mzee ruksa akiwasili makao makuu ya daily news na habari leo mtaa wa samora leo akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kutimiza mwaka mmoja kwa gazeti la kiswahili la serikali habari leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. kaka michu ebu achana na besidei za magazeti tumuvuzishie haka kahabari kanakovunjika(breaking news ka balali kujiuzulu.

    ReplyDelete
  2. namsifu hyu jamaa mzee wa ruksa baada ya kuingia madarakani tu nikapata visa kuja ugaibuni kanitoa kwenye vumbi kweli ningebaki huko ningekula vumbi hadi mdomo ungepauka kama wabongo walioko tz,na bado mtakura vumbi hadi matumbo yajae minyooo michuzi mjomba njooooooo huku achana na bia na chakula ambacho akina tbs hahahahahahaha wala vumbi

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja wa Habari Leo ingawa mmefanya kimya kimya mlianza kuitangaza habari hii jana tu ili kuanua ngoma juani, leo mmekula wenyewe.
    Mmeleta tofauti na changamoto kubwa.
    Wakati mwingi wasomaji tunataka habari za kawaida sana zinazotuhusu ambazo mara nyingine huwa tunazikosa.
    By Maganga Feruzi DSM

    ReplyDelete
  4. Mzee Ruksa ana miaka 80+ lakini bado anadunda bila matatito. Wengine inabidi tujifunze kitu kutoka kwa huyu mzee.

    ReplyDelete
  5. Huyu bwana ana Afya Nzuri sana,ataishi miaka mingi
    Hongera Mwinyi

    ReplyDelete
  6. Baada ya Kikwete Ni Mbowe
    Nafahamu wengi watasema mda bado na ni mapema sana kuwa na mjadala wa aina hii. Na pengine, watetezi wa Serekali ya awamu ya nne watanishambulia kwa kusema sikupaswa kuhukumu utendaji wa awamu ya nne sasa,kama ilivyozoeleka watasisitiza tuendeleze utamaduni mbaya wa tuwape “mda” na bado “mapema”. Msemo wa wahenga wa “nyota njema huonekana asubui” si mtazamo rafiki kwa CCM na serekali yake.

    Naandika haya ili mjadala uanze mapema, tuepuke yaliyotokea mwaka 2005. Mjadala ulikuja ukiwa umechelewa sana, tulichoamabulia ni kuchafuana miongoni mwa wagombea, bila kusikia maelezo ya kina juu ya mikakati na misimamo ya wagombea katika kulikwamua taifa toka katika makucha ya umaskini ambao sehemu kubwa ni wa kujitakia. Baada ya hapo, zikabuniwa taswira na sanaa za hali ya juu kumtengeneza “masihi”. Sanaa hizi ziliwalewesha watanzania katika kipindi muhimu cha uchaguzi. Hatukajadili mambo katika uasili wake,hatukutathimini uwezo wa “masihi” na pengine rekodi yake ya nyuma. Watu walijawa na ushabiki wakiwemo viongozi wa dini wakasahau shida na umaskini wa waumini wao, kwa kilevi cha sanaa, wakawasaliti waumini wao na kusujudu kwa sanamu ya kuchongwa!

    Leo hii naanadika haya, ili tuanze mjadala wa kweli na halisi sasa. Tuwatambue watarajiwa,tuwasaili,tuwakosoe na tuwajenge. Siasa za masihara hazipaswi kuwa na nafasi wakati taifa letu linaloendelea kulika kila uchao. Uzembe,uvivu,kutokuwa na muelekeo na ufisadi viaendelea kushamiri katika ardhi yetu iliyobarikiwa rasilimali ngingi sana.

    Makala haya yanajadili kilichodhahiri. Yanamjadili mtu ambae amebeba dalili zote za kumrithi Jakaya Mrisho Kikwete raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Nitachambua na kutetea minong’ono inayoendelea mitaani na hatimae kuthibitisha uhalisia wa yanayosemwa. Leo tunamjadili Freeman Aikaiel Mbowe mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).Nitaonyesha mazingira kazaa ambayo yanazidi kusafisha njia ya Tanzania mpya chini zao la uhuru,mtu huru.

