Ndugu Michuzi na wadau wote,
Siku moja, nilinunua umeme wa Tsh 10,000/= mara mbili ktk nyakati mbili tofauti (Na ambatanisha receipt hizo) moja ikionesha mahesabu yanayo endana na kutengeneza elfu kumi i.e. 8264.46+1735.54=10,000/= na receipt nyingine ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kununua umeme ikionesha mahesabu tofauti kabisa i.e. 5961.46+1251.91=7213.37/= ambapo ukiangalia kuna upungufu wa Tsh 2786.63/=

na ndio maana nika amua kununua umeme wa pili wa gharama hiyo hiyo kuthibitisha hayo mahesabu. Je hapa Tanesco wameniibia? na kama wameiba ni wateja wangapi wameibiwa? na Tanesco kujipatia utajiri mkubwa toka kwa raia masikini na wasio jiweza wanao tafuta ridhiki yao kwa shida kubwa?

kama mimi ni mteja mmoja je kuna wangapi walio ibiwa?

Ningependa kila raia kuwa makini na Receipt mnazo pewa baada ya kununua umeme kwa maana mnaweza kuibiwa kama mimi, Ningependa pia waungwa tulijadili hii issue na ata Tanesco nao waweze kutoa maelezo ya kiundani zaidi kuhusu hii issue maana najiona kama nimeibiwa.
Nashukuru.
Mdau Tabata

NB: Katika receipt zote mbili nimetoa meter no.
kwa maana sikupenda ziwe public.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. TANESCO ya Dar kumbe nao....
    Wilaya ya Mwanga hatuna LUKU yaani ndio wanatumaliza unakuta mtu umeamua kuacha kutumia kabisa umeme wao na kuwasha taa mbili tu usiku kwani bili wanaleta kubwa lakini mwezi unaofuata unaletewa bili karibu laki tatu ukienda kulalamika wanasema mita ndio imesomeka hivyo na computer zishatoa bili inabidi tu ulipe.Halafu walivyo mteja kwao ni MTUMWA badala ya MFALME. DUUUU mwaka huu kila mtu na EPA YAKE.

    ReplyDelete
  2. TANESCO OVYOO wanadhani bila wao hakuna umeme nchini wizi MTUPU hasa wale tulio na mita za kawaida ndio tunaibiwa haswaa..Tukiomba walete LUKU longolongo kibao jamani nchi hii kazi ipo..NINI KIFANYIKE KUDHIBITI TANESCO NA WIZI WAO?

    ReplyDelete
  3. Mimi sio Tanesco ila kutokana na kutumia LUKU kwa muda mrefu na kutoa malalamiko nikapewa mchanganuo.

    Kila mwezi unatakiwa kulipa kitu wanaita "SERVICE CHARGE" yaani hii ni charge ambayo ni fixed utumie umeme au usitumie na hii inaendana na aina ya Tarrif uliyojiandikisha, kama ni biashara, matumizi ya nyumbani au kiwandani.

    Cha pili ni malipo ya VAT 20% na hiyo ewura ni 1% ya hela ambayo iliyobakia baada ya Service charge kuondolewa.

    Kitu ambacho TANESCO wanakosea ni kwamba inatakiwa risiti iweke baya mchanganuo huo na inatakiwa akawaulize kulikoni?. Ila mimi nilikuwa napata mchanganuo kwenye risiti yangu.

    Ila kitu cha kupigia kelele hapo ni kwamba mzigo umekuwa mkubwa sana yaani EWURA hawakustahili kabisa kuingia hapo hata kigodo. Yaani sasa ni kama VAT ya umeme na nishati nyingine ni 21%. Huu ni ukamuaji ambao unatikiwa kupigiwa kelele.

    Kinachouma zaidi pesa hizi huenda zinaishia mikononi mwa wajanja badala ya kuboresha huduma na watu kuwa na uhakika wa umeme 365 days au 12months au 52 weeks au 8,760 hours of the year.

    ReplyDelete
  4. Tanesco fanyeni kazi yenu. sio na nyinyi mnatumiza. Sasa hii nchi itakua nchi ya aina gani kazi kumizana.hasa raia wasio na kitu yaani wasio na madaraka ya aina yoyote yale yanayousu ya umma,manake umekua umma wa kumizana,Mtu akipata ajila kwenye umma ANACHOWAZA ni kuwibia umma wa Tanzania, anadhani ndio utajili huo. sasa hii inakua too much jamani, Nchi inaendaje hii, kila mtu anawaza jinsi ya kuwibia umma.

