Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Spika wa bunge Mh. Samwel Sitta (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara ya Bunge ambaye pia ni mbunge wa Bumbuli, Mh. William Shellukindo (kulia) baada ya kufungua semina ya wabunge kuhusu mwelekeo wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2008/2009 iliyofanyia kwenye ukumbi wa Dar es salaam International Conference Centre leo
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na kiongozi wa Upinzani Bungeni na mbunge wa Wawi, Mh. Hamad Rashid Mohamed baada ya Waziri Mkuu kufungua semina ya wabunge kuhusu mwelekeo wa bajeti ya serikali (budget frame) ya mwaka 2008/2009 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Dar es salaam Internatinal Conference

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MHESHIMIWA WAZIRI MKUU POLE NA KAZI ZA KUHAKIKISHA KWAMBA MAMBO YANAELEKEA KUNAKOTAKIWA..NAONA LEO UMETOKA NA KOTI LA .."..KUWAKA WAKA.." SAFI SANA...

    ReplyDelete
  2. Mp ameanza kupiga pamba za uhakika! pesa nzuri sana jamani, remember alipoteuliwa kuwa waziri mkuu zile pamba alizokuwa amevaa na sasa ivi tofauti kabisa.

    ReplyDelete
  3. CCM haitowavua uwanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi

    2008-03-26 09:47:03
    Na Mashaka Mgeta


    Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakina mpango wa kuwanyang`anya kadi, waliokuwa viongozi wa Serikali na wabunge, wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi nchini.

    Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) utakaofanyika Machi 29 na 30, mwaka huu, kijijini Butiama, mkoa wa Mara.

    Alisema kuibuliwa kwa tuhuma za ufisadi, kulifanyika bungeni na Serikali iliagizwa kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe.

    ``Hawa watu kama walishutumiwa kwa ufisadi na wao kujiuzulu, si inatosha, kwa maana sisi kama Chama tuliwapongeza kwa kujiuzulu kwao... Sasa mnataka wanyang`anywe hadi kadi?`` Alihoji.

    Baadhi ya viongozi waliohusishwa katika kashfa hiyo na kutajwa kwenye mkutano wa Bw. Makamba na waandishi wa habari jana, ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa.

    Wengine ni waliokuwa Mawaziri, Dk. Ibrahim Msabaha, (Afrika Mashairiki), Bw. Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Mbunge wa Igunga (CCM), Bw. Rostam Aziz.

    Aidha, Bw. Makamba alisema hatua ya CCM kufanyia mkutano wa NEC kijijini Butiama, haina maana ya kwenda kufanya matambiko kwenye kaburi la Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere.

    Alisema hivi sasa, kuna fikra potofu miongoni mwa watu kuhusisha mkutano huo na matambiko ama kuomba radhi kwenye kaburi la Mwalimu Nyerere, suala alilosema halimo katika ajenda za mkutano huo.

    ``Hatuendi kutambika wala kuomba radhi, kama ni radhi tungeiomba kanisani, lakini hiyo haitatuzuia kuzuru kaburi hilo na kumuombea,`` alisema.

    Alizitaja ajenda za mkutano huo kuwa ni hali ya kisiasa nchini, kutoa taarifa ya mazungumzo ya mwafaka kati ya CCM na Chama Cha Wananchi (CUF) kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani humo.

    Kwa mujibu wa Bw. Makamba, ajenda nyingine ni kutathmini hali ya uchumi wa nchi kwa njia ya semina itakayoendeshwa na Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu, taarifa za uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Kiteto, sherehe za miaka 31 ya CCM na maendeleo ya shughuli za chama.

    Bw. Makamba alifafanua kuwa hatua ya kufanyia mkutano wa NEC mikoani ilianza tangu 1967, ulipofanyikia mkoani Arusha, mahali lilipozaliwa Azimio la Arusha.

    Pia alisema mikutano mingine iliwahi kufanyika Iringa, Musoma, Handeni mkoani Tanga, kijijini Mkongo huko Rufiji na Zanzibar.

    Naye Mweka Hazina wa CCM, Bw. Amos Makalla, alisema chama hicho kitatumia rasilimali zake kufanikisha mkutano huo, bila kutegemea msaada wa watu ama taasisi za kijamii.

    Alisema mkutano huo upo katika kalenda ya CCM, ikiwa na bajeti iliyoanishwa kama ilivyo katika shughuli nyingine za CCM.