    1. awamu ya nne Kushindwa kukidhi matarajio
    Jakaya ya Kikwete akisaidiawa na kundi kubwa watu toka sekta mbali mbali ambalo badae lilikuja kujilikana kama wanamtandao, waliweza kuibua matumaini makubwa sana miongoni mwa watanzania. Mengi yalisemwa na kuandikwa hatimae sehemu kubwa ya jamii ikaamini Kikwete ni mpinzani wa ndani.

    Inavyoelekea, washauri na wasaidizi wake walibuni taswira ya mgombea wao kwa unagalifu mkubwa wakitambua watanzania walikuwa wamekwisha choka na utawala ulioshindwa kuwaletea maendeleo. Ndipo walipokuja na ari mpya,kasi mpya na nguvu mpya.Lengo la ujumla lilikuwa kuwaonyesha watanzania upya ndani ya CCM iliyochakaa kimtazamo na kimkakati katika kuliletea taifa maendeleo.

    Ni kweli kwamba Kikwete ana miaka miwili na ushee kumaalizia muda wake wa kukaa ikulu au wengi wangependa tuaamini ni awamu ya kwanza jambo ambalo bado litaamuliwa na wanachi kunako 2010, mpaka sasa Kikwete ameshindwa kabisa kuyaishi maneno yake.

    Nyota isiyo njema imeanza kuonekama asubui. Bajeti ya mwaka 2007/2008 iliyopitishwa na bunge hivi karibuni ni kiashario cha ukomo wa uwezo wa utendaji wa serekali ya Kikwete. Wakichochewa na uvivu na ukosefu wa ubinifu kwa mara nyingine tena, serekali ya awamu ya nne imetengeneza bajeti kwa kuangalia vyanzo vile vile vya mapato, kodi imeendelea kuongezwa kwenye maeneo kama soda,sigara, bia ma mafuta kana kwamba Tanzania tuna vyanzo vichache. Kibaya zaidi serekali imekataa kupokea changamoto na kuwa na ujasiri wa kuchukua bajeti mbadala iliyowasilishwa na kambi ya upinzani. Bajeti ya wapinzani ni ya kimapinduzi kwa kuwa inaonyesha wanatanzania nani haswa anapaswa kuwa katika uongozi. Ni bajeti ambayo inalenga kutomkamua mwananchi yenye ubunifu katika kuhakikisha maisha bora kwa kila mtanzania. Baada ya bajeti mbovu, msingi mbaya umewekwa na kuonyesha muelekeo wa serekali ya Kikwete. Ni jambo liliodahiri kwa wananchi watapigigika zaidi katika mwaka huu wa kifedha. Kikwete kama bado ana nia ya kuwa mshindani mzuri mwaka 2010, atalazimika kuwa na bajeti wa kuwapoza “majeruhi” wengi wa bajeti hii katika miaka ya fedha ya 2008/2009 na 2009/2010, hatiame taifa litawasili katika uchaguzi tukiwa palepale au tumerudi nyuma kidogo mwaka 2005.

    Tukiacha bajeti, kikwete ameshindwa kujitofautisha kabisa na tawala zilizo pita kutuletea mradi wa Richmond ambao hivi karibuni umesafishwa na TAKURU, imefanya Kikwete asiwe tofauti sana na waliomtangulia kwani mradi huu ni pacha wa IPTL. Wengine tumeanza kuelewa dhana ya kupokezana vijiti na ile ya kuendeleza “mazuri” ya awamu iliyopita.

    Pamoja na mradi huu mbaya ambao ulibuniwa taifa likiwa na wakati mgumu sana, ripoti ya mkaguzi mkuu imeonyesha tunapoteza fedha nyingi sana kutokana na uzembe.Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa zaidi ya majibu laini ya waziri mkuu bungeni kwamba hela ambazo zimetajwa katika ripoti malezo yake yatapatikana hapo badae.Kwamba ni suala la kuwasilisha vielelezo tu! Muda utasema.

