visitors flock at the Tanzania pavillion in London
By Ayoub mzee
The world travel market has opened this week at the Excel exhibition center in London. The Tanzania delegation is led by the Tanzania minister of Tourism Hon. Shamsa Mwangunga and the parmanent secretary minister of tourism Mrs Blandina Nyoni.
This exhibition has opened on the back drop that Tanganyika wilderness camps is to due open an upmarket tented lodge at Lake Masekin in the Ngorongoro conservative area in 2009. And that Lateka Safaris is introducing new bird watching packages for two come 2009.
Also the brand new 200-room Movernpick Resort is due to open near Arusha in 2010 at the foot of mount meru.
Speaking at the event Mama Nyoni has said that business and tour enquries have been very high on the second day compared to last year
------------------------------------------------
Na Mwandishi Maalum, London
TANZANIA imeendelea kufanya vizuri mwaka huu katika kutangaza utalii wake kwenye maonyesho makubwa ya biashara ya utalii jijini London.
Hali hiyo imedhihirika hapa tangu Jumanne ambapo watu wengi wa mataifa ya Ulaya na kwingineko walionekana kutobanduka kwenye banda la Tanzania katika maonyesho hayo yanayofanyika eneo la Excel jijini hapa yakishirikisha zaidi ya mataifa 140 kutoka kila pembe ya dunia.
Karibu tangu saa 3:30 asubuhi mabanda ya Watanzania, wakiwemo wa idara za serikali na zile za binafsi, yalikuwa yamefurika watu wakitaka upatiwa taarifa zihusuzo vivutio vya Tanzania, huku wakichukua vipeperushi na machapisho mbalimbali kabla ya baadaye kuzama kwenye burudani ya ngoma za asili iliyokuwa ikishushwa na kundi la Sisi Tambala.
“Tumefarijika sana na manyesho haya, ambapo hakika Tanzania inazidi kupanda mwaka hadi mwaka kutokana na jinsi inavyotangaza utalii wake, tunaamini kwamba idadi ya watalii kwa msimu ujao itaongezeka zaidi,” alisema Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Peter Mwenguo.
Mwenguo alisema kwamba, kwa jinsi walivyojitahidi kuitangaza Tanzania katika sekta hiyo ya utalii wanaamini ujio wa wageni hao mwaka ujao utakuwa mkubwa zaidi kuliko miaka iliyotangulia.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Blandina Nyoni, alisema jana jijini hapa kwamba, Tanzania itegemee idadi kubwa ya watalii msimu jao, lakini akaonya kuwa changamoto nyingine zinapaswa kushughulikiwa haraka ili kutowakatisha tama watalii hao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na miundombinu kama mawasiliano ya barabara na huduma za vyakula na malazi, ambazo alisema zinapaswa kuboreshwa zaidi kwa kushirikisha wadau wote.
“Nadhani umejionea mwenyewe jinsi hali ilivyo, TTB wamejitahidi sana kuwaelewesha wageni mblaimbali waliotembelea banda letu, na wale waliovutiwa, ambao ndio wengi wamekuwa wakiwasiliana na makampuni mbalimbali yaliyopo kwenye maonyesho haya kuona kama wanaweza kuja Tanzania kutalii.
“Tunahitaji mpango wa ushirikiano wa amoja baina ya serikali na sekta binafsi utekelezwe kwa bidii sana na sisi kama serikali tutahakikisha tunajitahidi kuweka sera nzuri na kushirikiana na wadau wetu wenye hoteli na kampuni za utalii kuona tunashughulikia changamoto hizi ili kuweka nchi yetu kwenye chati ya dunia,” alisema.
