SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAUDI BALALI
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.
Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia.
Ni kazi ya Mungu haina makosa.
Tunawatakia mazishi mema.
Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema.
Amin.
IMETOLEWA NA OFISI YA MAWASILIANO, IKULU
TAREHE 23 MEI, 2008
ish, kumbe naye yumo!
ReplyDeleteyaaani Hapo ndo unajua CCM flip flop sana!!!
ReplyDeleteHAYA!!
ReplyDeleteMMEUMBUKAAAAAA... HAOOOOOOO...IONE MISURA YENU! HAHA MARA PLASTIC SAJARI,MARA KAFICHWA,MARA NINI,MARA OOH SERIKALI ITANGAZE
MSHATANGAZIWA SASA... BALALI IS DEAD
ACHENI NDOMONDOMO
LEILA SHAKUM - THE NIECE
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
ReplyDeleteJamani huyu Rais wetu vipi?
yaani mpaka sasa bado anasema Ballali alifariki Boston?
Yaani ukisikia kuwa wa mbili havai moja ndiyo hapaa!
tanzanian don't cry any more,
ReplyDeleteyou cry by the time nyerere pass away!
its over now, ....
we trust them...they betrays us.
we trust them they dishonor us!
they dishonor your country for very few dolars in their foreign acc'
leave the country dragging feet in no movement for every thing!
sorry ma' fellow tanzanian,
changes in not coming yet.
stop weeping....my country,
Nyie watu vipi? Si mlisema mbona serikali iko kimya haijatoa rambi rambi, haya rambi rambi zimetolewa, sijui mnaleta vitu gani tena. If he is dead, and you believe he is not dead, you wont bring him back to earth. Subirini na nyie siku zenu zikifika mkatae mseme wakati bado!
ReplyDeleteRIP Balali
leila nimependa comments zako, yani kama nakuona vile unavofanya kwa vitendo! lakini nafikiri watu wana uhuru wa kutoa maoni kwa namna wanavoona jambo kutoka katika pembe tofauti.na ndio maana kuna sehemu ya maoni na ujue hii dunia imejaa artists huwezi kujua nani ana kipaji mpaka aingie kazini na hiyo itakuwa pale inapobidi.
ReplyDeleteHivi wewe Leila unayedai kuwa ni Niece wa marehemu Balali mbona hueleweki uko upande gani wa serikali, wa Watanzania walipa kodi? kwanza hata huoneshi hata kama una uchungu maana tangu hizi taarifa za msiba zitokee wewe kutwa uko kwenye blog ya Michuzi, sasa si ujumuike na wenzio kwenye msiba huko nyumbani kwake? au umeewa kidogodogo na serikali ili uigize tu hapa? watu wana uchungu na hiki kifo kisischoeleweka na tumechoshwa na serikali kuwapoteza watu just like that!!!
ReplyDeleteNASIKIA KAFUFUKIA UARABUNI
ReplyDeleteKWAHEEERI!
anon wa 10:35 umeongea POINT!..huyu LEILA anatuzingua tu hapa.
ReplyDeletehuyu laila ndo alivyo...hata kule bc anakurupukaga,naona ndo kanunua kakompyuta
ReplyDeletehakuna chakuumbuka wala nini, bado hakuna kitu cha kuprove kafa. hata picha ya mwili wake. inawezekana kuwa ni mchezo tu huu. mbona hata picha ya marehemu mtoto aliyechinjwa ilitolewa humu? leteni picha ya marehemu balali.
ReplyDeletehuyu niece wa balali mbona ana jina la kiarabu jamani?isije tukawa tunajipendekeza bure,ili tuambulie urithi..mna undugu nae au?
ReplyDelete