    Baraza kubwa sana la mawaziri liliowahi kutokea katika historia ya nchi yetu lilibuniwa na Kikwete. Yeye alitetea uamuzi huu kwa kusema kuwa ana ajenda nyingi. Tulijiuliza je wakija watu wana ajenda mia itakuaje? Mapaka sasa baraza hili mzigo mkubwa kwa walipa kodi limeshindwa kabisa kuonyesha ufanisi wake.Limekwama.

    Kuwa na baraza kubwa kumendelea kupeleka fedha nyingi kwenye utawala badala ya miradi ya maendeleo ambayo kwa uhakika ndio haswa yangesaidia kuwaletea watanzania maisha bora. Wakosoaji wa serakali ya Kikwete akiwemo Mbowe ambae kwa kadri mambo yanavyoenda ndie mpinzani wake mkuu walisema inegukuwa ni vizuri Kikwete angeunda serakali ndogo yenye ubunifu ikiwa na mkazo katika miradi ya maendeleo.

    Mazingira haya yanazidi kumpa fursa nzuri zaidi Freeman kumbadali kikwete kutokana na Kikwete kuendelea kuonyesha dalili za kushindwa kukidhi matarajio ya watanzania walio wengi. Tofauti Kubwa inajitokeza kati ya Mbowe na Kikwete ambapo kupitia ilani ya CHADEMA alibainisha vipaumbele vitano tofauti na serekali ya kikwete ambayo inahangaika kujaribu kufanya kila kitu katika mda mchache na rasilimali chache.Mwisho wa siku hakutakuwa na mafanikio makubwa yatakayokuwa yameonekana. Kwa kuwa mkakati wa Kikwete wa kuwa na vipaumbele vyote umeshindwa vibaya, mtazamo wa wengi sasa ni mbadala wake,kwamba inawezekana Mbowe ndio alikuwa sahihi zaidi.

    Freeman Mbowe amewahi kumsihi Raisi atulie ofisini na kulipa taifa muelekeo lakini wapi. Tunashuhudia gharama kubwa za safari za hapa na pale ambazo mafanikio yake yanabaki katika midomo ya Kikwete na Lowasa. Taifa linaendelea kuumizwa na misururu ya mikutano ya Ngurdoto na mmoja wa Dodoma. Udhaifu wa kiuongozi wa Kikwete kwa upande mmoja na majibu mbadala anayayatoa “raisi Kivuli” yanazidi kumpambanua Mbowe kama mtu anae enea zaidi katika nafasi hiyo.


    2. Kukorongaka kwa CCM na Kupoteza asili yake
    Katibu Mwenezi wa CCM aliwahi kunukuliwa bungeni akisema kuwa;sasa hivi hakuna itikadi ni shughuli tu. Alikuwa sahihi,CCM ya leo chini ya Kikwete ni shughuli mtindo mmoja. Ni kokoro liliokusanya watu wenye lengo moja tu, kutawala.

    CCM ya leo si ile ya Nyerere na hata yeye mwenyewe alikiri hilo katika kitabu chake ungozi na Hatima yetu. Kwamba CCM si chama cha kijamaa tenaingawa viongozi wanaendelea kuwadanganya watanzania kwamba CCM bado ni chama cha kijamaa. Mtazamo kama huu pia uliwahi kusisitizwa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Hayati Horace Kolimba aliposema CCM haina dira.

    Viongozi wa CCM wamekosa ujasiri na uwezo kuukabili ukweli huu. Ni chama kisicho na itikadi inayoeleweka. Ni chama cha shughuli, jambo la kusikitisha ni kwamba; alama kuu ya utambulisho wa CCM si tena itikadi yake ya ujamaa na kujitegemea bali nyimbo za mhamasishaji wake Mheshimiwa John Komba.Ukiacha nyimbo na rangi hakuna jambo la wazi na linaloeleweka kama kitambulisho rasmi cha CCM.