Maonyesho hayo, ya pili kwa ukubwa duniani baada ya yale ya ITB ya Ujerumani, yanashirikisha zaidi ya wafanyabiashara 120 wa sekta ya utalii nchini Tanzania.
Wafanyabiashara hao wanatoka katika makampuni 61 yanayojishughulisha na huduma za utalii, hoteli na sekta nyinginezo, idadi ambayo inaonekana kuongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni.
“Siku zote tumejitahidi kuutangaza utalii wetu nje ya nchi ingawa baadhi ya watu wamekuwa wakikejeli juhudi zetu hizi, lakini siyo siti, atasaidina sana kukuza pato la taifa kupitia sekta hiyo.
Hii ni mara ya 16 tangu Tanzania ianze kushiriki maonyesho hayo kiasi cha kuongeza na imefaidika na maonyesho hayo ambapo yameongeza idadi ya watalii kutoka Uingereza kwa kiasi kikubwa.
“Ingawa Waingereza wamepitwa kidogo mwaka 2007 na watalii kutoka Marekani, lakini hakika maonyesho haya yamekuwa chachu kubwa kwa idadi ya watalii wanaokuja nchini,” alisema Mwenguo, mkurugenzi wa TTB.
Aidha, alisema kwamba kuongezeka kwa watalii kutoka Marekani kulitokana na kutangazwa kwa vivutio vingi vya utalii katika nchi hiyo kuanzia mwaka 1999 wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.
Hata hivyo, Mwenguo alisema, maonyesho hayo yanatarajiwa kuongeza idadi ya watalii mwaka huu, ambapo wanatazamia watalii 800,000 watakuja kutembelea Tanzania na hivyo kuiingizia serikali kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.1 ikilinganishwa na mwaka 2007, ambapo jumla ya watalii 719,000 walikuja na serikali ikakusanya dola bilioni 1.
Mbali ya wafanyabiashara hao, serikali nayo kwa kiasi kikubwa itajitahidi kuutangaza utalii, ambapo ujumbe wa maofisa 19, wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi, wameshiriki maonyesho hayo.
Maafisa hao kutoka Tanzania Bara ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsha Mwangunga na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni, Mkurugenzi wa TTB Peter Mwenguo, Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Amat Macha na Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena.
Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Modestus Lilungulu, Mkurugenzi wa Tanapa Gerald Bigurube, Mkuu wa Hifadhi ya Kitalo, William Mwakilema, Kaimu Muhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro B. Murunya na afisa utalii wa mamlaka hiyo, Ole Mariki Lazaro pamoja na maafisa wengine.
Kutoka upande wa Visiwani ni Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji, Samia Sululu Hassan, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Issa Ahmed Othman, Katibu Mkuu wa kamisheni hiyo, Dk. Ahmad H. Khatib, Mkurugenzi wa Chuo cha Utalii, Mohammed Omar, Mkurugenzi wa Masoko wa kamisheni Ali Khalil Mirza, Meneja wa Bwawani Hotel Juma Shomari Juma, na Afisa Habari, Mawasiliano na Utalii, Amour Mtumwa Ali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. hii tanganyika hapa inamaanisha nini? si tumeambiwa haipo tena hii?

