Washiriki waliokuwemo katika mkutano wa zaidi ya masaa sita kujadili na kupitisha katiba mpya ya Jumuiya Ya Afrika Mashariki London, jumapili iliyopita. Toka kushoto waliosimama: Francis Busingye (Uganda), Victor Ngabu,(Rwanda) Nina Shimimana,(Burundi) John Bunyeshuli,(Rwanda) Andrew Fatooza,(Uganda) Aida(Uganda). Waliokaa: Alinda Annet(Uganda), Freddy Macha(Tanzania), Edson Muhanguzi (Uganda) na Mariam Kasangaki (Uganda, mbele kabisa). (Picha na Lilian Zawango mshiriki toka Uganda).
John Bunyeshuli, mzawa wa Rwanda, Msemaji Mkuu na Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, London (East African Community Networking Association) akiongoza kikao kilichopitisha katiba mpya Jumapili iliyopita. Jumuiya itasajiliwa juma lijalo na kutangaza tovuti yake rasmi punde. (Picha na Freddy Macha)


JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAUNDWA MJINI LONDON BILA WABONGO NA WAKENYA...


Na Freddy Macha

“Hii imekuwa ndoto yangu siku nyingi,” John Bunyeshuli, mwigizaji tamthiliya wa Kinyarandwa ananieleza. Yeye ni mwasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, London ambayo lengo lake ni wananchi walioko nchi za nje kukusanya nguvu, kutafuta namna ya kuondoa umaskini nyumbani.

Jina kamili la Jumuiya itakayosajiliwa karibuni ni East African Community Networking Association (EACNA).

Bahati mbaya toka Jumuiya ilipoundwa washiriki wakubwa wamekuwa Waganda, Warundi na Wanyarwanda tu. Kisa? John analalamika imekuwa vigumu sana kuwakutanisha Wabongo na Wakenya shauri kila aliyeitwa mkutanoni amekuwa anafikiria utajiri na matokeo ya haraka haraka, badala ya kuangalia mustakbali.

“Sisi Waganda, Warundi na Wanyarwanda” anaendelea kufafanua, “huwa tunakutana mara kwa mara kubadilisha mawazo ya kirafiki, kibiashara na kupeana moyo hapa Ughaibuni. Lakini nyinyi wenzetu yaelekea kila mmoja anafanya mambo kivyake vyake. Nimegundua karibuni nyinyi Wabongo mwenzako akikuona unaendelea anajaribu kila njia akuangushe badala ya kukuunga mkono muendelee pamoja. Maendeleo yatakuja hivyo kweli?”

Networking...
Hili neno muhimu sana. Huu ni mtindo wa mawasiliano ulioenea fika nchi zilizoendelea. Ku-network huwa na misingi ifuatayo: watu wa taaluma mbalimbali wanakutana, wanakunywa kidogo, wanakula kidogo, wanasikiliza muziki na kuongelea dili ndogo ndogo. Ni kutokana na mtindo huu ndiyo maana Waganda nchini Uingereza wanaendelea kishenzi. Mabaa mengi, klabu nyingi, maduka na sehemu chungu nzima zinaendeshwa nao. Karibuni baa mashuhuri wanayopenda kuhudhuria Wabongo mjini London , kula nyama choma, Club Afrique (yatamkwa Kifaransa Klab Afrikk sio “Afrikiu” kama wanavyosema baadhi) ishanunuliwa na Mganda.

John na wenzake ni watu wenye moyo sana. Wala si wanasiasa.

Jumapili iliyopita nilikaribishwa kuhudhuria kikao ambacho Jumuiya hii ya EACNA ilipitia katiba na kuchagua wajumbe wa idara mbalimbali. Kati ya kipengele kikuu cha katiba ni kuendeleza miradi ya kielimu, kiafya, kiutamaduni na kiuchumi katika sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki. Ni rahisi kufanya miradi ya aina hii ( na hata kupokea misaada ya kifadhili) ikiwa watu mmeungana kuliko kila mmoja peke yake. Majadiliano yalichukua zaidi ya masaa sita na kuipitisha katiba, kuiangalia tovuti rasmi ya EACNA ambayo itakuwa hewani mara baada ya Jumuiya kusajiliwa karibuni.

