Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kipanya wewe sasa basi,nimekuvalia kanzu mze!Usisahau,ile zawadi yako ya Juisi ya Pilipili na Thupu ya Ndimu bado ipo kwenye Freezer!Michuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuz pia atakuwepo,Richmond atakuwepo,Mkwanja pia atakuwepo pia tumemwalika yule ndugu yetu wa TWIN TOWERS akipata ahueni pia atakuwepo!Bila kushau PekechaPekecha.Usisahau kuja na ndizi katika Koti lako.Pilau pia atakuwepo!Very Creative,Very Bright!She's all yours for the asking,pardon!Jamaa alifikiri Segere Matata,yatamtokea puani sasa.

    ReplyDelete
  2. Bro Hujafa hujaumbika, waswahili walisema - siku zako zinahesabika

    ReplyDelete
  3. Jamani kipanya kaniacha kidogo... maelezo wadau

    ReplyDelete
  4. Aise KP this is brilliant my man! Yaani nimekubali. You know your art.

    Peace!

    ReplyDelete
  5. Kusema kweli, dogo Kipanya wewe ni Msanii halisi.

    ReplyDelete
  6. !!!!!Hoya "KP" Nakuaminia babake...!!!.Mimi niko Minnesota,usa lakini always unanipa live from Bongo as I dont need kuperuperuzi saaana,just your simple talented messege napata all I need from back home..Wow..........!.Congraturation kaka "KP"....!

    ReplyDelete
  7. Yaani Kp wewe!!huwa unanifurahisha sana keep it up kp

    ReplyDelete
  8. te hehehehehehehe tetetetete Kipanya Umedata sio mchezo !! well done and very funny !

    ReplyDelete
  9. nawe anony. said wa April 3 unaetaka maelezo mbona unakuwa mgumu wa ku-read behind the image lakini ? okay ni kwamba kama unafuatilia news za yanayoendelea huko bongo kwetu ni kwamba JK aliahidi muafaka na CUF kuhusu issue za uongozi huko kwa ndugu zetu wa visiwani sasa baada ya kikao cha kamati kuu ya chama tawala amabako waliahidi watafikia uamuzi wa mwisho sijui kitu kam hicho mambo yanaonekana yanaenda upande kwa sababu hawakuja na solution ya kudumu sasa hapo imajini upande wa pili wa convesation hiyo ni JK anampigia simu Mzee mstaafu BM kuomba ushauri, hapo sasa papaa Ben ndio yuko katika simu yake ya Tigo sijui hiyo anakula laifu na pesa zetu za nchi kajibanza pembeni hataki hataki hata kusikia yanayoendelea nyumba kubwa ndio anamtolea nje bwana mdogo wake.........bwana wee nawe malizia mpaka nikueleze kila kitu ??? use ur imagination thats the whole point of Kipanya's art tafsiri picha uwezavyo mwenyewe ili muradi uwe unakaribia ukweli au sio wadau ? and I thinkI got this one ! KIPANYA THIS ONE IS good and very funny mimi nimemaindisha hiyo pedejee ya Mzee Mhishimiwa na suspenda zake ! hahahahaaha

    ReplyDelete
  10. Mererani na Maisha ya Kumtegemea Mungu

    2008-04-03 08:56:53
    Na Charles Kayoka


    Taifa limefikwa na mkasa na msiba mwingine. Kufukiwa kwa wachimbaji wadogo wadogo kule Mererani.

    Wakati tukimnasihi mwenyezi Mungu kuwa awapokee viumbe wake waliofariki kutokana na ajali hiyo, na awasamehe dhambi zao na zetu, lakini tunapaswa kujiuliza sana sisi tulio hai kuhusu dhambi zetu hadi zikasababisha vifo vya ndugu zetu.

    Aidha tuendelee kuwaombea majeruhi, kama wapo, na ndugu wa waathirika wa ajali hiyo ustahimilivu mkubwa katika kipindi hiki kigumu.

    Tukio la Mererani, bila kutaka kulipigia chuku, linaweza kuelezeka katika mikabala kadhaa, lakini nasema kwa uhakika kuwa ni ajali tuliyokuwa tukiisubiri itokee.

