JK akioneshwa na Rais George Bush wa Marekani mandhari ya ikulu ya Marekani,White House, wakati Rais Kikwete alipomtembelea Rais Bush Ijumaa asubuhi jijini Washington D.C.Rais Kikwete yupo nchini Marekani kwa mwaliko wa Rais Bush
JK na mwenyeji wake Rais George Bush wa Marekani wakiwa katika mazungumzo ofisini kwa Rais Bush,Oval office iliyopo ikulu ya Marekani White house jijini Washington D.C Ijumaa asubuhi. picha na mdau Freddy Maro wa ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hii...noma. Mimi ninakaa Marekani lakini raisi wangu amekuja hapa hata sina habari. Kweli Africa ni nchi ndogo na changa sana hapa duniani.
    Naangalia sana news lakini Bush leo yupo Minnesota ijumaa mchana na JK kajaa mjini lakini wala hasikiki...long ways to go brothers and sisters

    ReplyDelete
  2. Bwana Kichaka alivyokuja Bongo, JK akamuiga tie nyekundu mpaka akabadilisha official portraits zake. Tangu siku hiyo JK anavaa tai nyekundu tu. Ila check sasa Bwana Kichaka kapiga tai ya blue, sijui JK atabadilisha picha yake tena? Hmmm. Lakini jamni raisi wetu handsome!

    ReplyDelete
  3. Ndege wafananao huruka pamoja.

    ReplyDelete
  4. Rais wetu anacheza "Baba kasema tu....

    ReplyDelete
  5. ..... wanamichuzi , naomba kuuliza ni nani anampa advice Rais wetu katika suala zima la uvaaji , nchi za dunia ya kwanza kuna mtu special kazi yake ni kumuandalia Mkuu wa nchi avae ni sehemu gani ...Rais wetu alichemsha kidog alipochanganya rangi ya Suit alipokuwa Hokkaido , Japan wakati wa Global Summit .Juu alipiga dark blue na chini akaweka grey trouser ... .. kiliwa kichekesho kiasi kwani rais pekee aliyechanganya rangi , Viongozi wengine woote G 7 , walikuwa uniform up to down rangi ilkuwa moja ..full colour suits na walipendeza ...
    Kurudia kosa ni kosa .
    Mdau
    Kisiwani

    ReplyDelete
  6. anony hapo juu unasema Africa ni nchi ndogo?? Africa ni bara ndugu kama lilivyo bara la amerika...labda kama umekusudia kivingine.
    JK ushkaji alioanzisha na Kichaka utaleta impact kuliko Akudo na kupita Big Ben. Nyepesi nilizonazo Kichaka baada ya kumaliza kuku wake wa miaka 8 jumba jeupe anatarajia kuja kufanza buz huku...ni mambo ya madini nadhani ndo wapo kwenye mjadala wa muda mrefu thats y JK anatia maguu sana huko US...

    ReplyDelete
  7. Acheni ulimbukeni wabongo, mambo ya kumchunguza mtu kavaa nini leo ni uswahili ulopita kikomo. Nyie ndio mkirudigi bongo mnajifanya kuvaa kimarekani na kiingereza chenu kibovu cha kuiga.
    Hebu cheki vizuri hapo, JK kapendeza sana. Acheni upuuzi.
    pigeni box mrejee nyumbani muwekeze, sio vijisenti mnavyopata mnunue vijisuti vya sale mje kutukoga bongo.

    KIROBA

    ReplyDelete
  8. Hellow Ndg. Kiroba ,
    Napenda kujibu hoja hayo , suala la uvaaji siyo suala la kuchunguzana ...suits ina heshima yake na ni lazima ibaki pale pale .. Suala la kubeba maboksi na suit kamwe haziingiliani .Miezi iliyopita baada ya Mh, Pinda kuchaguliwa naye alifanya hivyo hivyo alisalimiana na Balozi wa Uingereza huku vifungo vya Koti amefunga vyote...ni kutofahamu ..na tukasema hapa ukumbini na amejirekebisha vilivyo anagalia sasa hivi ni mtanashati . President , Vice P na viongozi wetu wanapokosea ni lazima tuwape tahadhari .
    Kukaa ughaibuni ni kujifunza mengi katika maisha na kuweza kuwa kioo kizuri cha jamii .Kuwafundisha mazuri wenzetu .Kaka Suit ina heshima yake lazima tuilinde .
    Kama Kaka Kiroba unataka darasa la Suit sema tu tuitoe hapa ukumbini .
    Kidumu !
    Kisiwani

    ReplyDelete
  9. huu urafiki wa haraka haraka na hawa jamaa angalieni sasa hivi nchi itauzwa hawa jamaa kwenye mali hawana ujamaa wala urafiki hapa ndio utamkumbuka nyerere aliwaambia hawa jamaa kama hatuwezi kuchimba tutangoja mpaka tutapoweza kufanya wenyewe sasa mjomba anaenda mbio kujaribu kufanya nao ujamaa mshtueni angalia walivyomfanya saddam alikuwa mshikaji wao ile mbaya hakuamini walivyomchenjia haya yetu macho

    ReplyDelete
  10. jamani kuweni macho minavyojua marekani bwana aendi sehemu bure bure,na mimi kauoga kameniingia huyu mtu anataka nini?kuna kitu kaona si bure.labda tusilalamike sana anaweza kuwa na habari njema!

    ReplyDelete
  11. Mimi binafsi kwa kweli ninwasiwasi sana na huu ukaribu wa Kichaka kwa Kikwete na Tanzania kwa ujumla.Hawa watu wanajali masilahi yao tu.Hawana kingine.Nafikiri Kikwete awe macho kwani mimi nimekaa na wazungu yaani huwanza benefit kwanza kabla ya kuanza chochote.Na ni wajanja kweli kama si mwerevu.Kwani ni wakarimu sana mdomoni na machoni kumbe wanakupumbaza tu.Kikwete usije ukatuuza bwana.Umeanza vita ya mafisadi ndani ya nchi,Ukifanikiwa raisi ajaye aanze vita na haya mataifa manyonyaji hapa dunia ndipo tutafika walipo wachina,na wengine.Please Kikwete be carefully na hao watu.Ni wanyama hao.

    ReplyDelete
  12. Jamaa wanamuweka sawa kama awajamuingiza katika line tayari wewe usafiri kutoka tanzania mpaka marekani ukae siku tatu halafu unarudi bongo halafu unatuambia umealikwa kutembea hiyo ni wazi jamaa(BUSH) kazi inakwisha na hawa ni wafanyabiashara wameshaona mali bongo sasa wanapiga mahesabu wewe nchi zote hizi africa misaada tunapewa sisi tu urafiki umepita kiasi msilete kamba hapa

    ReplyDelete
  13. nyerere mwenyewe alibeba box uk mpaka akamaliza shuleyake acheniwivu watu wanatafuta maisha hatuibi,
    kazi yoyote halali ni heshima
    tunakujakua mabosiwenu pigenimayowetu.

    teh teh teh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...