Na Mwandishi Maalum,

MIRADI 15 mikubwa ya ujenzi wa barabara nchini imekamilishwa katika miaka mitatu iliyopita na miradi mingine 33 iko kwenye hatua mbali mbali za kukamilishwa katika jitihada kubwa za kuboresha mawasiliano ya barabara nchini.

Kati ya miradi hiyo 15, barabara saba zenye urefu wa kilomita 441 na zilizogharimu kiasi cha sh bilioni 161.2 tayari zimefunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Miradi mingine minane yenye urefu wa kilomita 370.95 na iliyogharimu kiasi cha sh bilioni 135.16 tayari imekamilika na inasubiri kufunguliwa na Rais Kikwete.

Hayo ni baadhi ya maelezo ambayo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Ephraim Mrema alimpa Rais Kikwete mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano wa kutathimini utendaji wa Serikali, Wizara na mashirika yaliyoko chini ya Wizara uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Ijumaa, Januari 16, 2009.

Katika mkutano huo uliohusu Wizara ya Miundombinu na mashirika yake, Mrema alimwambia Rais Kikwete kuwa miradi mingine ya barabara yenye urefu wa 2, 706.81 yenye kugarimu sh bilioni 1, 165.29 inaendelea kujengwa katika sehemu mbali mbali za nchi.

Alisema kuwa mchakato wa kwanza utekelezaji wa miradi mingine mitano mikubwa umekamilika na unasibiri kutiwa saini, mingine 18 iko kwenye hatua ya manunuzi, mingine 23 iko kwenye hatua ya maandalizi ya usanifu.
Alisema kuwa usanifu wa miradi mingine 11 umekamilika lakini bado fedha za ujenzi wa barabara hizo zinaendelea kutafutwa na Serikali.

Mrema alisema kuwa miradi saba iliyokamilishwa na kufunguliwa na Rais Kikwete katika miaka mitatu iliyopita ni Buzirayombo-Geita, Issuna-Singida, Singida-Iguguno, Iguguno-Sekenke, Sekenke-Shelui, Tinde-Mwanza/Shinyanga Border na Nzega-Tinde-Isaka. Barabara hizo zote zimejengwa kwa kiwango cha lami.

Kati ya miradi hiyo, miwili imegharimiwa na Serikali ya Tanzania (GOT), mwili imegharimiwa na Jumuia ya Ulaya (EU) na mitatu imegharimiwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia (WB).

Mrema alisema kuwa miradi minane ambayo imekamilika na inasubiri kufunguliwa na Rais ni Kyamyorwa-Buziyarombo, Mbwemkulu-Mingoyo, Sam Nujoma Road, Daraja la Ruvu, Tarakea-Rongai-Kamwanga, Kidahwe-Uvinza, Kisili-Buhigwe, na Uvinza-Malagasi.

Kati ya miradi hiyo, mitano imejengwa kwa kiwango cha lami na mitatu imejengwa kwa kiwango cha changarawe na kati ya yote, mitano imegharimiwa na Serikali ya Tanzania, na mitatu ya kiwango cha lami imegharimiwa na Shirika la Mafuta Duniani (OPEC).

Mrema alisema kuwa miradi 33 ambayo ujenzi wake unaendelea ni Geita-Sengerema, Manyoni Isuna, Sengerema-Usagara, Mwandiga-Manyovu, Kagoma-Kidahwe, Ndundu-Somanga, Dodoma-Manyoni, Naguruku-Mbwemkulu, Bagamoyo-Msata, na Mbeya-Lwanjilo ambayo yote inagharimiwa na Serikali ya Tanzania.

Mingine ni Arusha-Mananga unaogharimiwa na Banki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kilwa Road Phase Two inayogharimiwa kwa pamoja na GOT na shirika la JICA la Japan, Chalinze-Tanga Phase One unaogharimiwa na Tanzam Highway (Iyoyi) inayogharimiwa na DANIDA, Marangu-Rombo Mkuu unaogharimiwa na NORAD, Daraja la Unity Bridge linalogharimiwa na GOT na Serikali ya Mozambique, na Nelson Mandela unaogharimiwa na EU.

Mrema aliitaja miradi mingine kama Tingi-Kipatimu, Nanganga-Ruangwa, Nachingwe-Kilimarondo, na Nachingwe-Liwale ambayo yote inagharimiwa na OPEC na inajengwa kwa kiwango cha changarawe.