    Mtazamo huu wa Chama shughuli umeathiri sana uwezo wa chama kusimamia serekali yake.Imefika hatu ilani ya chama inatengenezwa kwa kudesa miongozo mbalimbali ya serekali. Hatimae tumekuwa na chama kisichokuwa na mijadala mizito ndani ya chama na kutokuwa na uwezo wa kukabili changamoto. Yanayoendelea katika kipindi hiki ni ushahidi tosha wa maandiko haya. Kamati ya wabunge wa CCM chini ya uenyekiti wa Edward Lowasa imejijengea utamaduni hasi wa kudhibiti wabunge wake kuikosoa serekali ya CCM.Jambo hili lina athari mbaya sana kwa taifa. Wabunge wa CCM wanalamika kisha kupitisha bajeti na misuaada mingi ya serekali hata kama inaumiza wanachi na kuhujumu maslahi ya taifa.


    Matokea ya CCM kuwa chama zezeta kimtazamo na kiitakadi yamepelekea kuwa na wanachama wasioweza kuwa na msimamo inayoeleweka. Wakati wa kampeni za kutafuta wagombea urasi wa CCM ukiacha Iddi Simba hakuna mgombea ambae aliweza kuonyesha misimamo yake binafasi wote walikuwa wanasema wanaisuribiri ilani ya chama na kwamba wataendeleza mazuri ya awamu ya tatu. Huwezi kuiona mijadala ndani ya chama.Hakuna itikadi na muongozo matokeo yake mijadala ya kuibua fikra na sera nzuri hamna. Leo hii tunajua Iddi Simba anaamini katika sera yake ya uzawa.Simba anaweza kusimama pekee yake na kujitambulisha na kujadiliwa kwa yale anayoyaamini.Kwa ujumla,CCM ni mkusanyiko wa watu ambao wanataka madaraka kwa kutumia ngazi ya dola wakiwa wamekosa ono. Wengi hawavuki mstari mbele ya matamanio binafasi.

    Leo kila mtu anaetaka kuwa mgombea wa uraisi baada ya Kikwete akili yake ni kujenga mtandao. Hakuna suala la dira au mkakati wa kutoa suluhisho kwa umaskini wa chi. Shughuli ni moja tu kuwa raisi.

    Wakati hali hii ya kusikitisha na kutisha inaikabili CCM, CHADEMA chini ya uongozi makini wa Mbowe, hivi karibuni wamezindua tumaini jipya. Wamefanikiwa kufafanua vizuri sana itikadi yao ya mrengo wa kati na falsafa ya nguvu ya umma.CHADEMA ni kinyume cha CCM. Ni mbadala wake. Kwa kuongoza kwa mafanikio chama kinachoendeshwa kisasa na chenye ono ni chapua jingine kubwa kwa mwenyikiti wa taifa wa CHADEMA miongoni mwa watu wengi makini.


    Ukuaji wa CHADEMA na uwezo wa makada wake
    Tofauti na baadhi ya vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa na migogoro ya hapa na pale CHADEMA kinabakia kuwa chama makini chenye demokrasia ambacho mpaka sasa kimefanikiwa kuwa na wenyeviti wa tatu.Kuweza kuwa na wenyeviti watatu ndani ya miaka 15 ya uhai wake ni kielelezo cha demokrasia na ukomavu wa kisiasa wa CHADEMA.


    CHADEMA ni chama kinajitoufatisha kimuondo na kisera na vyama vyote vya siasa nchini.Hali hii inakipa uhalali na upekeee wa kuwa chama mbadala.Wakati wa kumtafuta mgombea wa urais ndani ya chama hicho.Walikuja na mfumo wa kikanda ambapo wagombea uraisi wa CHADEMA walizunguka katika kanda za nchi katika kutafuta mgombea wa chama.Ubunifu huu uliwezesha ushiriki wa wanachama wengi kuchagua mgombea wa chama na kupunguza uwezekano wa kikundi kichache kuepika maamuzi ya chama.