    Bw. Makalla, alikuwa akifafanua kuhusu swali kama kuna wafanyabiashara waliojitokeza kutoa msaada wa usafiri kwa wajumbe wa NEC kwenda kijijini Butiama.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  4. WAZIRI MKUU ANAPENDEZA..ANAMEEEREMETA..ANA..MEREEEMEETA..OLDI IS GOLDI...UMPE WAZIRI HESHIMA YAKE..PICHA ZA ZAMANI TAFADHALI..

    ReplyDelete
  5. Ingekua vyema maswala ya bajeti kwa ujumla, na uingizaji wa pesa nchini tanzania ikiwa katika mapato ya kodi, pesa za kigeni, na misaada kwa ujumla, yanawekwa wazi kwa jamii kupitia katika mtandao.

    Hii itatusaida sisi sote kama wananchi, kuweza kujua wapi pesa inatumika kibajeti, na vipi pesa yetu inapatikana.

    Jengine la kuongezea, miradi miundo mbinu, pamoja na miradi mengine ambayo imeanzishwa na kudhaminiwa na serikali, pia iwekwe wazi katika mtandao na kuona ni wapi tumefikia na pesa yetu imetumika vipi katika miradi hiyo.

    Ninakumbuka kwamba serikali inataka kuanzisha utaratibu wa mtandao wa wizara zote za serikali, hii itatusaidia sisi kupata hizi habari za utumikaji wa pesa na mali za umma kwa ufasaha kabisa.

    Kwa sababu nikisema hivi, na hili siliongelei kama ni mpinzani, bali ni kutaka kilicho jema kwa serikali yetu na nchi kwa ujumla.

    Manufaa ya karibu, itaondoa na kufichua UFISADI na ubadhilifu wa mali ya umma.

    NI MUHIMU WANANCHI KUJUA KILA SHILLINGI IMEKWENDA KATIKA MATUMIZI GANI..HAPO PEKEE NDIO TUTAJIKWAMUA KIUCHUMI.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  6. Hello Michuzi na watoa mawazo wengine. Mi naona kama hamko serious. Nguo gani hizo amevaa PM hala mnamsifia. Hizo kiitikadi hazifai. Mshauri wake wa mavazi hapo ni zero tu. Hizo ni very unprofessional. Pamba hizo ni safi kama wewe ni DJ au mtangazaji kwenye mashindano ya u-miss au uko kwenye Disko la sekondari. Huyu ni waziri mkuu. Hawezi kuvaa koti la kijivu la kung'aa, suruali ya udhurungi, tai ya bluu, viatu vyeusi halafu mkamsifia Pamba safii. Wrong!
    Na endeeleeni kumsifia tu kama siku moja hamjamuona yuko kwenye mikutano ya UN na mavazi kama hayo. Halafu wataalamu wanam-disqualify hata kabla hajaongea.
    Hamumuoni mwenzeka JK na EL walivyokuwa wajanja kwenye pamba.

    ReplyDelete
  7. Ushuri wa Bure,

    Napendekeza Rais ampe Pinda safari nyingi za nje. Na kila napoenda awe makini kuangalia ma-PM an Marais wa wanavaa pamba gani za kisasa. Asije akawa kwenye ulimwengu wa peke yake.
    Hapo ndio nilikuwa namvulia Lowassa kofia inapokuja kwenye pamba. JK anajitahidi lakini na yeye akiamuaga anaweza kuvaa kama Pinda ingawa yeye anavaaga tu ofisini sio kwenye oficial ceremonies.
    Sasa Pinda duuuu...iko kazi. Hizo ndio Old Schools bwana

    ReplyDelete
  8. Subiri kidogo:

    Shati jeupe,
    Tai ya Bluu,
    Koti la kung'aa,
    Suruali ya kahawia,
    Viatu (labda vya kijani au vyekundu),

    Nakubaliana kabisa na mtoa hoja alyesema kwamba mshauri wa mavazi wa Pinda - zero

    ReplyDelete
  9. Natafuta kazi ya kumvisha waziri wetu mkuu, niende wapi jamani, maombi niombe wapi maana hii hatari utafikiri waziri wetu sio mmbongo.. duhh

    ReplyDelete
  10. EEEEH Muheshimiwa Pinda naona unawasiloiana na Muanzilishi haswa wa kimbembe cha Richmond Mh. Shellukindo. Mungu wape uzima na furaha viongozi kama hawa kina Shellukindo wenye hisia na faida ya nchi na wananchi na sio maslahi binafsi. Nimefanya kazi na huyu mzee miaka 20 iliyopita ninamfahamu fika msimamo wake na jinsi alivyo safi. Pinda chukua ushauri wa dhati hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...