Kikao kilisisitiza kuwa EACNA si Jumuiya ya wanasiasa wala haitaki wanasiasa maana mara nyingi hawaaminiki. Inataka watu wanaotaka kuleta maendeleo nyumbani hususan wataalamu.
Ombi walilonipa majirani hawa wetu ni kuwahimiza Wabongo nyumbani na Majuu kujiunga.
Ikiwa unahisi yanakuhusu usisite kuwasiliana na mwenyekiti John Bunyeshuli kwa barua pepe:
Au, Freddy Macha
kitoto2004@yahoo.co.uk.
Fuatilia pia habari zaidi katika blogu hii:
http://kitoto.wordpress.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Na vipi huyo Freddy Macha? Mi nilifikiri ni Mtanzania, kumbe ni "Mbongo"?

    Is it my understanding kwamba "Mbongo" alihudhuria ila "Mtanzania" hakuhudhuria? au ni katika kuifanya issue iwe kubwa?

    After all, vijumuiya nchi za watu vya nini? Kwani wakiishi kata waafrika haitoshi?

    Uk sasa kazi, mara sijui "WAO EMU sijui NYIE EMU" (Kile chama tawala), mara EAC, what next...........????????

    Matabaka, matabaka,kujibagua bagua tu, tu, tuuuuuuu.

    Yetu macho!

    ReplyDelete
  2. Haya mambo ya kuundwa kila iku jumuiya na kila mtu ankuja na lake kwa mie tangu nimeisha hapa London hakuna cha maana nilichokiona katika hizi jumuiya ni ujinga ujinga tu na kutafuta umaarufu watu wankuambia jumuiya ya watanzania nenda umepata shida hakuna wa kukusaidia utaambiwa wewe si mwanachama hizi ni jumuiya za watu kutafuta ulaji na maisha hamna kitu tuwe wakweli.

    ReplyDelete
  3. Mi hata siajelewa,

    Kama hakukua na Wabongo mbona nimemuona Macha hapo kauza Sura vilivyo tu??

    Na jumuia gani ya East Africa katiba ya pitishwa london?? Hiyo nin jumuia huko huko kwao, sisi tunaitambua jumuia ya Kina Kikwete, Mu-7 na Raila Odinga Sorry, i mean Mwai Kibaki

    Na mwisho imesajiliwa huko au hapa Bongo??

    ReplyDelete
  4. Tumetoka kwetu MAHENGE, tukaja DAR ES SALAAM, kucheza ngoma!

    Kaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  5. Watanzania popote pale masuala kama hayo huwaoni,ila waite kwenye kubanjuka na kula kitimoto na beer utawaona na michango watatoa.

    Hongereni Freddy Macha na wenzako

    ReplyDelete
  6. Kachabali inatemeba hapo!

    ReplyDelete
  7. Yale yale yaliyosemwa na hao jamaa huko juu. Sie yetu macho kama kweli mnataka kuleta maendeleo nyumbani muache kupiga kelele za mlango, mfanye kweli mjiunge na wenzenu mlete maendeleo. Watu wa west africa wana jumuia yao na imefanya makubwa, nyie kelele na ubinafsi.

    Haya fanyeni kweli sasa sio kila siku kulalamikia wanasiasa wafanye kila kitu, nafasi ni hiyo umoja ni nguvu!!

    ReplyDelete
  8. Ni kutafuta umaarufu tu wa kukutana na viongozi wetu wanapotembelea hizo nchi. Jumuiya gani ya Africa mashariki wakati hata nchi zenyewe hazijafikia muafaka wa hiyo jumuiya yenyewe? Imarisheni jumuiya za nchi zenu kwanza, kabla ya kukurupukia makubwa.

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli, hizi jumuiya sasa zitatuchosha. Hao hao wanaotaka jumuiya ya EA, Vitu vidogo vya kumaliza ukabila kwenye nchi zao vimewashinda sasa wanataka lijumuiya la EA. Hapo ni maslahi tu ya wajanja wachache ambao wanataka kuwatumia wenzao. Hakuna lolote.

    ReplyDelete
  10. Nanukuu: (Na hata kupokea misaada ya kifadhili)!

    Teh teh teh teh.........

    Nilijua tu, lazima kuna hiden agenda hapa, Asalaaleh.............