    Wakati wa uchaguzi CHADEMA iliendelea kujitofautisha na vyama vingine kutokana na muundo wa ilani yake ya uchaguzi ambayo ilibainisha vipaumbele vitano ikielezea maeneo ambayo ingeyatilia mkazo iwapo ingepewa ridhaa ya kuunda serekali.Ilani hii ni tofauti na ile ya Chama cha mapinduzi ambayo ilikuwa ni mkusanyiko wa matatizo yote ya nchi. Tofauti kati ya mgombea wa urasi na CCM ziliongezeka pale mgombe wa CHADEMA alipokuwa makini kufafanua na kutotoka nje ya vipaumbele vilivyoanishwa katika chama chake ihali mgombea wa uraisi wa CCM alikuwa na ahadi za ilani na ile alizoziita za papo kwa hapo au wengine wanaziita ahadi za VODAFASTA. Sera ya majimbo ilikoleza tofauti ya CHADEMA na CCM.Kwa muktadha huu, umaarufu wa Mbowe na kukubalika kwake unakuwa sambamba na Chama anachokiongoza.


    Uwezo wa viongozi wa CHADEMA unaondelea kuonyeshwa na watu kama: Katibu Mkuu wake Dr. Wilboard Slaa, Chacha Wangwe,Halima Mdee,Zito Kabwe,John Mnyika na wengine unatoa ushahidi wa chama cha watu wenye uwezo ambao wana uwezo wa kushika dola tofauti na propaganda zinazoenezwa na makada wa CCM. Hali hii inakolezwa kwa kuwa chama pekee cha upinzani chenye wenyeviti wawili wastaafu ambao inaendelea kuvuna ushauri toka kwao, hawa ni Mzee Edwin Mtei na Bob Makani.


    Uwezo wa Mbowe na Utendaji wake
    Upo ushahidi wa kitwakwimu wa uwezo wa kiongozi wa Mbowe kama kiongozi wa chama. Baada ya kushikia madaraka ya unyenyekiti wa taifa wa CHADEMA amefanikiwa kukuza chama kitaasisi na kukiongezea makada wengi.

    Chini ya uongozi wa Mbowe CHADEMA imeweza kupata ongezeko mara mbili la wabunge na madiwani. Mbowe alikabidhiwa chama kikiwa na wabunge 5, yeye pamoja na safu yake ya uongozi wamefanikiwa kuwa na wabunge 11 pamoja na vikwazo vya kidemokrasia viliopo nchini.

    CHADEMA ilisimamisha kwa mara ya kwanza mgombea wa uraisi na kushika nafasi ya tatu. Mbowe alijotofautisha sana viongozi wengine wa upinzani kwa kukubali kwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo ya uraisi. Kwa kuwa tangu anagombea uraisi alijua kabisa anagombea katika uwanja usio sawa hakuna mantiki katika kugomea matokea baada ya kukubali kushiriki uchaguze ule. Kwa kufanya vile alijijiengea taswira chanya miongoni mwa watanzania. Yapo maelezo kuwa watu wengine walimtazama Mbowe kama raisi wa badae, walimpigia Kikwete huku wakimtazama Mbowe kama raisi anaefuata.

    CHADEMA kimekuwa chama kinachojiendesha kisayansi na kitaasi. Si chama mtu, mwenyekiti wake amakuwa masomoni na bado kimeendelea kujiendesha kwa umakini mkubwa. Kimefanikiwa kutoa matamko mbadala juu ya uchaguzi mkuu, rushwa na mengineyo.

    Mbowe na viongozi wenzake wemeweza kufanya ziara za chama mikoani kuondokana na dhana kuwa vyama vya upinzani ni vyama vya uchaguzi. Ziara za mbowe za kushukuru wanachi na muendelezo wa programu kama CHADEMA ni msingi zimeendesha kuwahakikishia watanzania umakani wa CHADEMA.

    Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA ameweza kufafanua vizuri malengo na ono lake kwa maandishi kwa kuandika makala na machapisho mbalimbali. Tangu wakati wa Nyerere, hatujawa na viongozi wanaoandika na kufafanua mawazo na mikakati yao. Maandiko yake yanatupa rejea nzuri za katika kumjadili kama kiongozi.

    Tofauti na viongozi wengi, mbowe ameweza kujichanganya vizuri na viongozi wengine wa kisiasa. Uamuzi wake wa kwenda kutembelea kamba ya Taifa stars na kuchaingia pamoja na kuhudhuria mechi kati ya Taifa Stars na Bukinafarso imetoa upande wa pili wa Mbowe kama mtu anaethamini michezo na juu ya yote mzalendo mwenye kutanguliza maslahi ya taifa.

