Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Afrika ya Mashariki, Mh. Juma Mwapachu akiongoza mjadala wa Uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki,uliomalizika leo hapa London Uingereza. Kulia ni Bwana David Flit, Mwenyekiti wa Mkutano huo kwa sehemu ya kwanza.
Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mheshimiwa, Mwanaidi Senare Maajar, akitoa maelezo na msimamo wa Serikali ya Tanzania na Jumuiya kwa ujumla kuhusu Sera na Mikakati ya Serikali za Nchi za Afrika Mashariki katika kuwekeza.

Bwana Paul Kukubo kutoka Kenya ICT Board, akichangia maada kuhusu uwekezaji katika mfumo wa Benki na Teknologia ya habari na mawasiliano.
Mh. Enos Bukuku, Naibu Gavana wa BOT, akichangia mada katika Mkutano wa Uwekezaji wa nchi za Afrika ya Mashariki jijii London

Picha ya pamoja ya washiriki. Toka shoto Balozi wa Kenya Nchini Uingereza, Mh. Joseph Muchemi, Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mh. Mwanaidi Sinare Maajar, Waziri wa Biashara wa Kenya, Mh.Amos Kimunya, Dr. Cyrus Njiru Katibu wa Kudumu katika Ofisi ya Makamu wa Rais naWizara ya Biashara Nchini Kenya, Mh. Hafsa Mossi-Waziri wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wa Burundi.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Naibu Ganava: Enos(Sio Amos) Bukuku

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, kwa nyuma ya balozi majaar namwona mtu kama MASHAKA WA UK (aka Dr Shayo). Kapendeza kweli mwaya na suti yake. Halafu alikuwa kama anasubiri picha kwa jinsi alivyotoa macho. Kumbe naye ni mwekezaji? Hongera kaka mashaka wa UK. Nawakilisha, mdau Kesy wa Japan.

    ReplyDelete
  3. Ni kweli hata mimi nimemchabu Mashaka wa UK na miwani yake. Sikujua kuwa Shayo ndo mashaka wa UK. All in all huwa anajitahidi kutoa maoni yake na jamii kama jamii ili ikamilike inahitaji watu kama hao. Hongera Shayo na endeleza lebeneke la Uma-Shaka ukiwakilisha UK as a whole. Big up Mashaka wetu.

    Victorine, W.

    ReplyDelete
  4. Jamani!Shayo tangu lini amekuwa mwekezaji? Halafu kumbe ndo mashaka wa UK? Kwani Mashaka ndo nani? Tufahamishane basi jamani.

    ReplyDelete
  5. Du wadau hamuachi kumsaka mtu? huyu kajamaa tangu ameanzisha hako kajikonsultancy kake cha ushauri wa biashara na uwekezaji huko UK, ameshashauri makampuni mengi tu ya kutoka UK/EU ambayo yamewekeza Tanzania. Hapa nitakupeni mfano wa kuonyesha haka kajamaa hakana makuu

    Kule Mbeya... tukuyu kamleta muwekezaji amewekeza milion £3 kama kianzio. Matazamio ni kuwekeza £15million in the next 7 years Iringa million £5, lengo ni£ 10million nk.nk

    Jamani tuache kufuatilia hawa jamaa, Wanasonga mbele wengi wetu ni majungu tu na kujadili vitu visivyokuwa na manufaa kwa taifa la tanzania.

    Hapo siyo kuwa amekaa mkao wa kusubiri picha, alikuwa akimuangalia waziri mmoja wa kutoka Rwanda ambaye balozi wenu UK alikuwa anasistiza jambo.

    Dr. Shayo usitishwe na hivi vijikoment kumbuka "kelele za chura hazimnyimi tembo kunjwa maji"

    Endelea kutuletea wawekezaji ili watoto wetu wapate ajira mwaya

    ReplyDelete
  6. Mbona hii mikutano ya uwekezaji ni sisi wenyewe wa nyumbani tu! Kwanini tusingefanyia nyumbani tu?