    ReplyDelete
  11. I think you should start the East Africans Abroad Association so you include more members, or help the African Unification Front, 2382 Mariana Place , Coquitlam, BC V3K 6S2 , Canada – nini maana ya zote zafanana??

    ReplyDelete
  12. sasa nyie watoro, huko ughaibuni nasikia wengi wenu mnasafisha vyoo na vyombo tuu!!!nimeambiwa wote wanasaidiwa na fitra na zakaa za kiserekali yaani social security,wengi pia nimesikia wanajishughulisha na vidonge vya haramu,usherati,uwizi n.k.(hayupo hata mmatumbi au mdengeleko mmoja kwenye wadhifa maaluna ya maana,
    JAMANI RUDINI KWETU MBEYA!!!

    ReplyDelete
  13. watanzania nyumbani wameikataa hii jumuiya. halafu watu wanakwenda ulaya wanaanzisha jumuiya.

    ReplyDelete
  14. Huko Londo mna kazi kweli kweli...mhhhhh...lol.....Kila siku jumuiya ara matawi....lakini hatuoni hata yanaishia wapi.....

    ReplyDelete
  15. Kila ra-kheri. Mrundi, mnyarwnda, mtz, mganda. Ipo kazi, wote vichwa ngumu

    ReplyDelete
  16. ni gumzo tu babu!madebe matupu hupiga kelele zaidi!!!

    ReplyDelete
  17. Jumuia sijui jumuika kazi kweli kweli kila kukicha hebu tuwaulize hao wanaojiita wanjumuia wamedanya nini cha maana tangu wamefika huku ughaibuni maana wengi twawafahamu wao kwao wanijiita viongozi kwanza hawaivi kila mtu anataka aonekana yeye ndo yeye. sis wengine sio washabiki wa ujinga ujinga huo. Na ndio maana hata wanachama si wengi kwani ila mtu ankundi lake. Angalia uchaguzi wa tawi la ccm London waliochaguliwa viongozi wote wanatoka Reading na wote wanzania wakiwa viongozi huku basi wakirudi kule bongo watapata nafasi kiurahisi kuingia uongozini kwa kweli wamechemsha sana. Na hawa wenzetu wa jumuiya ya watanzani London hamna hata wanachokifanya cha maana wanishia kumuingiza balozi wetu huyu mama katika shughuli ambazo hata hazina kichwa hivi haoni kuwa ni bla bla tu. Nasikia eti wamemualika mh rais aje waongee jinsi ya kuisaidia Tanzania kuleta maendeleo kwanza ningewaona wa maana kama wao wenyewe wangekuwa wamejiletea maendeleo sio bla bla na misifa isiyokuwa na kichwa wala miguu tuwe waw wazi jamani katika sehemu zote nilizotembelea dunia watanzania tuko hoi kabisa kwetu sisi ni majungu, wivu kuangushana kuchekana na ubishoo hakuna ushirikiano hata kidogo na ndio maana hatusongi mbele.

    ReplyDelete
  18. wewe Freddy fikisha ujumbe kwa huyo John,kwanza mwambie kwanza awe proud kujiita mnyarwanda kabla u East Africa,pili asitutusi, wabongo ni watanzania and from the picture we see a Tanzanian, how rude of him and how can you Freddy as a Tanzanian take such stupidity,its obvious you have no say in whatever,tayari kuna wajuaji waganda na warwanda hizo nchi nyingine zina sauti kweli,wewe Freddy una deal na huyo John kakutumia umtangazie kazi yake ya kumuiga marehemu Luther Vandross,to me John has a big ego thinking he is Mr Vandross and think he can change E.Africa too.Here is some advice for you Mr John sorry Mr Vandross you cannot have East Africa without Tanzania and Kenya.And to be a good leader you dont go insulting people,there's a million words you can use to encourage people to join your organisation,I think your intentions are good but I despise what you think of Tanzanians and Kenyans you cannot generalise just because you've talked to a few Tanzanians you end up convincing yourself all Tanzanians are like that,I for one didn't even know you existed until I read this in Michuzi's blog,it shows how you are doing things in an old African way and expect people to join,If you are an E.African guy you should use sites like these to publicise what you want first before making decisions who is the chairman or vice chairman of EAfrica.

    ReplyDelete
  19. Amen and the way forward is bright.. At least Rwanda Day came out of what I started. Thanks Mr Mutoa. Greetings from John Vandross... Smile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...