Miradi mingine ni miradi mingine ni miradi miwili ya kuboresha mwasiliano Mkoani Rukwa na mingine miwili ya Jiji la Mwanza ambayo yote inagharimiwa na GOT na Wakala wa Maendeleo wa Kimataifa (IDA), Masasi-Mangaka Phase One, Masasi-Mangaka Phase Two ambayo inagharimiwa na GOT kwa kushirikiana na JICA, Rombo Mkuu-Tarakea unaogharimiriwa na BADEA, barabara mbali mbali za mikoa mbali mbali yenye urefu wa kilomita 497 na inayogharimiwa na DANIDA.

Mrema aliitaja miradi mingine kuwa ni Kidatu-Ifakara, Singida-Katesh, Katesh-Dareda, na Dareda-Minjingu.

Mrema alisema kuwa miradi mikubwa ambayo inasubiri kutiwa saini ili utekelezaji uanze ni Same-Mkumbara, Mkumbara-Korogwe, Kigoma Lusahunga na ujenzi wa barabara za Tanga mjini.

Alisema kuwa miradi iliyoko katika hatua ya manunuzi ni Tabora-Nyahua, Mkata-Handeni, Korogwe-Handeni, Handeni-Mziha, Mwigumbi-Maswa-Bariadi-Lamadi Bariadi-Lamadi, Dodoma-Babati, Sumbawanga-Mpanda, Sumbawnga-Kanazi, Sumbwanga-Mpanda-Kanazi-Kizi-Kibaoni, Kyaka-Kayanga-Bugene, Sumbawanga-Matai-Kasesya, Barabrara za Kuzungumza Mkoa wa Dar es Salaam (ring roads) ambao ni mradi maalum, na Kitumbi, Segera-Tanga.

Mingine ni Tunduma-Laela-Sumbawanga, Tunduma-Kana, Tanga-Horohoro, Songea Mbinda, Songea-Namtumbo ambayo yote itagharimiwa chini ya msaada wa MCC wa Serikali ya Marekani.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. INASIKITISHA KUONA MIRADI MINGI YA KIGOMA NI YA KIWANGO CHA CHANGALAWE. KIGOMA NAFIKRI WAZO LA KUJITENGA SIO BAYA KWANI SERIKALI IMETUTENGA SIKU NYINGI. HAKUNA BARABARA, UMEME, NA MAJI.
    MIRADI YA LAMI TZ YOTE WANAGHALIMIA WATU WA NJE,MADENI, SERIKALI HAISEMI KUWA NI MADENI, TA TZ YOTE CHANGARAWE, WIZI MTUPU.

    ReplyDelete
  2. Hapa naona ni usanii tuu, miradi mingi hapa imeanzishwa na serikali tukufu ya bw. mkapa ya awamu ya tatu,, kuweka katika maendeleo ya serikali ya awamu ya nne ni usanii.... Kikwete hajafanya la maana so far...

    ReplyDelete
  3. kama hao kigoma wana mawazo ya kujitenga sasa sisi wa unguja na pemba tusemeje!! sioni hata mradi mmoja wa visiwani!!

    ReplyDelete
  4. Tangu JK aanze kutembelea taasisi mbalimbali kwenye wizara ya miundo mbinu...

    Kwa mara ya kwanza nimeona taarifa ambayo Rais ameambiwa tu, yeye hajatoa amri yoyote... inaonyesha hii taasisi ya TANROADS angalau wanafanya kazi yao vizuri

    ReplyDelete
  5. KUJENGA BARABARA KWA KIWANGO CHA CHANGARAWE NI UPOTEZAJI WA PESA ZA UUMA NA KUWAACHIA VIZAZI VYETU VIJAVYO MADENI YASIYO NA MSINGI, KAMA HAMNA UWEZI WA KUJENGA KWA LAMI NI BORA KUTOKOPA PESA KWA AJILI YA CHANGARAWE KWANI INADUMU ONE YEAR NA BARABARA INABAKI PALEPALE KAMA ILVYOKUWA BEFORE CHANGARAWE, KAMA TUNAKOPA PESA BASI TUKOPE ZA LAMI SI CHANGARAWE HUO NI UPOTEZAJI WA PESA ZA UMMA NA NI UZEMBE MTUPU. NDUNDU SOMANGA HUU NI MRADI WA SIKU NYINGI HADI LEO HII HAUJAISHA/ NASHANGAA, TUJIKUNE TUNAPOWEZA KUFIKIE KAMA HATUNA UWEZO SI BUSARA KUANZA MIRADI MINGINE WAKATI MINGINE HAIJAISHA SIMPLY BECAUSE YOU NEED POLITICAL CAPITAL, TUMALIZE MMOJA NA NDIPO TURUKIE MWINGINE. SIJASIKIA BARABARA YA MASASI SONGEA AMBAYO NI MBAYA SIJAPATA KUONA HAPA DUNIANI. NI VIZURI KUKAWA NA BARABARA YA LAMI TOKA DAR KWENDA SONGEA KUPITIA KILWA, LINDI, MASASI TUNDURU HADI SONGEA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI BARABARA YA IRINGA.