    Inaaminika katika wanasiasa waliopo hakuna anaemkaribia Mbowe katika uwezo wa kushwahishi,kuzungumza na kuvutia hadhira.Sifa hizi ni muhimu sana kwa kuwa na kiongozi anaweza kulipa taifa muelekeo katika kufikia dira ya kimaendeleo. Ninao marafiki wengi ambao hawakumkubali moja kwa moja na wakihoji uwezo wake kama mgombea uraisi, mtazamo wao ulibadilika ghafla baada ya kuwa wamehudhuria mikutano yake au kuwa wamezungumza nae ana kwa ana. Walikuja kubaini ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo na kutoa masuluhisho.

    Kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza, kusimamia na kuchochea ukuaji wa chama chake , uwezo wa kuandika na kutetea mawazo yake vinamfanya kuwa mmoja wa viongozi adimu ambao taifa limewahi kuwapata katika miaka ya karibuni.


    Ongezeko na muendelezo wa kazi za Asasi zisizo za Kiserekali
    Asasi za kiserekali zinafanya kazi nzuri ya kuelimisha umma na kuimsha na kuhamasisha serekali kutekeleza uwajibu wake. Hali hii nazidi kuwajengea uwezo wa wananchi kuchambua na kufuatilia mambo yenye maslahi ya kitaifa na wakati huohuo kuanika udhaifu wa serekali na hatimae kuwapa wanachi kinga dhidi ya propaganda za CCM.

    Wabunge na viongozi wa CCM wameanza kuweweseka na hali hii kufikia hatua ya kutishia uhai wa asasi zisio za kiserekali mathalani matukio ya hivi karibuni dhidi ya HAKIELIMU.

    Baada ya muda mfupi sehemu kubwa ya wananchi watakuwa na uwezo wa kupambanua pumba na mchele. Hakutakuwa na nafasi ya wao kupokea malezo ya mafiga matatu au ahadi za papo kwa hapo. Komba ataimba na kutoa ngonjera na baada ya hapo wananchi watataka kuskiliza sera nzito zenye lengo la kukwamua kuondokana na umaskini.

    Kwa sasa CCM haina uwezo wala sera nzuri kama CHADEMA hali hii itaipa nafasi nzuri zaidi CHADEMA kutwaa madaraka.

    Haja ya Kuongeza idadi ya wabunge toka kambi ya upinzani
    Ni jambo li dhahiri kwamba tuna bunge dhaifu sana lisiloenea vizuri katika kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia serekali ipasavyo. Hali hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na uwezo mdogo wa sehemu kubwa ya wabunge na wabunge wengi kuwa wa chama kimoja, matokeo yake ni bunge kugeuka mhuri wa serekali.

    Hali hii imejenga kiu ya jamii kuongeza wabunge wengi zaidi toka upinzani katika bunge lijalo ili kulipa meno bunge. Huo ndio utakuwa mwisho wa bunge kuwa sehenu ya tambo za kisiasa na mawaziri kutoa majibu fyongo dhidi ya maswali ya wabunge.

    Hali hii inatarajiwa kunufaisha zaidi CHADEMA kama moja ya vyama vya upinzani kutokana na kazi nzuri ya wabunge wake kama Zito Kabwe, Wilbloard Slaa,Halima Mdee na Chacha Wangwe. Hali hii pia itachagizwa zaidi na ongezeko la umarufu wa CHADEMA kama chama mbadala.

    Pamoja na kiu ya wananchi ya kulipa wabunge meno, bado wananchi watakuwa na sababu ya kuwa na wabunge wengi zaidi wa upinzani kutokakana na uwezo mzuri ulionyeshwa na na kambi ya upinzani katika mjadala wa bajeti unaoendela. Bajeti mbadala imejenga taswira chanya kwa wabunge wapinzani kama viongozi wenye uwezo wa kuiongoza serekali kwa ubunifu,ufanisi na uadilifu mkubwa.