    ReplyDelete
  7. Huu ni Mkutano wa "Kuvutia Wawekezaji toka Uingereza kuja kuwekeza Afrika Mashariki?" au ni Mkutano wa "Kujiuza au Kuuza Sera za Uwekezaji katika nchi zetu za Afrika ya Mashariki kwa Wawekezaji toka Uingereza?".Kuna tofauti kubwa sana kati ya mambo haya mawili.Let me start here:Do Potential Investors need to be told where to invest,in this case East Africa?What makes a British Investor invest in any particular African country?Is Tanzania really competitive comparatively across the spectrum of african countries?Tumejiuliza,kwanini Kenya imetuzidi sana katika Viwanda?Kwanini Uganda,ambayo uchumi wake uliharibiwa sana na utawala wa Idd Amin,lakini walikusanya nguvu na kuanza tena kwa kasi na hivi sasa wametupita katika viwanda pia?Tumejiuliza,kwanini wawekezaji toka nje na hususan toka huko Uingereza wako tayari zaidi kuwekeza Kenya au Uganda lakini sio Tanzania LAKINI watafanya hivyo matarajio yao makubwa yakiwa SOKO LA TANZANIA? For how long are we going to remain Fools in this respect? Why should we deserve all this? And Who is our real Enemy? Sawa,Watanzania wamekwenda Uingereza na wamehudhuria Mkutano huo wa Uwekezaji,Lakini mwisho wa siku tujiulize,hawa ndugu zetu ni "Kweli Walijizatiti kwa Kazi hiyo Pevu?" ya kuwarubuni na kuwashawishi WAWEKEZAJI WA UINGEREZA waamini kwamba sasa watanzania tumebadilika na tunazungumza lugha moja ya uwekezaji na wao Waingereza? Kitakacho wavutia wawekezaji "siyo malikauli au maneno matamu ya ulaghai" bali sera na sheria za uwekezaji zitakazo linda Mtaji na kumhakikishia mwekezaji "mtiririko wa faida"kwa kipindi cha kutosha kuweza kurejesha mikopo ya mabenki na kodi za nchi zote mbili,Tanzania na Uingereza!Tutabakia Kuhubiri sana kuhusu Uwekezaji hapa nchini.Lakini mwisho wa siku tutaishia kuwapigia debe wenzetu wa nchi zingine za Afrika ya Mashariki ambako ni wepesi kusikiliza na kutenda!Kwenye masuala ya Uchumi,siasa haioni ndani!Porojo na Usanii wa Kisiasa huwekwa pembeni.Kwa taarifa yenu,"Waingereza wanatufahamu sisi watanzania na wana wa afrika ya mashariki,ZAIDI KULIKO, VILE TUNAVYO JIFAHAMU SISI WENYEWE!Have we really changed? Mbona Bandari zetu na Reli zetu zinatushitaki kwa wawekezaji?Mbona umeme wa Tanesco na Vyanzo vingine vya Nishati vinatushitaki kwa wawekezaji?Mbona Mishahara Duni na mapato dhaifu ya wafanyakazi wetu yanatushitaki kwa wawekezaji?Mbona ukosefu wa wafanyakazi wenye Stadi za Uzalishaji Viwandani unatushitaki kwa wawekezaji?Nchi Tajiri duniani hivi sasa zimekuwa zikizungumzia kuhusu "Global Fallen Demand" ambayo dawa yake ni "Economic Stimulus" to boost government spending,inorder to revive ailing industries,in order to reduce unemployment,inorder to increase individual spending,inorder to boost industrial production!No Spending,No More Production!The Government should stimulate private expenditure if industries have to receive a Boost so that the economy may prosper!Watanzania mwelekeo na msimamo wetu uko wapi?Tutaendelea kuwapigia debe wenzetu au tupo tayari kujipigia debe sisi wenyewe?TUBADILIKE KWA VITENDO BASI.-----papperazzi antonnio---

    ReplyDelete
  8. Mkuu wa Wilaya ya nanii, hao wadau waache zao za kumpakazia huyo mshkaji Shayo. Itakuwaje wamfananishe na Mashaka? Acheni hizo wadau. Sio fresh.

    ReplyDelete
  9. Mkuu wa Wilaya ya nanihii, hivi Amos Kimunya bado ni waziri au hizo picha ni za zamani kidogo.

    ReplyDelete
  10. poa,,,
    uyo balozi wa Tz UK kahamia na mumewe uko??

    ni swali tu

    ReplyDelete
  11. Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya naniihi! Tafadhali wafahamishe waduu ya kuwa akina Mashaka kama kina Shayo wanahitajika katika hii dunia. Otherwise wote tukiwa na busara zako nani atatumbuiza? Ati kamleta mwekezaji Iringa? Yeye mwenyewe kachoka! Huyu daktari sijui wa wapi? Ni daktari wa uchumi kweli huyu? hahaaa JK kuwa macho na hawa watu wanaojiita wanauchumi, isijekuwa ni kama yule daktari wa Iringa. Anyway, anafurahisha blog yetu hii ya jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...