Salam Kaka Michuzi,
Pamoja na mvua zote za juzi , daraja letu la Vingunguti liko shwari na watu walikuwa wanakatiza kama kawaida,hakuna adha ya maji kujaa kama ilivyokuwa mwanzo.


Tunashukuru sana Serikali kwa kuliona hilo na kujenga daraja, ila tatizo liko kwenye barabara kipande cha Baracuda ndio kuna mashimo ajabu ,na maji yamejaa sana, sasa inabidi tupige short cut ya G.B.F GARDEN ambapo njia ni nyembamba Mno na kupishana inakuwa tabu.

Samahani Picha imechululiwa asubuhi hii wakati wa kijua kikali .Ila kwa Barabara za Vichochoroni kama alivyosema Mdau chini pale kwa Upande wa Tabata ndio nimeona Kokoto Jana Tabata Muslim karibu na Ofisi za CCM na Soko kubwa na MSikiti ndio zimemwagwa pal, natumaini hawatozirundika tu watazishughulikia chap chap.

Kwa Upande mwingine Soko la Tabata Muslim ni kubwa ila Wafanyabiashara wamelikimbia?? Serikali za Mitaa ziko wapi? Mzee Msamvu Vipi ?

Mdau Flo%

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ebwana MIPUSU hapo kidogo mbna sijapafahamu vizuri ni pale vingunguti machinjiyono au wapi? mbna pale tabata muslimu (al farouq seminary, shule ya mwl.HASHIM SAIBOKO) hakuna daraja kuna uhusiano gani na hizo kokoto?

    ReplyDelete
  2. Ebwana MIPUSU hapo kidogo mbna sijapafahamu vizuri ni pale vingunguti machinjiyono au wapi? mbna pale tabata muslimu (al farouq seminary, shule ya mwl.HASHIM SAIBOKO) hakuna daraja kuna uhusiano gani na hizo kokoto?

    ReplyDelete
  3. Wewe mdau hili daraja limejengwa sehemu gani?, ni ile njia ya kutokea Tabata Chang'ombe kuja machinjioni?. Hii njia ya kutokea machinjioni inasaidia sana watu wakati wa foleni, ila ikifika wakati wa mvua ni balaa. Nakumbuka mwaka fulani kipindi kama hiki nilipita huko asubuhi kuogopa foleni ya Ubungo ili nije nitokee tabata relini nikamate Mandela road. Nilipofika maeneo ya njiapanda ya Tabata chang'ombe nikakutana na Foleni inayotokea Tabata relini. Ikanibidi nikunje kulia niende kuvuka huo mto nilioutaja hapo juu (kutokea machinjioni). Ngoma niliyokutana nayo njiani kabla ya kuvuka huo mto sitaisahau. Kuna mahali kabla ya kufika kwenye huo mto palikuwa na korongo lenye matope, kwa kujifanya nina 4x4 nikaliingia hilo tope. Kutoka kwenye hilo tope ilinibidi niwapatia vijana kichele kisichopungua elfu kumi. Nilikoma ubishi siku hiyo.Nilifika kazini saa nne badala ya saa moja na nusu asubuhi.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  4. Yes Mdau kutoka cadiff, ni kweli hapo ni pale palipokuwa na matatizo ya matope zamani, ila kwa sasa pako shwari kama unavyoona kwenye Picha ,Pamejengwa daraja na maji yanapita chini ya daraja...

    Kwakweli ilikuwa inakera sana ila kwa sasa ni Pazuri sana hamna tatizo zaidi ya ile njia ya Baracuda,kutokea pale opposite na Chang'ombe ..
    Mdau Flo%

    ReplyDelete
  5. jamani sio kuwa mi nimkandiaji wakila kitu ila hilodaraja mbona kama limejengwa halina hata mvuto kama limepachikwa halina unadhifi hata kidogo hata usalama halina

    ReplyDelete
  6. daraja la muda lenyewe bado

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...