    ReplyDelete
  2. ya na pia muwambie mlima kilema kiaro upo tanganyika sio kwa obama

    ReplyDelete
  3. Jamani hii exhibition iko wapi? Tungependa na sie tuudhulie

    ReplyDelete
  4. Sasa watu wenyewe wanafanya exhibition wakiwa wamenuna na kuuchuna namna hii??!!! Hii picha ya chini si park warden incharge wa Kitulo National Park!!? Mwakamela au Mwakilema?! Umenuna mno na sidhani kama watu wanakuja kwa uzuri wa maonyesho au uzuri wa vitu. Hata picha ya juu. Lazima mtabasamu ati! Haya tabasamu sasa.

    ReplyDelete
  5. We annony wa 2.00 unayemsema Mr. Mwakilema hizo ni chuki zako binafsi tu huna lolote inaelekea una kijiba cha roho na baba wa watu, na inaelekea hujaenda shule ama shule haijakusaidia.Kasome acha wivu wa kijinga. Nyie ndo wale BMW aliwambia mna WIVU WA KIKE. Lione kwanza KASOME. MSSSSSY!!

    ReplyDelete
  6. wako wapi tupeni address.

    ReplyDelete
  7. supportive staffs au junior officers wako wapi waudumie watu??mana sielewi mara mawaziri na wakurugenzi ndo wako "ktk banda la maonyesho"
    JAMAN IZI PER DIEMS IZI??ata kwaachia junior officers basi nao wakale raha uropa wapi wakubwa wameganda tu,,i can imagine mkurugenzi wangu ati kaenda bandani,uyo shamsa yuko wapi sasa?

    ReplyDelete
  8. Mimi bado sijaridhika na jinsi sekta ya utalii inavyotumika kama nyezo ya kukuza uchumi wetu,kwanza kama chanzo muhimu cha fedha za kigeni(sijui ni Dola ngapi zinazoingizwa nchini kila mwaka);pili,kama kinasa biashara ambacho tungekitumia kikamilifu ili kuuza biashara yetu nchi za nje na kuvutia wawekezaji wakati huohuo;tatu kama kituo cha mafunzo ya biashara ya utalii duniani na hifadhi ya mazingira kwa manufaa ya nchi zote duniani.Wapo watakao sema tumenufaika sana na Utalii toka miaka ya 1960(?),lakini manufaa hayo yako wapi na katika nyanja zipi?Au mapato mengi yamekuwa yakiishia nchi za jirani na hapa kwetu watalii wakarubuniwa waingie na fedha za hapa hapa Afrika ya Mashariki?Na hivyo rasilimali yetu ya utalii ikatumika kuzinufaisha nchi za jirani badala ya kutatua matatizo yetu wenyewe?Mbona kiwango cha umaskini vijijini kimezidi kiwango cha kutisha licha ya mapato hayo ya utalii kama inavyodaiwa?Je,hapa nchini tuna chuo gani cha utalii chenye hadhi ya kimataifa katika miaka yote hiyo?Je,kuna msukumo gani wa kitaifa katika kuwafundisha vijana wetu mashuleni wazifahamu lugha mbalimbali kuu za ulimwenguni?Kama vile Kifaransa,Kispanish,Kirusi,Kijerumani,Kichina,Kijapani,ki Xhosa,ki Fulani,kireno,kiitaliano,kigiriki na nyinginezo muhimu katika mahusiano ya kimataifa hususan katika biashara hii ya utalii?Je,kuna jitihada gani za kujenga Hoteli za kisasa zenye hadhi ya Kimataifa sehemu mbalimbali nchini zenye vivutio vya utalii?Serikali imefanya jitihada gani katika kuiwezesha Sekta Binafsi iwe na uwezo kitaaluma na kifedha na kinyenzo katika kuingia katika soko la kimataifa la biashara ya utalii na uchumi wetu ukanufaika kupitia kwao?Ni maswali mengi ya aina hii yanayo nifanya niwe na wasiwasi kama kweli tunacho kizungumza siku zote ndicho kinacho tendeka kwa vitendo!Kwa mfano onesho hilo la London lilitangazwa kiasi gani humuhumu nchini watanzania wakapata fursa ya kuchangia kwa hali na mali kabla hata ya tukio lenyewe?Sisi wenyewe Watanzania tumepigwa na butwaa kumbe kuna promosheni ya utalii London ya namna hii pasipo kutaarifiwa mapema?Huo utalii mtau promoti nyie wenyewe bila ya support ya watanzania locals mtaweza?this is your first mistake.

    ReplyDelete
  9. EXHIBITION IPO EXCEL,PANDA TRAIN MPAKA CANNING TOWN,UKIFIKA SHUKA,THEN PANDA TRAIN JINGINE LINAITWA DLR LINALOKWENDA BECKTON,UTASHUKA EXCEL!NI VITUO VITATU KUTOKA CANNING TOWN,WALA HAPAPOTEZI,UTASHUSHWA NA TRAIN MLANGONI MWA EXCEL!

