bango la jirushe
mkurugenzi wa masoko wa zain, margareth kositany na mkurugenzi wa mauzo, herbert louis, wkitanganza kuzinduliwa kwa huduma za 'Jirushe, leo makao makuu ya zain, dar.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain yenye mtandao ulioenea katika nchi 22 barani Afrika na Mashariki ya Kati, imezindua promosheni mpya ya Jirushe, itakayowawezesha wateja kutumia pesa kidogo kila siku kwa kupiga simu za mtandao wa Zain kwenda Zain.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Tanzania, Margareth Kositany, amesema leo Dar kwamba wanachotakiwa kufanya wateja wa Zain ni kuandika neno JIRUSHE kila siku na kutuma kwenda namba 15354 ili kupata huduma hiyo na kuendelea kupiga simu na kuongea bure kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi saa 12:00 jioni, siku za wiki.

“Zain leo inafurahia kuzindua ofa mpya ya kupiga simu bure inayojulikana kama JIRUSHE ili kuwawezesha wateja wetu kutumia pesa kidogo na kuendelea kupiga simu bure, na kuweza kuwasiliana kwa urahisi na ndugu, jamaa, marafiki, washirika wao kibiashara, familia na wawapendao,” alisema Mama Kositany.

“Ofa hii ni kwa simu za Zain kwenda Zain pekee na ni kwa wateja wa malipo ya awali. Hakuna mtandao mwingine utakaokuwezesha kuwasiliana kwa urahisi na watu wengi zaidi kuliko Zain,” alisema.

“Hakuna mtandao mwingine unaomwezesha mteja kupata faida zaidi kila siku zaidi ya Zain, na wateja wetu wataendelea kufaidika kupitia promosheni zetu za JIRUSHE na Mambo Wikendi,” aliongeza.

Kupitia promosheni ya Mambo Wikendi, wateja wa Zain wamekuwa wakipiga simu kwa bei ya Tsh 1 kwa sekunde kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3 usiku hadi saa 12 asubuhi na saa 24 wikiendi nzima.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Meneja Masoko huyo wa Zain, alisema Zain imedhamiria kuboresha maisha ya wateja wake, na hii pia ni namna nyingine ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi.

“Kupitia JIRUSHE na Mambo Wikendi, wateja wetu watanufaika na viwango vyetu ambavyo vitawawezesha kuongea kwa kiasi kidogo cha pesa, nah ii itawafanya wajione wako katika Ulimwengu Maridhawa,” alisema Mama Kositany.

Zain Tanzania ambao ndio mtandao wa simu unaotoa huduma bora zaidi nchini, hivi sasa ina wateja zaidi ya milioni 3 na inatarajia kuwa na wateja zaidi ya milioni 4 kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ninavyofahamu Zain ndiyo iliyokuwa Celtel. Je hii inamaanisha kuwa wateja wa Celtel waligeuka kuwa wateja wa Zain pale tu Celtel iliponunuliwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...