mwenyekiti wa mikutano ya sullivan balozi carl masters akiongea na waandishi asubuhi hii hoteli ya kempinski kilimanjaro juu ya mkutano wa nane wa sullivan utaofanyika a-taun wiki ya kwanza ya mwezi ujao. kulia ni mkurugenzi wa habari wa taasisi ya sullivan nichet smith.
balozi masters amesema amefurahishwa sana na maendeleo ya maandalizi ya mkutano huo ambapo sasa yamefikia asilimia 90, na akasema kila mtu anakaribishwa kushiriki kwani madhumuni yake ni ya kuwakutanisha wamarekani weusi wapatao 3,000 watakaokuja na wabongo katika nyanja mbali mbali.
amesema ana uhakika mkutano huo sio tu utakuwa wa kukumbukwa bali pia utakuwa ni 'mama wa mikutano yote iliyotangulia' ambapo leo zimesalia siku 19 tu kabla ya huo mkutano.
kwa wanaotaka kujisajili kwenye tovuti fungua www.thesullivansummit.org au www.thesullivansumit.org/summit na fuata maelekezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2008

    Mbona hatuambiwi hao wamarekani weusi wanaokuja wanakuja na miradi gani ili tujipange kuainisha maelewano. Isije ikawa tunaletewa porojo tu na kuachiwa vumbi!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2008

    Hiyo `akaa babu wee' kwenye piha kulikoni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...