niko na anko zangu hivi karibuni kwenye mnuso fulani hivi...najua nitashambuliwa lakini mie kumeng'enyua kiinglishi kwa kimatumbi sijui. sasa wajomba niwaiteje? na baba ama mama mdogo nao niwaiteje- smoo faza ama smoo maza? msaada tutani wadau....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2008

    Maanko kwa mtindo upi hapo?

    Manake kwa jinsi ninavyofahamu Anko ni ndugu wa kiume wa baba au Mama sasa hawa ninaowaona kwenye picha ni wanawake, huo U-anko umekujaje na kuna uhalali wa kuwaita wanawake Ma-anko pia?

    Michuzi nifungue macho mwenziyo manake naona kama umepotoka vile kutumia neno ndivyo sivyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2008

    Michuzi bwana, kwa totoz hujambo, yaani hii mikonoziii bado hujaacha, kweli aka kaugonjwa kamekukolea. anyway bwana we enjoy tu maisha yenyewe ni kama hivyo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2008

    Hey Michuzi!!

    Kwanini hao madada unawadhalilisha kwa kuwaita anko "uncle", wewe wakikuita anti utafurahi!!! Maskini ya mungu dada zetu hao wanacheka kwa furaha...lakini Michuzi kaamua kuwa ita eti "Uncle" yeye kasema anko zake....angewaita hata wipwa kwa uwingi tungejua watoto wa dada yake...lakini huwezi jua duniani mambo mengi yanabadilika.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2008

    baniani husema
    wewe janja iko

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2008

    hao ni nephews wako bwana misupu...

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 14, 2008

    wakiwa wakike kama hao ni 'niece' sio ma anko, wakiwa wakiume ni 'nephews' ...naomba udugu hapo michuzi

    ReplyDelete
  7. mi nina maoni/swali linaloenda sambamba na swali la michuzi hapo juu. Nimeona watanzania wengi wakiwaita nieces and nephews (i.e. watoto wa dada zao au watoto wa kaka wa wake zao) WAJOMBA.

    Sidhani kama ni kiswahili fasaha. Navyofahamu mimi, wewe ndio wanakuita MJOMBA. Ila wewe unawaita wao WAPWA. (Umjoja MPWA). Wadau mnasemaje juu ya hili, lipi ni sahihi?

    PS: mdau wa May 14, 2008 5:58 PM ameshatoa jibu sahihi kwa nanihii wa Tegeta

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 14, 2008

    Walioandika niece na nephews hebu yatafsirini hayo maneno kwa kishwahili hayo ni maneno ya wenzetu kwani msije kujifanya mnakosoa kumbe hamjui maneno sahihi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 14, 2008

    Kwako wewe, kila mmoja ni mpwa, au wapwa katika wingi wao. Ila wewe kwao ni "ami" au "mjomba" wao. Sina uhakika kama kuna tofauti kati ya ami na mjomba...labda ami ndio baba mdogo/mkubwa. Msaada tutani wadau.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 14, 2008

    sawa jamani ngoja tusaidiane,maana najua kwetu watanzania tunapenda kutafsiri kiswahili mojakwamoja kwenda kiingereza ndio maana tunakosea maranyingi.
    kaka/mdogo wakiume wa baba yako[baba mkubwa/mdogo],au kaka wa mama yako[mjomba]=uncle.
    dada wa baba yako au wa mamayako=aunt
    watoto wa baba yako mkubwa/mdogo[kaka,au dada],na watoto wa shangazi,au mamayako mdogo[binamu]=cousin
    watoto wa dada yako,au kaka yako[wapwa]= kama niwakiume[nephew],kama wakike[niece].
    shemeji,wifi,wakwe,=inlaws,ilahapa inategemea kitangulizi,mfano mother inlaw,sister inlaw etc.
    babu,bibi=grand parents.
    wajukuu-grand children[son,daughter]
    baba/mama wa kambo=step father/mother.
    baba/mama wa babu/bibi yako=grand grand parent,
    mchango wangu ndio huo.

    mdau-ughaibuni

    ReplyDelete
  11. Peter bwana :)
    Naomba niwarahisishie wadau...huyo dada wa kushoto anaitwa Maria na wa kulia anaitwa Namsy. Kwani Michuzi wewe mpare?????

    ReplyDelete
  12. sasa we Anony wa May 14, 2008 8:08 PM sijui unataka watu watafsiri kwa lugha gani tena? Maana Michuzi ameuliza kwa awaiteje hao wapwa (ingawa katumia kimakosa neno "wajomba") zake kwa kiinnglish na wadau wamejibu kwa usahihi ni nieces na iwapo wangekuwa wa kiume nephews.

    Sasa unataka watu watafsiri kwa lugha nyingine ipi tena? Kiyao au?

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 15, 2008

    Waosha Vinywa, lugha is not reachable. Hao ni "NIECES" not Nephews.

    Wabongo noma sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 15, 2008

    Samahani hapo mdau wa Ughaibuni amesema Grand Grand...ni sawa ? au inabidi Great Grand....sio ugomvi ni katika kutaka maelekekezo tu ya Lugha.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 15, 2008

    Jambo michuzi,
    Mzee wa konoziii naona mdo mlikuwa mmemaliza kuutwika ulabu kwani naona makuti yakitangaza ze biazi. endeleza kona ndo maana ukaruhusu salam na picha.

    ReplyDelete
  16. Mzee, naomba nije kuleta posa ya binti mmoja. They are so cute!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 15, 2008

    Ukiuangalia uso wa Michuuz kwa makini hauko 'sraight',shavu limelalia zaidi kushoto kwake au kulia mwa picha!Message imeshafika Mze wa Konoooooooooooooooooooooooz!Ze Konooooz zingeshuka chini kidogooooooooz,ofcooooooooooooooourse!Jembe halimtupi Mkulima,MChuuuuuz!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 15, 2008

    nikaktka mkono kuteleza tu, nikweli anonymous wa trh 15 2008,saa4:45 uko sahihi,ni GREAT GRAND parents/children. nashukuru kwa kutopita kimya,wengine huenda wangepotoka kwa hiyo typing error yangu. japo kwa kuangalia inakuwa haifanani na error bali mistake!

    mdau-ughaibuni.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 15, 2008

    eehh kaka michu na ww mpare maana i know namsifu n maria!!!maria amekuwa kweli..nyc 1

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 16, 2008

    Misupu hapa umewakomesha wadau, wamekodolea macho watoto (WASICHANA), wamesahau THE FULANAZZZZZZZZZZZZ. Bila kuwawekea hizo sura ungesikia FULANAZZZZZZZ!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 16, 2008

    Pengine Kenya west na Jamie Foxx watakusaisia
    [Chorus:]
    (She steal me money)
    Now I ain't sayin' she a gold digger (When I'm in need)
    But she ain't messin' wit no broke niggas (She steal me money)
    Now I ain't sayin' she a gold digger (When I'm in need)
    But she ain't messin' wit no broke niggas(I gotta leave)
    Get down girl, go 'head get down (I gotta leave)
    Get down girl, go 'head get down (I gotta leave)
    Get down girl, go 'head get down (I gotta leave)
    Get down girl, go 'head
    From M14

    ReplyDelete
  22. Michuzi hivi hiyo fulana utanipa au ndo hadi aje bint ndio utatoa!basi mpe swahiba wako chibiliti maana si watu wa iringa hatuthaminiki ndio maana mjengwa kakimbia iringa!!

    ReplyDelete
  23. wadau nisaidieni nipate hii Fulana itanifaa kwa baridi!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 17, 2008

    Salim, Mjengwa yupo wa siku hizi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...