maafisa wa polisi wakikagua hali halisi
magari kibao yasagwa
baada ya kukaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10 bila kugombolewa, na baada ya wenyewe kuingia mitini kwa kushindwa kulipia ushuru, magari kibao yamekula kisago huko kwa watani wetu wa jadi, na magari 200 zaidi yanatarajiwa kupata kisago kama hicho mwisho wa mwezi huu. wadau mnasemaje, hapa dar libeneke kama hili linafaa kuja?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kwa mtazamo wangu nadhani baada ya kukaa miaka kumi bandarini hayafai na si salama kwa matumizi. Hapa nazungumzia viwango vya moshi na uimara wa vyuma kutokana na chumvi ivukishwayo na bahari. Hivyo ni sahihi kusagwa. Lakini pia sidhani kama walistahili kuyaacha yakakaa pale kwa miaka yote kumi. Wangekuwa na utaratibu wa kuyapiga mnada baada ya miaka kama miwili ili kuondoa uwezekano wa wenye nayo kuyasusa na wao pia kukosa pesa kwa kutokuwa na sehemu ya kuhifadhi magari mengine ambayo yangeweza kukombolewa ndani ya muda mchache. Ukweli ni kwamba hata kama nikipata pesa sasa, sidhani kama ningeweza kukomboa na ama kununua gari iliyokaa bandarini kwa miaka kumi maana haitakuwa salama na itagharimu matengenezo. Hivyo ndivyo nionavyo tatizo, lakini tukumbuke kuwa NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO LAWEZA KUWA TATIZO.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Si sahihi ingelikua madawa ya kulevya au au pembe za ndovu ningeliunga mkono.Hayo magari yamekaa bandarini kwa miaka 10!Nayalikua yakilindwa na mamlaka husika ambapo wafanyakazi wanalipwa mishahara ambayo inatokana na kodi za walala hoi.Kwa maoni yangu nafikiri ingelikua bora magari hayo yapigwe mnada na na pesa zitakazopatikana zitumike katika kuimalisha sekta mbalimbali katika jamii hospitali,watoto yatima au kuimalisha bandari yenyewe n.k.Hapa unapocheza mchezo wa wote tukose ni serikali kujikomoa wenyewe nani analipa gharama za kuifadhi magari hayo kwa kipindi cha miaka kumi?Nani analipa gharama za kuyaangamiza magari hayo.Ni wazi hapa kunawatakaofaidika na si walalahoi au serikali.Magari 20 yatakandamizwa kama mfano nayatakayobaki yatatoka kupitia mlango wa nyuma kimazingaombwe haya ni mazingaombwe.MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete
  3. kwanini serikali isiyauze na kupata extra mapato na kusaidia wananchi wake kwenye nyanja nyingi tu badala ya kuyadestroy?

    ReplyDelete
  4. Sasa hayo masalio wanayafanyia nini? mimi naona wengeuza kama spears au kwa viwanda vya chuma vinavyotengeneza nondo ili kurudisha baadhi ya gharama za storage.

    ReplyDelete
  5. Mzee wa Changamoto

    You are genius...

    ReplyDelete
  6. Mimi naona huu ni ujinga kwa nini wasiwe na muda wa kama miaka miwili kama mtu hujakomboa gari lake basi linapigwa mnada? Wangeyauza mapema kulipia gharama ya kuyahifadhi kwa muda huo wote. Kuyaweka kwa muda wa miaka 10 halafu kuyafanya hivyo ni kuengeza pollution ulimwengu huu.

    Na pia wangeangalika kwanini watu wanashindwa kukomboa magari yao? Ni ushuru mkubwa sana kama vile kukomoana vile. Hivi wanadhani mtu ashughulike gari lake kulifikisha hapo halafu alidump hivi hivi? ushuru wa nchi zetu uliwekwaga kudiscourage importation na kuprotect our factories and products as if we have any....lakini kuna vitu vya kudiscourage kama kuingiza chai ya south Africa, coffee ya columbia, (pamba) kutoka UK and USA. Sasa magari tunacho hata kiwanda cha magari jamani?