    ReplyDelete
  10. haaa! Sasa we annon Nov 12 10am una nini hivi? Kwani wewe umeelewaje comement yangu kuhusu Mwakilema au Mwakamela? Was just a good comment to take, if you undersstood what it meant!. I did mean anything bad. Nina wasi wasi nan wewe. Uelewa wako nadhani wa kushikilia. Hapa kwenye blog kama uelewi unauliza. Kama hujui, kama ulivyo wewe unakaa kimya!

    ReplyDelete
  11. Nimemuona Mzee wangu Bwana Gerald Bigurube wa TANAPA. Mungu akulinde na akutie nguvu sana Mzee wetu.

    Tanapa wanatoa Tax kubwa kuliko kampuni nyingine yoyote tanzania.. mabillioni ya dollar (sio shilingi)

    yaani huyu mzee ni 'corruption-free' na ni mchungaji.. Amen mzee wetu!

    ReplyDelete
  12. we annon wa 3.36 pm matatizo unayo wewe, comment yako ilionesha una chuki binafsi kbs. watu wameenda kufanya kazi siyo kuuza sura na kucheka cheka. Pole sana kama kimekuuma mwakani utaenda wewe kwenye exhibition!!!

    ReplyDelete
  13. annony wa 3.36 pm kajifunze kwanza kuandika vizuri kiingereza mana unaandika broken sana. Nenda The english fountain au kawaone british council kwa msaada zaidi. Pole bila msaada.

    ReplyDelete
  14. Jamani hivi vivutio vyetu vya utalii si vina wataalam wa kuviuza?(sales personel au sales agents). Hawa sales agents wana uzoefu na wanavijua hivi vivutio inside out maana wamesomea jinsi ya kuviuza, sasa inakuwaje mtu kama Waziri, wakurugenzi, katibu wa wizara na kadhalika ambao hata hajawahi kufika ktk vivutio vyote hivi wanaenda kukaa ktk banda la Tanzania? Jamani tungewaachia wenye fani yao ndio watuwakilishe huko maana wana majibu ya maswali yote, nina uhakika hapo kuna maswali yanaulizwa na hao potential watalii ambayo hao wakurugenzi watashindwa kuyajibu.Walao basi hata mameneja wa vivutio hivi ndio wangeenda kama inaonekana maofisa mauzo watafaidika sana kufika ulaya, hapo ukiangalia utakuta ni asilimia 10 tu ya "right" people ndio wapo hapo.
    Hivi nchi nyingine nazo zinapeleka mawaziri na wakurugenzi kweli???
    Tupeleke the right people jamani ndio tutafaidika na maonyesho kama haya.
    These are just my views.

    ReplyDelete
  15. We annon 13 9:48 wala siwezi kuwa na chuki binafsi. For what reason? Watu wanaenda kwenye maonyeso wanatakiwa wawe wachangamfu na siyo kununa kama kwamna hawana uhakika wanachoonyesha kama inavyoonekana hapa. Safi uone mambo. Nenda Asia, Thailand au Malaysia hata Hongkong. Unapoingia Airport tu unavyopokwa na Tabasamu huwezi sahau maishani! Mitaani kote watu wanatabasamu. Sasa hapo watu wamenuna kama vile wamekata poachers!

    Na wewe wa kiingereza, annon 13 9:50 nimekusikia. Sawa kabisa. Ila ningesoma chako ningefurahi zaidi. Kila siku ni siku mpya. Tunajifunza. Sijui mwenzangu wewe!

    ReplyDelete
  16. Hivi kweli huyo ndiyo GM wa TANAPA? Anaonyesha naye??! Mhh! Kwa kweli bongo tumekwisha. Yaani boss kaacha ofisi kwenda kuonyesha maonyesho?!! Sipati picha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...