Mabibi Na Mabwana,
Kwa niaba ya familia ya marehemu Mzee Leonard Merere napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kuwa kutakuwa na Misa na kuaga mwili wa mzee wetu siku ya jumamosi 02/21/09 saa 11 asubuhi, naambatanisha anuani ya sehemu ambayo misa itafayika hapo chini.
Tafadhalini mabibi na Mabwana tunaombwa kuzingatia muda na kufika kwa wakati ili kufanikisha shughuli ya kumuaga mzee pindi tupatapo ujumbe huu basi tuwataarifu wale wote watakaopenda kuhudhuria shughuli hii muhimu.
Jacob ,Naomi & Anna Merere wameniomba nisisahau kuwashukuru watu wote kwa ukarimu wao wa kuchangia kwa hali na mali kuhakikisha uwezekano wa kuupeleka mwili wa marehemu baba yao nyumbani Tanzania kwa mazishi.
HOSANA GOSPER CENTER,
120 Stafford st Worcester, MA
Contacts:Jacob & Anna Merere (978)-726-2227/(978)-957-2153
Naomi Merere (978)-413-3722/978)-632-9823
Juma Malika (781)-244-7353
Simon Twalipo (978)-423-1192
Pastor Abisalom Nasua (214)-554-7381
Jacob na familia yote ya Merere, nawaombea mungu awabariki katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteJamani natamani kuhudhuria hiyo misa ya kumuaga mzee mwenzangu lakini huo muda wa saa 11 asubuhi(hiyo ni alfajiri) sitaweza na uzee nilionao. Kama kutakuwa na mabadiliko ya muda msisite kunijulisha. Naweza kuhudhuria wakati wowote kuanzia saa 2 asubuhi.
ReplyDeletePoleni sana Jacob na Naomi,Mungu awatie nguvu katika kipindi kigumu cha kumsindikiza Baba,Mungu ni Mwaminifu na roho mtakatifu awape faraja ya pekee.
ReplyDelete