    Inabidi waangalie haya mambo kuna sheria zingine zimepitwa na wakati sana. Wajue kuwa na gari sio leisure tena au wanataka tuendelee kubeba wagonjwa na machela au punda wakati wao wanatembea na magari mazuri?.

    ReplyDelete
  7. Hizi ndo bangi, matope ya viongozi wa afrika. inawezekana kabisa walioingiza magari hayo wameshindwa kuyatoa kwa sababu kadhaa, kama vifo, ugonjwa, kutowasili kwa hati za kuyatolea, ukata n.k sasa kwa nini yasiuzwe yakatunisha mfuko? huu si ujinga?
    sasa unayapondaponda halafu unagharamia kuya DISPOSE OFF si ujinga huu.

    ReplyDelete
  8. Thanx alot ANON 4:08 AM. Karibu kijiweni

    ReplyDelete
  9. hivi nyie mnabishana nini na wakenya their selfish bas wana roho mbaya sana ? huwa hawajui wanyonge.
    during x'mass nilikuwa nasikiliza bbc na watoto waliokosa makazi baada yaa vita vya wenyewe kwa wenyewe hakikyamungu nililia hawa watu ni wanyama kweli kweli

    ReplyDelete
  10. HAMA KWELI AKILI NI NYWELE NA KILA MTU ANA ZAKE.ACHA TUENDELEE KUWA MASKINI NA AKILI ZETU FINYU.HAYO MAGALI YANGEPIGWA MNADA ZAMANI SANA NA HELA INGETOSHA KUREKEBISHA MAISHA MALE KIBIRA.
    KWELI CHIZI SIO LAZIMA AOKOTE MAKOPO.

    ReplyDelete
  11. Nenda kakate tiketi nchi yoyote katika ofisi ya kenya airways utakuta watu kede lundo wanalalamika wamepoteza mizigo,na kuapa hatasafiri tena nao. hata kama rahisi, hawa jamaa si watu.

    ReplyDelete
  12. Ama kweli kusoma ngumbaru kuna kazi zake.Sasa hizo gharama za kukaa bandarini kwa muda wote huo ni nani analipa?Hapa ndio unaona tofauti ya sisi ni Western, wanathamini mali, kwa hiyo ni bora wangeliuza na kutumia hizo pesa kwa lulelea watoto yatima kibao.Yaliyobaki msifanye ujinga kama wa haya yauzeni yanayobaki fungueni salvage area uzeni parts ili muwaongezee askari marupurupu Uko wapi Kibaki mbona unarudi nyuma?

    ReplyDelete
  13. WA-KENYA WATU WABAYA WANA ROHO MBAYA, SI VISA ZA U.K. ZIMEHAMISHIWA HUKO BASI MTANIAMBIA TUTAKAVYOLIZWA MIMI YAMENITOKEA MPAKA NIKA MVA BALOZI KWA NGUVU NIKAPATA FASTA FASTA, NILIOMBEA KENYA KWA VILE NILIKUWA HAPO. HAWA WATU NI JEURI HAWAFAI MTANIAMBIA.

    ReplyDelete
  14. Ujinga na roho mbaya tuu hakuna chochote. Kama Hamuamini nyie wakaribisheni kwenye ardhi yenu kama hamkuwa wenyewe watumwa kwenye nchi yenu

    ReplyDelete
  15. WAKENYA HAYO MAGARI SI MNGEYATOA DONATION AU MATUMIZI MENGINE WENZETU. HATA HAPA MAREKANI MAGARI KAMA HAYO YANAPIGWA MNADA NDIO MAANA HATUENDELEI

    ReplyDelete
  16. Photoshop ..........hapo cio Kenya!!!

    ReplyDelete
  17. Kwa nini wasingeuza na kudonate hizo pesa kwa wasio na kipato?

    ReplyDelete
  18. mapungufu ya shule hayo!hao viongozi nafkiri hawakuelewa darasani kama walienda,maana mtu aliyekwenda shule hawezi kufanya huo utumbo.wangepiga mnada ingesaidia kuboost kipato cha serikali halaf wangetatua shida zingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...