mama wa mitindo asia idarous akionesha ubunifu wake wa mavazi ya harusi
mkongwe khadija mwanamboka anaonesha mamodo wake wa kiume katika mavazi ya harusi huku khadija kopa (shoto) na sabbah muchacho wakiimba wimbo wa 'kimasomaso mwanangu msimuone"
mustafa hassanali akionesha ubunifu wake wa mavazi ya harusi
mamodo wakiwa katika mavazi ya harusi yalobuniwa na rose valentine



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2008

    safi wamejitahidi, nimependa nguo za khadija mwanamboka

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2008

    Mz. Michuzi asante sana kwa kutubandikia picha hizi. Nimefarijika sana kuona kwamba tunaanza kujikomboa kiutamaduni na kuondokona na KASUMBA iliyotawala miongo kadhaa sasa kuwa vazi murua la harusi ni lile lililobuniwa huko "ULAYA"!!!! Ninawapa pongezi wabunifu na kuwaomba waendelee na ubunifu wao kwa kasi mpya na kwenfa nje ya mipaka ya harusi. Nani anajua, pengine wanaweza kuja na ubunifu utakaotutoa kwenye unifomu ya mikoti na mitai ya ulaya, na kutuweka kwenye vazi ambalo tunajisikia raha na bado tunaonekana kuwa watanashati na waungwana katika mijumuiko rasmi ya kitaifa na kimataifa.

    Hongera wabunifu,

    mkereketwa wa utamaduni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2008

    Hongereni sana.
    Nimependa vazi la Rose Valentine.
    Natumaini next maonyesho wabunifu wote mtaondoa huo U-Nigeria kwenye mavazi mbuni kitu pekee kidogo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2008

    Wapi Africa Sana???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2008

    vazi la rose valentine ndo bomba sana wengine bado sijaona kitu hapo,jaribu tena baadae.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2008

    ndugu anony wa hapo juu, kumbuka kwamba ubunifu ni pamoja na umairi wa kuchanganya vitu kutoka vyanzo mbalimbali. Katika dunia ya sasa ya utandawazi tusitarajie kuwa wabunifu wa kitu cho chote kile wataanzia kwenye zero. Bali watachukua hapa na pale kutoka vyanzo mbalimbali nigeria, south africa, ulaya, india, china, congo, uganda, nk. huo ndio utamaduni hai na endelevu na umairi ni jinsi gani mtu anavyochagua na kuchanganya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...