    Istoshe, mnamo 2010 CHADEMA itaingia katika uchaguzi ikiwa na ushahidi wa kiamendeleo katika halmashuri ya karatu iliyoshikiliwa na CHADEMA. Hata raisi Kikwete amekiri juu ya mafanikio ya Karatu na kuzitaka halamashauri nyingine ziige mfano. Hapo wananchi watakuwa wamepata dokezo la CHADEMA Kama chama tawala.Itakumbukwa kwamba; jimbo la karatu limeshikiliwa na CHADEMA kwa vipindi vitatu mfululizo na hivyo Slaa kuweka rekodi kama mbunge pekee wa upinzani alieweza kushikilia jimbo lake kwa miaka mitatu mfululizo.


    Ongezeko la matumizi ya Teknolojia katika kusambaza habari
    Pamoja na hofu ya serekali ya CCM dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari, maendeleo ya teknolojia ni chachu muhimu kwa wananchi kupata habari. Leo hii CCM haina uwezo wa kudhibiti taarifa na mijadala katika simu za mikununi na kwenye intaneti.

    Ukosefo wa habari za upande wa pili imekuwa silaha muhimu ya CCM kujiimarisha. Ongezeko la matumizi ya intaneti na simu za mikono kunatoa mirija mizuri ya habari mbadala kupitisha kuwawezesha wananchi kuchambua vizuri maelezo yanaotolewa kupitia mfumo rasmi wa habari.

    Usambazaji wa habari unaokosa serekali ya CCM unalainisha ngome ya CCM na kuupa nguvu zaidi upande wa Upinzani. Imekwisha zihirika kuwa kwenye mijadala huru na ya wazi CCM haiwezi kusimama. Kwenye inteneti na simu za mikononi hakuna dola,ndio eneo pekee ambalo CMM inalalamika,huko hakuna tume ya uchaguzi wala magazeti ya chama na serekali.

    Ongezeko kubwa la wapiga kura wapya
    Chaguzi za 2010 na 2015 zitaingiza maelefu ya kizazi kipya katika upigaji kura. Hichi ni kizazi kipya ambacho hakikuenda JKT na wala hakina utii kwa chama. CCM itakuwa inapanda mlima kushawishi kizazi kipya chenye kiu ya mabadiliko.

    CHADEMA kitaswira tayari kinaonekana ni chama cha kizazi kipya. Kuwa na safu nzuri ya vijana kati safu ya uongozi inakiweka katika nafasi nzuri kuvuna wapiga kura wapya katika mwaka 2010 na 2015.

    Hitimisho
    CCM wamekwisha tambua uwezo na nguvu za Mbowe, ndio maana kuaniza wakati wa uchaguzi kila anachosema CCM inajaribu kujibu. Hatujasahau jinsi Mkapa alivyokuwa anashambulia Helkopta,Kikwete nae akijaribu kupangua hoja nzito za utetezi wa sera ya majimo ambazo kimantiki alishindwa kabla ya Mzee Kingunge kujiabisha kwa kumtaka Mbowe asimtaje Nyerere katika hotuba zake, kwa kuwa Nyerere ni mali ya CCM!

    Wakati wa ziara za kuwashukuru wananchi tumeonna CCM ikihangaikakujibu hoja za mbowe,Makamba,Mwanri na hata taasisi za kiserekali zikipoteza fedha za umma kujaribu kujibu mawazo mbadala ya mbowe.

    Kwa kumaliza naomba niwe miongoni mwa mtanzania wa mwanzo kabisa kuzungumzia uwezekano wa kuwa na raisi Freeman Aikael Mbowe.

    ReplyDelete
  7. Gazeti la Serikali !DUH! Mimi mbeba maboksi fulani kwa muda , naombea kuwa magazeti haya ambayo siyajui , yana julisha, Bro Michu , unanielewa?

    ReplyDelete
  8. Aikaeli Mbowe, kama anaipenda TZ, mbona kakimbilia Ulaya kusoma? Kwani vyuo vyetu havithamini? Mbona vinatoa shahada za juu hata kushinda hiyo iliyompeleka Uingereza?