    ReplyDelete
  5. Hapo umeshaingizwa mjini. Hizo Tshs 2786.63/ tayari huyo operator ameenda kujipongeza kwa bia jioni baada ya mzigo. Hivyo ndivyo dili zinavyoenda. Mjini hapa kwa hiyo usishangae sana...siku hizi wakwambia wenyewe kuwa 'kina mtu ana EPA yake' yaani unakula pale ulipo. Sasa sijui kama tutafika

    ReplyDelete
  6. dawa yao ni kununua system ya SOLAR POWER unaachana nao hao wapuuzi,kama mnaweza kulipa lakika tatu kila mwezi mnawezi afford nunua solar wala sio bei.Ndo nachotaka kukifanya mimi home.
    Mdau UK.

    ReplyDelete
  7. Labda sijaelewa, lakini sioni tatizo hapo. TANESCO wanauza umeme kwa unit na ukiangalia hapo ukifanya mahesabu inaonyesha unit 1 ni Tsh.129 kwa zote invoices. Total Paid siyo gharama ya umeme, hicho ni kiasi cha hela ulichompa muuzaji na kitu ambacho alitakiwa kufanya ni kukurudishia salio lako na kwa ujinga wako na wewe hukudai. Yaani wewe mchagga unaibiwa sasa watu wengine itakuwaje?

    ReplyDelete
  8. HAPO INAONYESHA: COST=5,961.46
    TAX= 1,251.91
    TOTAL PAID=10,0000.00

    KWA MAONI YANGU MDAU HUJAIBIWA NA HUYO CASHIER ALOUZA HIZO UNITS BALI CHECK NA MTU ULIOMTUMA KWANI TOFAUTI YAKE NI CHANGE ULOTAKIWA KURUDISHIWA NA HUYO CASHIER NA INAWEZEKANA MTU ULOMTUMA NDO ALIWEKA HIYO CHANGE MFUKONI OR OTHERWISE BASI HUYO CASHIER ANAFANYA WIZI WA KITOTO NA KWASABABU JINA LAKE LIPO HAPO WAZI BASI NENDA KWA WAKUU WAKE ILI AFUKUZWE KAZI MARA MOJA.INAWEZEKANA MACASHIER WA TANESCO WAKAWA WANAFANYA WIZI HUO WAKIJINGA NA WANACHUKUA HIYO TOFAUTI AU PUNJO HILO NA KUWEKA MIFUKONI.TANZANIA WIZI MTU KILA MTU MWIZI

    ReplyDelete
  9. Tafuta mwanasheria mzuri akusimamie muishtaki tanesco. Wakulipe kwa ajili ya usumbufu ulioupata ukizingatia watu wengi sana wanalizwa na tanesco.

    ReplyDelete
  10. PENGINE HIYO MACHINE HAINA AKILI, NAKUSHAURI NENDA KWA HUYO KARANI AKUPE MAELEZO YA KUTOSHA, PIA UNAONA HAPO KWENYE VAT PIA TUNAWAPA EWURA PESA ZA BURE ASILIMIA MOJA (1%) KWA NINI? KWANI SISI NDO TUMEIANZISHA HIYO EWURA, NI JUKUMU LA SERIKALI KUIPA RUZUKU SI SISI, EBU WANANCHI TUKATAE HII KITU, DUNIANI KOTE VYOMBO KAMA HIVYO VIPO LAKINI HAVICHUKUWI PESA TOKA KWA MLAJI, VAT INATOSHA NA TUNALIPA KODI, EBU ANGALIENI VIZURI HII KITU YA EWURA INANIUDHI SANA.

    ReplyDelete
  11. Mdau nashukuru kwa kulete hii kitu hewani, nakumbuka nilishawahi kutokewa na kitu kama hicho way back in 2007.Sikumbuki vyema kama ilikuwa exactly kama hivyo ama ala ila nakumbuka kwangu mimi ilikuwa ni umeme nilionunua ulikuwa mdogo kulinganisha na hela niliyotoa. Nilifuatilia hili suala kwa ukaribu na walinipa jibu kwamba huwa kuna gharama za huduma za kila mwezi. so katika manunuzi yako ya kwanza ya luku katika mwezi hayata kuwa sawa na kiasi cha umeme unachonunua kwani watakuwa wamekata automatically hiyo service charge yawezekana ndio maana ulivyonunua mara ya pili mambo yalikuwa Mswano.Sikukubaliana na utaratibu huo wa kukata moja moja katika manunuzi yao.. na niliondoka kwa mduhumu nikimuachia ushauri kuwa wateja wanahaki ya kuelemishwa na kufahamishwa mambo mbali mbali kama hayo sio mpaka mtu apate tatizo.