    ReplyDelete
  6. Kabla hujalaumu uliza uambiwe. Walio Kigoma wanaona bara bara ya Kigoma Kasulu imeanza kujengwa kiwango cha lami!!!!

    ReplyDelete
  7. WAZO LA LEO:

    Bora muwe mnatupatia hizo takwimu ili tuweze kufahamu serikali yetu ya awamu ya nne inaendelezaje miundo mbinu nchini.

    Kuna viongozi wa awamu zilizotangulia wamekuwa wakijisifu kuhusiana na uboreshaji miundombinu nchini, na wakitaka huruma ya wananchi kwa madhambi waliyoyafanya, kwa kuwa waliboresha miundombinu.

    Hicho kisiwe ni kigezo cha huruma ya wananchi, kwani hata awamu ya nne inaonyesha kwamba imeweza kuboresha miundombinu

    ReplyDelete
  8. Let us be honest:
    1. Why should every road be opened by the President, and others have even to wait until he gets time? What is this?
    2. This government has been around for three years, that means if a road project started just after the installation of the fourth phase government, then the credits should go to the previous one? Be honest guys.

    ReplyDelete
  9. Misupu tunaomba usituwekee taharifa za ccm huku waeleze watumie mitandao waliyonayo kama vile www.ccmmarekani.blogspot.com sio wanatufata huku kwenye blog ya jamii. Hatuwataki hao mafisadi

    Uk

    ReplyDelete
  10. Michuzi habari.Kwa kweli tuwe waungwana,nina wasiwasi na hao wanaolaumu hili suala la serikali,nadhani hawa wengi ni wanaoishi Daresalaam au wanaokaa majuu,wakirudi wanaishia Dar.Serikali imefanya kazi nzuri sana kwenye hizi barabara na lazima tuishukuru na hasa hii ya kati ya Dar-Mwanza.Zamani ilikuwa ni balaa.Kanda ya ziwa tunaomba uharaka wa kukamilisha kipande cha Kagoma-Kyamiyorwa na ile ya Geita-Usagara vipewe kipaumbele ili kurahisisha usafiri kati ya miji ya MWZ na BK kuliko kusafriri kwa kutegemea meli tu,inshallah walau sasa hivi kuna mabasi ya mwz-Buk kwa sababu 60%ni lami,walau.

    ReplyDelete
  11. barabara zetu,its good now
    ni mipango ya awamu ya 3 Nkapa

    ReplyDelete
  12. We michuzi niagent wa JK, na ndo maana kila safari yake ya matanuzi upo nyuma. Najua hutatoa msg hii lakini ujumbe utakufikia. Pumbafu!

    ReplyDelete
  13. SHUGHULIKIENI MAFISADI KWANZA NDIO TUTAWAPA SUPPORT. SIYO KUTAKA KUJISAFISHA KWA INFORMATION ZISIZOKUWA NA MSINGI.
    UNATAKA KUTUELEZA KUJENGA BARBARA. MASWALI YA KUTAFAKARI BILA KUANDIKA UJINGA. STANDARD GANI ZA BARABARA MNAJENGA? MOTORWAY AU ZILEZILE ZINAZOUWA WATU KILA SIKU? NANI AMELIPA HIZO PESA KAMA SIYO MISAADA YA KUOMBAOMBA? NA CAMPUNI ZA NJE AU ZA KITANZANIA NDIO ZINAJENGA HIZO BARABARA. UKIYAJIBU MASWALI HAYO UTAJIONA UMEONGEA PUMBA KWENYE BLOG HII. KWASABABU MAJIBU YOTE YATAONYESHA UDHAIFU WA UNGOZI WA NCHI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...