    Hatukujua ni lini, lakini nataka kuwahakikishia Watanzania wenzangu kuwa katika kuiendesha nchi katika karne ya 21 kwa kutegemea kuwa atashusha mibaraka yake na ulinzi kama mana, bila sisi wenyewe kuweka mifumo ya kujilinda na kujineemesha, ni sawa na watu wa karne za awali za kuumbwa kwa dunia walioishi wakidhani kuwa radi ikipiga na kuua, au mafuriko yakitokea ni kwa sababu miungu imekasirika kwa vile wamecheleweshewa sadaka yao ya binti mrembo na kigoli.

    Hawakuelewa uwezo wa nguvu za mazingira na zile za kiasili. Lakini katika karne ya 21 ambako hatuishi tena kwa hofu ya mizimu au miungu sidhani mwenendo huu unafaa katika kuiendesha nchi.

    Kwamba migodi ya wachimbaji wakubwa haikukumbwa na mkasa kama huu ni ushahidi tosha wa haya niyasemayo kuwa tatizo sio Mungu aliwataka viumbe wake, bali ni kwa sababu ya kutumia teknolojia duni, na kukosekana kwa usimamizi bora wa kitaalamu ambao serikali ingeweza kuwapatia wachimba hawa hata kwa kuwatoza ushuru kidogo kwa huduma hii.

    Kama mvua kubwa ilinyesha Mererani yote, nini kilifanya migodi ya wenye fedha isiporomoke: mtaji mkubwa na utaalamu wa hali ya juu.

    Nadhani serikali ingeweza kufungua ofisi ya ushauri ya wahandisi wa migodi, ambayo ingeweza kutumika kufuatilia hali ya usalama ndani ya migodi na kutoa ushauri kwa wanaoimiliki.

    Ukaguzi wa mara kwa mara ndani ya migodi na maelezo kutoka kwa wachimbaji ``nyoka`` ungekuwa unatoa picha ya nini kinachoendelea huko ndani. Hilo lingesaidia kupata taarifa ambayo ingetumika kuzuia wachimbaji wasiingie migodini nyakati fulani fulani, kama za mvua au matetemeko ya ardhi.

    Ukanda wa kaskazini ni eneo la matetemeko ya ardhi, kama ilivyo kwa mvua nayo hayatabiriki katika ukubwa wake na athari kwa wakazi na hasa migodi, je tumejitayarisha nalo vipi?

    Ninalotaka kuzungumzia hapa ni swala la kushindwa kujenga mfumo wa kujitayarisha na ajali- disaster preparedness.

    Serikali ambayo ndiyo msimamizi wa kila siku wa maisha ya raia inapaswa kujua au kushauri nini watu wafanye katika kuzuia ajali na vifo au kupunguza athari za ajali kama hizo zikitokea.

    Sisi tulio mbali tunataka kujua serikali yetu imeweka tahadhari au vifaa gani vya kuokoa na kuzuia ajali si tu Mererani, bali maeneo yote yenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo popote pale ilipo nchini.

    Tungetaka kujua kama serikali imekuwa ikitoa mafunzo kiasi gani kwa wachimbaji na wenye migodi kuhusu suala la usalama kazini- maeneo ya migodini.

    Maeneo ya migodi ni maarufu kwa kuwa mazingira hatarishi; ugomvi, kuuana, wizi, kubakana na mapenzi yasiyo na kinga dhidi ya maambukizi ya maradhi mbalimbali.

    Lakini kubwa kama hayo ni athari ya kiafya ya kimwili na kiakili kwa wachimbaji.

    Vumbi linalotokana na uchimbaji huko mashimoni linaweza kuwa na madini au gesi ambayo hawa watu wasio na utalamu wasiijue na hivyo ni rahisi kufa au kuathirika mara moja au dalili zake kutokea taratibu.

    Tumezungumzia athari ya madini ya mercury na zingine zinazotumika migodini kwa afya ya binadamu.

    Na raia wenzetu wanakufa, wanapata maradhi na hakuna linalofanyika zaidi ya kumsingizia Mungu kuwa aliwapenda zaidi; ni kweli sisi hatuwezi kuwa tunawapenda zaidi kama hatuwapatii ulinzi wa kutosha dhidi ya hatari za maisha yao wakiwa machimboni.