    ReplyDelete
  12. Kaka Michuzi;
    Hili suala nadhani lina ukweli mwingi.
    Kwani saa nyingine ni vigumu sana ku-justify makato. This time unanunua umeme kwa bei flani na ukijanunua tena next time, hata kama ni siku hiyo hiyo utaona tofauti. Unashindwa kuelewa!
    Naomba kama unaweza ututafutie uongozi wa TANESCO, hususan Dada Badra Masoud atueleze na ikithibitika waturudishie umeme "waliotuibia".

    Asante kwa ushirikiano

    ReplyDelete
  13. Hili tatizo ni lako binafsi usitegemee ummautaangalia risiti zako pindi unaponunua kitu.
    Kosa lako hukusoma risiti punde baada ya kuuziwa huo umeme.
    In short umesahau kuchukua pesa yako iliyobaki au
    kama ulimtuma mtu, basi amekuingiza 'king' amenunua umemewa kiasi kidogo.
    Hata hivyo kwa next 10,000/= -LIPA UMEME KADRI UNAVYOTUMIA' yaani LUKU inaweza ikakuuzia umeme katika rate tofauti ambayo ni ya juu kidogo. Hii ni kwa sababu unaponunua units nyingi zaidi basi gharama kwa unit huongezeka. Kwa maana kuna uwezekano kuwa unapotoa next 10,000 ukapata units chache kuliko the previous 10,000/=.

    lakini kwa issue yako hapo juu ni kwamba nenda kafuate albaki yako kwa vendor.

    ReplyDelete
  14. Utakacholipa ndicho kitakacho andikwa katika Invoice yako.Kwa hiyo siyo rahisi karani wa Tanesco pale dirishani kukuibia.Umetoa Elfu Kumi,Invoice inaonyesha umelipa Elfu Nane Mia Tano,basi bakio lako la Elfu Moja Mia Tano shurti karani akupe palepale.Kama hukupewa na wewe hukudai labda ulimwachia KeepChange,maana siku hizi hilo linaeleweka.Kama ni ujanja wa makarani kukuibia labda uje katika usomaji wa mita usio wa kweli.Kitu cha kulalamika hapa ni jinsi huduma muhimu kama umeme pale inapotozwa kodi ya VAT.Kama vile hiyo haitoshi utabandikiwa Kodi ya Ewura au Dawasa au Mamlaka za Maji katika miji mingine.Mambo ya ajabu kabisa.Naamini utakapo kwenda Ewura au Dawasa kulipa bili yako ya maji nako pia utatozwa Kodi yao kwenye Invoice yao.This is Triple Taxation.Nafikiri sasa wizara ya fedha na TRA wamepoteza kabisa Common Sense!Kodi siyo suala la kukusanya mapato tu ya serikali,bali ina makusudio yake kiuchumi!Kodi inayo vuruga jitihada za kuchochea ukuaji wa uchumi ni sumu katika nchi!Nobody cares but the Fat Belly!

    ReplyDelete
  15. Katika Tanzania hii nimjifunza kitu kimoja, kuwa huduma ikiwa inatolewa na mtu mmoja, nina maana kampuni moja tu(monopoly) basi huduma huwa mbovu na dhuluma nyingi kama rushwa huwepo.
    Kampuni yetu ya Tanesco ni moja ya huduma ambayo ni pekee, ingawaje kumeanza kutokea huduma mbadala, lakini asilimia kubwa tunaitegemea TANESCO. Angalia TTCLwalivyoboresha huduma zao, kwasabau wana mshindani.
    Kwanza kuipata huduma yenyewe ni mpaka upitie mlango wa uani, jaribu kuulizia wengi walioipata huduma hii watakupa taarifa za usumbufu fulani.
    Sasa umeshaipata huduma yenyewe, nilifikiri ili Tanesco waongeze kipato wangejaribu kuiboresha na kuhakikisha wateja wao wanaipata huduma hii bila kukosa. Kwasababu wakiuza ndipo mapato yao yanaongezeka, lakini cha ajabu upatikanaji wa umeme wenyewe shida, unaweza ukaupata leo kesho hakuna, na wanakata wakati wowote. Kwanini wasiwe wanatoa taarifa kabla.
    Kuhusu LUKU, najua kuna viwango vya kulipa, mfano ukizidi kiasi fulani, gharama yake inakuwa kubwa zaidi, mfano mtu anayetumia chini ya uniti 50, si sawa na yule anayetumia juu ya unit 50, kwa mwezi. Sasa hili wangeliweka wazi.
    Na kwa mfano wa mlengwa hapo juu, alitakiwa adai chenji yake,na hii inaonyesha uaminifu wa wahudmu wenu ulivyo.
    m3

