MAMA MZAZI WA CHARLES KIZIGHA, MWANDISHI WA HABARI MKONGWE NCHINI (PICHANI JUU), AMEFARIKI DUNIA MACHI 1, MWAKA HUU NA HIVI SASA TUPO KANISA LA AZANIA FRONT KUAGA MWILI WA MAREHEMU TAYARI KWA SAFARI YA KWENDA MOSHI KWA AJILI YA MAZISHI.
MOLA AIWEKE PEMA PEPONI ROHO YAA MAREHEMU - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. poleni sana,mama+baba brenda na wafiwa wote.mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.Jirani CVU

    ReplyDelete
  2. Huyo Charles Kizigha alisoma Mawenza Secondary? 1986 - 1989? Manake kuna Charles Kizigha nilisoma naye Mawenzi. Pole sana kwa kuondkewa na mzazi wako.

    ReplyDelete
  3. POLENI KWA MSIBA

    ReplyDelete
  4. Poleni sana Charles na wanafamilia wote kwa msiba huo mkubwa.Mwenyezi Mungu amempenda zaidi.Hatuna la kufanya isipokuwa kumshukuru Mungu na kuzidi kusali tukimuenzi azidi kutuongezea faraja na ujasiri wa kukabiliana na majaribu yaliyo tuzunguka.Pokea salaam za rambirambi kutoka kwetu.Tuko pamoja nanyi katika kipindi hichi kigumu cha majonzi makubwa.Sisi sote tuko njiani.Mungu awabariki!

    ReplyDelete
  5. Wewe ANONY #2 kweli zumbukuku ile mbaya...Umeshaambiwa kuwa huyo Charles Kizigha ni mwandishi mkongwe, halafu unamouna kabisa kwenye picha hapo juu kuwa ni mtu wa makamo...Sasa inawezekanaje huwezi kumtambua na inawezekanaje mtu wa umri wake akawa amesoma sekondari mwaka 86-89?

    UMESHIKILIA MKIA WA MBWA, HALAFU UNAULIZA ANANYEA WAPI?

    ReplyDelete
  6. poleni sana wanafamilia kwa msiba uliowakuta. ni kazi ya mola hivyo hatuna jinsi, kilichobaki ni kumuombea rehema huko aendapo

    ReplyDelete
  7. mwandishi mkongwe hawezi kuwa amesoma 1986-1989~

    ReplyDelete
  8. Kaka Charles na familia, poleni sana.

    Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu. May she rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  9. Charles Kizigha mwenyewe ndio huyo aliye beba msalaba sasa tueleze kama kweli ulisoma naye mawenzi sekondari miaka ya 86 -89

    ReplyDelete
  10. MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI..
    HE WAS HERE (MALAYSIA) WHEN HE GOT THAT NEWS...
    POLE SANA MR KIZIGHA, POLE ANGELA, POLE BRENDA

    ReplyDelete
  11. we michuzi unamaanisha nini unapoandika "pichani hapo juu" ?? Vp inamaana marehemu ni huyu bwana alibeba msalaba???? Naona machungu ya kufiwa yanakuchanganya na kushindwa kufikiri vizuri.

    Poleni kwa msiba

    Mdau, Jeremani

    ReplyDelete
  12. Pole sana George (Charles), Diana, Lilian na wana familia wote. Rest in Peace Mama mpendwa.

    ReplyDelete
  13. Poleni sana kwa msiba huu mkubwa ndugu zangu wote upande wa Kizigha na ukoo wa Mziray/Mchomvu. Mama Kizigha kipenzi changu. Tutaku-miss sana nyumbani pale Majengo.

    (Ole wetu sisi mierenzi, kwa maana msonobari umeanguka)

    Poleni zaidi Mzee Kizigha, Kaka George (Charles), Dada Rosella, Diana, Lillian, Sheddy, Pepe, Dotto na Baby (Catherine). Bwana awafariji katika wakati huu mgumu.
    Bwana ametoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.

    ReplyDelete
  14. Sisi Watanzania mbona tunapenda kusema hivyo.Hivi maana ya comma na fullstop huwa ni nini?Michuzi katumia hizo comma na fullstop kwa ajili ya kutujulisha wapi sentensi inaishia.
    WAFIWA POLENI SANA.

    ReplyDelete
  15. Pole sana kaka Kizigha na wafiwa wote.

    ReplyDelete
  16. POle kwa wafiwa,Tumshukuru Mungu.Na nyie watoa hoja mchague ya kusema kulingana na topic inayozungumziwa.Ustaarabu jamani!! huo ni MSIBA.

    ReplyDelete
  17. Nashukuru kwa kunielewesha, sikujua kama aliyeshika msalaba ndiye Charles mwenyewe. Bila shaka ni majina tu yamefanana na Charles Kizigha aliyesoma Mawenzi Secondary na si huyu mzee. POLE KWA WALIOKERWA NA SWALI LANGU.

    ReplyDelete
  18. mwenyezi mungu awe nanyi wakatii huu mgumu. mama yetu alikua mkarimu kwa wote sie mungu amuweke mahali pema peponi, nanyie watu mnaopenda kubishana huyu alisoma mawenzi AU WAPI NAONA HIYO TABIA ACHENI MUWE MUNAANGALIA SEHEMU YA KUONGELEA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...