Msanii AY ametoa wimbo mpya ambao tayari umeshaingia kwenye vituo mbalimbali vya radio na mtandaoni kama tovuti ya BongoCelebrity. Wimbo unaitwa 'Leo' na umetengenezwa katika studio za Hermy B. Video ya wimbo huu inatarajiwa kuanza kutengenezwa wikiendi hii chini ya kampuni kutoka nchi jirani ya Kenya inayojulikana kama Ogopa Video. Jumatano hii anatarajiwa kukwaa pipa kuelekea Marekani akiwa na meneja wake John Mahundi kwa ajili ya shoo kadhaa katika miji mbalimbali. Ratiba ya ziara hiyo itawekwa hapa muda si mrefu ujao
Usikilize wimbo huo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AY ninakubali kazi zako,lakini nimesikiliza wimbo wako mpya ktk BC,sijapenda,kama utakua unafanya hivyo utaharibu usanii wako,endelea jinsi ulivyokua,kama utataka kutegemea computer,watu tutakushusha sasa hivi.

    ReplyDelete
  2. Na huyu anakimbia vumbi kwa ngazi ya ziara ya kimuziki kama Ali kiba? Tuliwaambia bora kupiga box kuliko kula vumbi mkabisha,Ona sasa vistaa vyenu vinatoka nduki.hahahahahahaha

    ReplyDelete
  3. AY uko tight mazee,

    Nashindwa kuwaelewa wadau waliontangulia hapo juu tusioshe vinywa tu, tuangalie trend ya mziki inaendaje na ndio tujadili. Ukicheck wana hiphop wengi wameingia kwenye computer production, cranks na kuimba kidogo. Na hayo ndio mahitaji ya soko la mziki kwa sasa, ni watu wachache sana wanataka hardcore hiphop.

    Nimeukubali huu wimbo na AY uko juu mazee you are among the best in tz including Lady Jd, FA, Prof,etc

    Keep it up bro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...