    ReplyDelete
  16. fungua kampuni nyingi za umeme kama simu vile uone good service hio ndo dawa yake tu tanesco wizi wizi tuuu wanaishi kwa milungula kila kona bila rushwa hupati chochote pale

    ReplyDelete
  17. Habari zenu Wadau, Mimi nilitaka umeme wa elfu kumi na SIKUPEWA chenji kwa maana mahitaji yangu ni ya umeme wa elfu kumi na nilipewa umeme kama unavyo onekana, Nikabisha na nikasema basi naomba umeme mwingine wa elfu kumi na ndio nikapewa receipt nyingine ambayo inaelezea vyema mchanganuo wa elfu kumi basi nikadhibitisha ya kwamba niliibiwa ktk receipt ya kwanza.

    Swali la muhimu, Je kwanini receipt zote hazifanani? kwa maana mahesabu yanayo onekana ni madogo sana na yanajieleza yenyewe.

    Na kama ni services charges basi zingeoneshwa, sasa kwa asilimia 100 SIO services charges, ata ktk receipt zote haikuoneshwa hivyo. Na siku zote services charges uandikwa kwa maandishi.

    Ni Mungu tu aliniambia niangalie receipt hiyo, Na kama nisinge nunua umeme wa pili then nisinge weza kudhibitisha huu ujanja na wizi, Nauita Ujanja au wizi mpaka pale Tanesco watakapo toa kauli yao.

    Akhasante.

    ReplyDelete
  18. KARIBU KILA KONA NI USANII UNAFANYIKA..NATOKA KIDOGO NJE YA MADA..NILITUMA TANZANIA MIZIGO IKIWAMO LAPTOP,IPOD,TV MONITOR FLAT SCREEN ETC...NILITUMA DHL CHA KUSHANGAZA NILIPASWA KULIPA 72,000TSH,KWA KUWA BWANA MDOGO YUPO MKOA JIRANI AKAPIGIWA SIMU KUWA MZIGO UMEZUILIWA AIRPORT ANATAKIWA KULIPA SH LAKI 1 ZAIDI,AKAFANYA UCHUNGUZI AKAGUNDUA KUWA KUNA BINTI DHL AIRPORT DSM NDIO MCHEZO WAKE ,ALIPOWASILIANA NA MAKAO MAKUU YA DHL HAPO DSM..AKAAMBIWA MZIGO UPO HAPO OFISINI NA HAKUNA HELA YA ZIADA ANAYOPASWA KULIPA ZAIDI YA SH 72ALFU ALIYOLIPA...KITENDO HICHO KIMECHELEWESHA KU-DELIVER MZIGO KWA WIKI 3 BADALA YA SIKU4,NA IMENIINGIZIA HASARA..WADAU KUWENI MAKINI KWA HILO PIA,TAMAA YA HUYO BINTI JE?AMESHAJIKUSANYIA KIASI GANI?KWA WENGINE...KUWENI MACHO NA HASA WENZANGU AMBAO MPO NJE YA BONGO NA HUWA MNA DESTURI YA KUTUMA VITU NYUMBANI KUPITIA DHL...

    ReplyDelete
  19. JE, KUNA MDAU YEYOTE ANAEJUA SERVICE CHARGE INA GHARIMU KIASI GANI KWA MADARAJA TOFAUTI?I.E DMESTIC, BUSINESS.......NA KAMA HIYO Tshs 2786.63/- HAITAOANA NA HIZO CHARGES THEN TUNAWEZA TUKASEMA KUNA USANII HAPO. KAMA SIJAKOSEA SANA KUNA KITUO FULANI,MIAKA YA NYUMA MNOO KAMA ZAIDI YA MIAKA 5 KILIKUWGA KINAFANYA MCHEZO WA KUPIGA PANGA HELA ZA WATEJA NA WAUZAJI KWAKWELI WALINEEMEKA MNOOO KWA SABABU NAWAJUA.NADHANI KITUO KILIFUNGWA,MAENEO YA SINZA-SHEKILANGO,MAY BE, NA BAADAE WAO KUFUKUZWA BAADA YA WAO KUWA WANATAMBA JINSI WANAVYOFANYA HADHARANI. MHH MJINI SHULE.!

