zogo limeumuka miongoni mwa wapenzi wa muziki kufuatia kuhama ghafla kwa Hassan, mtoto wa marehemu TX Moshi William, kutoka Msondo kwenda FM Academia hivi karibuni, ambapo kuna uoande unadai hiyo ni hatua nzuri kwake kwani ataendelea kimuziki katika mtizamo wa kisasa, na wengine wanadai ameharibu kwani Msondo licha ya kumuenzi baba yake pia ni bendi inayojua kulea wanamuziki kwa muda mrefu na sio kuwa wanamuziki wenye utamu wa Big G.
wadau mnakaribishwa kuchangia mada hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. men... who cares?!! let the guy figure out life for himself... he's no longer a kid.

    ReplyDelete
  2. nafikiri amechemsha,nimeshuhudia pale msondo,na nawafahamu kiasi hao fm. kwa hulka za watanzania ,najua hawapendi fujo.kwa hao wakongo mani ,najua hatakaa sana,ukichukulia kuwa huyo dogo sio mtu wa kujisikia sana.
    pia ni pigo kwa msondo,na ajiandae kuchukiwa,kwani najua wanazi wa msondo na miondoko yao walivyo.
    inawezekana pia ikawa ndo mwelekeo wa kufa msondo ngoma.

    ReplyDelete
  3. au safari ya kuja ughaibuni imemchanganya?maana msondo Mh...WAPOWAPO TU!

    ReplyDelete
  4. Abaki Msondo ndio bendi inayompendeza kuliko huko alikukwenda. Maana sauti yake inafanana na ya marehemu baba yake kwahiyo nyimbo nyingi anaziweza labda kama wamemfukuza.

    Nemganga

    ReplyDelete
  5. Maamuzi yake yaheshimiwe, amekuwepo msondo kwa hiyo anajua faida na hasara zake. Kwa viongozi wa msondo wala wasihangaike naye kwa maoni yangu ni kijana anayechipukia ila alikuwa ha "fit" ktk kundi hilo kwa aina ya muziki wanayopiga. Anafaa zaidi muziki wa kizazi kipya!!

    ReplyDelete
  6. Kaka Michu haya yote unapiga chenga tuu lakini mie ninakufahamu weye Abou wa Liongo MSONDO Damu sasa hapa unataka watu wakusindikize.... Pole Kaka mwachieni naye akahangaike!!! Mbona akina Papa Wemba walikacha bendi zao za zamani na kuwa na nyingine na bado wapo gado mpaka sasa.. (dRU)

    ReplyDelete
  7. Hajui atendalo, hajawahi kuwa mwanamuziki alilelewa na msondo kwa heshima ya babake, huko alikokwenda ndo kutamfundisha nafasi yake ni ipi katika muziki,mark my words

    ReplyDelete
  8. Msondo ngoma, Baba ya muziki, wazee wa Amana.

    Walikuwepo, bado wapo na wataendelea kuwepo.

    Wengi walikuja, na wakaondoka, lakini Msondo ndiyo imezidi kuwa imara.

    Kadri mwanamuziki mmoja anapotoka ndiyo baba ya muziki inafurahi kwani inakaribia kupata mtoto mwingine.

    Msondo ni chuo cha mafunzo, alpha na Omega.

    Msondo baba ya muziki, Msondo siku zote!

    Burudikeni na "Mtanikumbuka" utunzi wake hayati Moshi TX
    http://www.youtube.com/watch?v=9ebmlAVtHUg

    ReplyDelete
  9. MAISHA NI KUJARIBU BILA RISK HUWEZI KUJUA DREAMS ZAKO BWANA MIMI NAVYOONA KAMA MSONDO WANAMUHESHIMU SANA NA WANAMUENZI MZEE MZIMA MAREHEMU TX,WAMWACHE AKIENDA AKISHINDWA AKIRUDI WAMPOKEE KWA MIKONO MIWILI.......SABABU KUU NAYOONA MIMI MPAKA SASA BABA YAKE ALIFIKIA STAGE YA JUU SANA SANA NA MSONDO ALIYOTOKA NAYO ENZI HIZOO, HUYU KIJANA HAWEZI KUFIKIA HATA ROBO YA BABA YAKE NA NADHANI YEYE AMESHALIONA HILO NDIO MAANA ANAJARIBU KUONA ATOKE VIPI, NYINYI MSONDO NI WANAMUZIKI WAZURI SANA MIMI HAPO TZ HAMNA BENDI NINAYOIPENDA KAMA MSONDO PAMOJA NA KUPOTEZA WANAMUZIKI KAMA MBWEMBWE TX NA WENGINEO WENGI ROHO ILINIUMA SANA LAKINI BADO NASEMA KIJANA MWACHENI ATAFUTE JAMANI,LAKINI AKIRUDI KWA BABA MPOKEENI,HATA NYINYI MIAKA YA SABINI KUNA WALIONDOKA WAKARUDI SASA MIAKA YAKE YA SABINI KIJANA HUYU NDO SASA

    ReplyDelete
  10. Nakuunga mkono Anonymous April 03, 2009 1:46 AM
    Hakuna haja ya kumng'ang'ania kijana achiwe aendelee kujifunza muziki, wakati wa kurudi ukifika atarudi tu kwani msondo ndiyo baba yao.
    Sisi msondo tulikwisha pata mapigo mengi tu ya kuonndokewa na vipenzi vyetu, tena katika wakati ambao tunawahitaji sana, lakini hatuwezi hata siku moja kupingana na mipango ya mungu juu ya bendi yetu tunayoipenda sana.
    Tuliondokewa na Suleiman Mbwembwe, Athumani Momba, TX Moshi na hivi karibuni kiraka chetu Joseph Maina. Hao wote waliitwa kwa muumba wakati mashabiki tunawapenda sana lakini Mwenyezi Mungu aliwapenda zaidi. Tusife moyo wapenzi wa msondo kama tuumeweza kuondokewa na 'cream' nne kwa kipindi kifupi, tusiingiwe na simanzi kwa kijana kuondoka. Tumuombee mafanikio na afya njema, kwani moyoni mwake Hassan ni 'msondo damu'.

    Die-hard Msondo Fan.

    ReplyDelete
  11. Mshikaji wa 6:52 ulichoongea ndicho. The kid si mwanamuziki, wazee wamemtunzia heshima baba yake tu. Kuimba kwenyewe bado sana. Huko FM ndo atakumbana na wakongomani wanaojua ubaguzi na fitna za muziki. Mpe miezi kadhaa tu atanawa mikono. Bongo fleva ndiyo kimbilio pekee kwake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...