Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michuzi, kuna ile website ya links zilizokatika kila mara leo wameweka link eti mechi za yanga ni bure. ukweli uko wapi?

    ReplyDelete
  2. Hii ndiyo mijitu ya kuchapa viboko, hata haya halina....Kitendo tu cha kujisaidia hadharani ni cha aibu, sio kwa kuwa mgongo tu ndio uliokuwa - exposed basi hamna neno.....

    ReplyDelete
  3. Hii Taswira ni kama Mahakama Kisutu au nimekosea Mh. Balozi wa nanihii. lakini Jamaa alizidiwa na hali ya hela yenyewe mvua ndio kama vile tena japo anachafua mazingira

    ReplyDelete
  4. Naomba Halmashauri ya jiji la Dar waje Jiji la wajanja Mo-town au Moshi waone jinsi tulivyo serious na utunzaji wa mazingira. Hakuna kojoa kojoa ovyo wala kutupa taka.

    Ila naomba wawe makini, KABLA YA KUANZA KAMPENI YA KUZUIA KOJOA KOJOA OVYO NA KUTUPA TAKA, DUST BIN NA VYOO VIJENGWE KWA WINGI.

    ReplyDelete
  5. hivi mikoa migine haina sheria kama za mkoa wa kilimanjaro!!mkoa wa kilimanjaro kuna gambo kila mahala..na ukikamatwa unakojoa hovyo unalipa faini hapo hapo au jela..

    ReplyDelete
  6. He may have used the gutter behind him instead...

    ReplyDelete
  7. seriously tunahitaji kuadress hii ishu . Mimi sioni taabu mtu anapomwagia bustani na kojo lake taabu yangu ni kuwa hakuna hata vyoo vya kulipia katika mitaa ya uswazi na hata kwa matajiri nambie utaona vyoo wapi? Mnazi mmoja vipo vingapi? Kariakoo vipo vingapi? Posta vipo vinmgapi? Yaani p;osta ndio mchosho kabisa ukiw aposta mpya na kojo limekushika laizma upige mbio mpaka posta ya zamani upande wa baharini kupata vyoo. kama una hara jasho litakutoka.hawa site hovyopoo kama wapsiopojengwa vyoo kw astaili ya jiji basi tutakuwa tunamwaga kojo katika miti ili iendelee kumea vyema

    ReplyDelete
  8. Kama hakuna vyoo vya umma unategemea mtu akibanwa atafanyaje? Inabidi kuwe na vyoo kila mahali penye watu wengi hasa vituo vya mabasi.

    ReplyDelete
  9. HUYU AMEAJIRIWA KUSHIKA UKUNI WA TANGAZO HILO SASA ANAONA AIBU NDIO SABABU ANAFICHA KICHWA CHAKE KAMA JOGOO, SALALEEEEeeeeeee! Bongo kila kitu kinawezekana ila usiuze bigi jii hadharani askari wa jiji watakukamata kwa kuchafua mazingira!

    ReplyDelete
  10. Hivi kumbe excuse ya vyoo vya jiji kutokuonekana ni kujisaidia barabarani! Aluta continua, ukibanwa kati ya mji hangaika na mitaro tu....

    ReplyDelete
  11. Si mlaumu sana mtu huyu, kwa kuwa vyoo havipo kila mahali, na magonjwa ni mengi inawezekana ana kisukali ama presha na kajinywea vidonge vyake vya lasix unategemea nini? ajikojolee? inatakiwa kuwa na vyoo kila mahari ili kukomesha jambo hili vinginevyo hakuna kulaumiana sana.

    ReplyDelete
  12. MNACHONGA SANA
    BABAKE MTU HUYO
    MTOTO WAKE KIGOGO NA CELEBRITY BONGO
    SHAURI YENU
    Kidding! Lol

    ReplyDelete
  13. Ndugu zangu kwa wale mlio bahatika
    kusafiri kwenda nchi kama Marekani na baadhi ya nchi za ulaya mnajua jinsi kila barabara kubwa(Highway)zilivyo na kituo cha mapumziko(Rest Room)ambapo huwa madreva na wasafiri hupumzika na kujisaidia haja ndogo ama kubwa na ikibidi kujipatia kinywaji na vitafunio huduma hiyo huwa ni bure matunda ya kodi yao na eneo ni safi masaa 24.Haja ndogo ama kubwa ukiwa mjini mara nyingi vituo vya mafuta(Gas station au Petrol Station)kama tulivyozoea kuziita huko nyumbani hutoa huduma hiyo bure Je Huduma hizo nyumbani tunazo?,kama hatunazo wananchi watembee na vyoo au tutengeneze vyoo portable kwa dharura kama hizi?,mimi nina
    imani mtu kufikia hatua hiyo lazima ipo sababu sasa tushimshambulie huyo jamaa na wengineo tushambulie chanzo cha tatizo.Tatizo ni kwamba hakuna huduma na swala la haja ndogo au kubwa mida mingine halikupi taarifa(tumbo la kuhara utajizuia?.Tujenge ustaraabu wa kutatua matatizo haya mengine hata hayahitaji mabilioni kama ya EPA kinachohitajika ni Akili na ubunifu.

    ReplyDelete
  14. hatuhitaji hata kulipa kodi tanzania. watu kama hawa ndio wakulipishwa fine mpaka wakome. Hamna kuchapa kiboko hapa walivyo wengi kama hawa wakitozwa fine kwa week tu hela zao zinaweza kusafisha jiji la dar lote

    ReplyDelete
  15. kweli kabisa anony wa 7:54, hakuna vyoo na umezidiwa hakuna jinsi. Kwa wenztu umebanwa haja kubwa ndogo unaingia popote pale bila kuulizwa sana sana wewe ndio utauliza choo chao kilipo. huku kwetu ni kinyume kabisa. Hata ukingia mgahawani kula ukitaka kujisaidia lazima uombe ufunguo kwa cashier. Kwa mtaji huo lazima watu wakojoe popote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...