    Afadhali Mungu awachukue ili akawahudumie yeye mwenyewe.
    Na suala hili la kukosekana kwa tabia ya kujilinda dhidi ya hatari zilizopo na zinazoweza kuja imejengeka na pengine kufikia hatua ya kudhani kuwa hatari haitakuja tokea, na huku sheria husika zikiwa zimeweka wazi nini kifanyike katika kulinda afya na uhai wa wafanyakazi katika sehemu mbalimbali.

    Waajiri wamekuwa wakiwaweka wafanyakazi katika mazingira duni ya kazi wakitumia kemikali na teknolojia inayoathiri afya za watendaji lakini serikali imekuwa ikifumbia macho, hata pale ambapo idara husika zinafanya ukaguzi na kuwasilisha taarifa serikali kuu.

    Serikali kuu inaweka ripoti na mapendekezo katika kabati na huwa mwisho wa mambo.

    Waajiri sasa wamepata kichwa cha kiburi wakijua kuwa hakuna wanachoweza kufanyiwa na mateso dhidi ya wafanyakazi yanaendelea! Hapo tunamuhitaji Mungu kuja kuingilia kati, eti!

    Nenda katika maeneo ya maduka na makazi. Nyumba ni ya ghorofa, mwenye nyumba anaweka vyuma kuziba milango na madirisha kuzuia wezi.

    Lakini je kama itatokea moto au tetemeko au nyumba kuporomoka watu wa uokozi- fire and rescue- watawafikiaje?

    Je, sheria za jiji kuhusu ujenzi salama zipo, na kama zipo zinazungumzia nini juu ya ujenzi ambao huzuia waokoaji washindwe kufanya kazi yao ajali ikitokea.

    Ujenzi katika mitaa imewekewa maelezo ya kutosha kusaidia uokoaji na wale wanaoshughulikia maji taka. Lakini ni jambo la ajabu kuwa, kuta kati ya nyumba zinaunganishwa au kujengewa maduka na mamlaka husika zinaona ni kitu cha kawaida. Bora Mungu anaona.

    Pita majengo ya makazi na ya biashara hapa Dar-es-Salaam au popote nchini, utapanda ghorofa ya kwanza hadi ya mwisho, au utapita kila duka, hutaona dalili ya ufahamu wa kuzuia moto.

    Huwezi kuona ndoo ya mchanga, au kizima moto ambacho mtu anaweza kukitumia mara moja moto unapoanza kama yuko ofisini kwake.

    Inawezekanaje mtu anamiliki nyumba au biashara ya mamilioni ya shilingi lakini hakumbuki kuweka vizuizi vya ajali ikiwemo moto- sidhani kama kweli wamiliki hawa wa majumba na maduka wamekata hata bima za ajali/moto.

    Na serikali inawaangaliaje watu kama hawa wanaoishi kwa kumtegemea Mungu.

    Elimu gani inatolewa kuwaelimisha watu wawajibike juu ya maisha yao wao wenyewe.

    Ni ukaguzi gani unafanyika katika nyumba za kulala, na hasa magorofa yanayoota kama uyoga hapa nchini kuhakikisha kuwa moto na hatari zingine zimewekewa kinga au tahadhari za kupunguza madhara, kulinda na kuokoa maisha na mali za wakazi.

    Tukio la Mererani litukumbushe mambo mengi! Kusimamia sheria zilizopo; kujua kuwa hatuwezi kuishi kwa kumlazimisha Mungu aje kutulindia raia wenzetu; kuhakikisha kuwa utaalamu unatumika kila wakati katika kufuatilia maisha ya wanaotenda kazi katika mazingira yenye vihatarishi. Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  11. Anoni Anoni,
    Asante sana kwa ufafanuzi wako na huyo aliyeuliza swahili kuhusu ufafanuzi big up sana!
    Ukitaka kujua watu wengi walikuwa hawajaelewa angalia comment. Sana sana watu wanaishie kusema KP nimekuvalia kofia...KP you make get me all i want back home, lakini hawasemi wamepata nini. Yaani hakuna anayegusa kinachorejelewa. Wengine ndio wameamua kutoka nje ya mada. Kwa wale mnaoelewa picha za KP msisite kufafanua lau kidogo
    Mwenye nyumba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...