of the society at the time as far as what is expected of a secondary school student.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...