    ReplyDelete
  20. Wewe mdau kama umeibiwa kwani hujakwenda polisi unasubiri Tanesco watoe kauli? Hii siyo siasa mkubwa, nenda panapostahili badala ya kulalamika humu kwenye blog na kutaka kauli za kisiasa.

    Usinikumbushe yule jamaa aliyekuwa anasosomekwa yeye ametulia tu anagojea jamaa amalize ili apate ushahidi

    ReplyDelete
  21. Mdau wa DHL hapo nakuunga mkono mimi niliagiza gari Japan, kilichofanyika ni kwamba jamaa hawakufunga CD radio kwa kuwa zinaibiwa wakanitumia kwa DHL thamani yake ni $100. ambayo ni part ya gari niliyoagiza. Jamaa wa DHL wakaniletea tax assessment ya Ths 76,000 na hapo hapo nikalipa tena kodi ya kuingiza gari, yaani usanii ni kila mahali. Watu wanaona mtu ukiagiza kitu ni kama vile utafaidi wanaamua kukukomesha ushindwe lipia ili wote mkose.

    ReplyDelete
  22. Vile vile, dalili nyingine ya wizi au tax evasion inajitokeza kulingana na hiyo karatasi kuandikwa TAX INVOICE badala ya CASH RECEIPT au SALES RECEIPT.

    Maana yake ni kwamba hata wakija kubanwa baadaye watasema hiyo ilikuwa Invoice, na Invoice siyo ushahidi wa manunuzi au malipo.

    ReplyDelete
  23. Huo sasa ndiyo tunaouita upunguani, umeshaambiwa kuwa TANESCO inuza umeme kwa units wewe unaomba umeme wa $10,000 hata mimi nitakuliza. Ukienda kununua umeme sema naomba units 50 na muuzaji atakuambia ni kiasi gani. Hiyo ni sawa sawa na kwenda baa na kuomba bia ya 5000 huyo muuza baa si atakuona wewe wakuja na atakuliza. Bia zinauzwa kwa chupa, chupa ndiyo unit. Hizo lisiti hazina makosa labda niseme zina upungufu labda wangeongeza sehemu ambayo inaonyesha change yako ni kiasi gani ili watu kama wewe muweze kudai hapo hapo na pia jina la muuzaji.

    ReplyDelete
  24. yan msiseme huo wizi apo tanesco na maji,,,ivi kwanini hamfafanui kimaandishi ktk invoice izo gharama za makato mengine?shenzi sana na wizi mkubwa yan nakereka adi ntatoa mtu jicho siku,,,
    kila mahali wiiiiizi khaa
    why tulipe EWURA?jamaniiii sijui dawasco na uchafu mwingine,,,afu izo kodi wala hatuoni zimesaidia nini nchi hii adi sasa
    hatuna viongozi wee fikiria mtu toka secondary aliiba mtihani,chuo alidesa,kazi ya awali aliforge documents,sasa mwategemeani awe waziri,director etc km sii wizi tu kwa kwenda mbele??yan wao ili haliwaumi ata kidogo

    ReplyDelete
  25. Kwa kweli kama kuna sehemu inatia kichefuchefu ni huduma za TANESCO. Tunaomba serikali iliangalie hili kampuni kwa macho mawili. Msione wananchi wamenyamza kimya mkafikiri wajinga.
    Boresheni huduma zenu. Mfano eneo la Moshi Bar, Kipunguni kuna line kila siku wanakata umeme. Inabidi kila siku watu waende kuomba, sijui kuna nini wanakitaka. Je kuna mgao? Je kuna nini tumewakosea, tuelezeni jamani ni kero isiyopendeza, na baya zaidi wanakati muda wa usiku, kuanzia saa moja...
    Hayo ya LUKU ndio kama walivyoeleza wenzangu. Wekeni kila kitu wazi, makato kiasi unachodaiwa nk. Pia chunguzeni vijana wenu mnaowaajiri, wengine hawana uaminifu.
    Kama kungekuwa na Tanesco mbadala tungewakimbia, lakini ombeni mungu Ujamaa bado unaendelea Tanzania

    ReplyDelete
  26. Jamani, wajasiriamali (na mabepari) wanahitajika kuwekeza kwenye sekta ya nishati Tanzania. Tunateseka sana na umonopoly huu wa TANESCO. Tunaumia na uchumi unazidi kwenda mrama kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu, achilia mbali sababu nyingine zinazofanya maisha kuwa "mbofumbofu" kutokana na matatizo ya TANESCO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...