    Chadema, Chama cha siasa, ama chama cha ushemeji shemeji?

    Chadema, Chadema...kwani CCM haina watu mbali ya Kikwete?

    CCM ina "reservoir" kubwa ya kuwapata viongozi, pamoja na ujanja wa kupiku sera za vyama vidogo vidogo na kuvitangulia!

    Ngoja Kikwete amalize wakati wake utaona!

    Hivi wengine mnafikiria kuwa CCM ikitoka, basi ndio "panaceas" za maendeleo zitaingia TZ?

    Chadema = Chama sawa na itikadi za wakina Republican na Conservative wa Uingereza wafariji wake?

    Vyama hivyo vidogo vidogo havina hata sera = tofauti za "personalities". Inawezekana kuchuka zaidi ya miaka 50 hivi kukua na kuweza kuing'oa CCM - wengi tutakufa tukiongozwa na chama tawala cha sasa, CCM...

    CCM, OYEEEEEEEEEEEEEEEEE!

    ReplyDelete
  9. Huyo Mbowe nani ampe URAIS Tanzania, yaani hata sikusoma hicho ulichoandika nilichefuka kwa sababu ni ndeefu kama ulikuwa unaandika risala ya wapi sijui. Fungua blogu yako!!1

    Jamaa unaota kweli, ni mchaga nini? Wachaga waliota Mrema Raisi wa Inji hii wee mpaka basi ndoto ikafilia mbali. Sasa mnaota kuhusu huyo Mbowe aliyepewa uwenyekiti wa Chadema na mkwewe? Hebu angalia kwanza idadi ya wabunge wa kuteuliwa wa Chadema (viti maalum au kwa msemo mwingine, wanawake) ni wangapi wachaga na wangapi kutoka sehemu nyingine? Hapo ndio utaijua misingi ya Chadema ilikolalia. Ukimtoa huyo Zitto Kabwe wengine wootee mhuuu!!!

    ReplyDelete
  10. WaTZ kwa kupenda Lotto na michezo ya kuigiza!! Siwawezi, sijawahi kuona uchumi wa nchi yoyote ukipaa ndani ya miaka 2. Ukizingatia kipindi kilichopita walikuwa wanadeal na Macroeconomics na imewachukua miaka kumi na bado hali ndio kwanza inatengamaa. Sasa hiyo microeconomics ambayo waTz wataona matunda yake ndani ya miaka 2 ni ya ajabu. Watu wamekaa wanasubiri maisha bora badala ya kuyatafuta yote kutaka dezo. Inachotakiwa hao CCM waweke misingi ya kuwawezesha watu kupata hayo maisha bora. Sio watu warudi kule kwenye kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.

    Hata hiyo Amerika, na Nchi nyingine zilizoendelea hazikuendelea ndani ya miaka 2!! Ingawa watu watasema tulipata uhuru miaka 46 iliyopita, je mna uhakika tulipata uhuru wa kiuchumu au wa bendera? Hao hao wanaompa Mbowe pesa apate Urais na wao wana malengo yao, neocolonialism imerudi kwa kasi kubwa.

    Kwa hali ilivyo Bongo hata hao waliopewa hiyo mitaji kupitia Saccos itakuwa imeishia kwenye mambo hata ambayo haya kupangaliwa, ili uweze kutoka lazima na wewe ujitoe, kama unafanya biashara basi ufanye biashara kweli sio ukipata faida kidogo unakula mpaka mtaji. Kama unafanya kazi ufanye kazi kweli, tushukuru mungu nchi yetu unaweza kutoka hali moja kwenda nyingine nchi nyingine zenye caste system hudhubutu na wala hupewi hiyo nafasi. Kwa mtindo huu tulionao Tz hata akija Masihi mwenyewe kutuongoza bado hatutatoka katika hali tuliyomo kwa sababu mawazoni na fikra zetu hatujaamua. Siku tukiamua na umaskini utaondoka.

    ReplyDelete
  11. mzee wa watu huyo, hana makuu kabisa, wala chuki na mtu, ataheshimiwa daima na wote, aliofanya nao kazi mpaka sasa, tunakupenda sana mzee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...