Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Busanda Finias Magesa (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe usiku wa kuamkia leo mara baada ya kupata matokeo kwamba chama chao kimeshindwa kwenye uchaguzi huo.

MGOMBEA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lolesia Bukwimba ametangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Busanda baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine vilivyokuwa vikishiri uchaguzi huo mdogo wilayani Geita kwa kura 29,242 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho hata hivyo kimekataa matokeo, kilishika nafasi ya pili kwa kupata kura 22,799.

Chama cha Wananchi (CUF) kilichopata kura 977 na cha United Democratic (UDP) chenye kura 271, viliingia mtini baada ya wagombea na mawakala wake kutoshiriki mchakato wote wa kuhesabu na kuhakiki kura katika hatua ya mwisho.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi, Dani Mollel alisema idadi ya waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 135,163, jumla ya waliopiga kura ni 55,660, kura halali zilikuwa 53,309 na zilizoharibika ni 2,069.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2009

    JAMANI DJ MBOWE KACHOKA KIASI CHA MAKENGEZA YAKE KUONEKA WAZI.

    HONGERA CCM WAONYESHENI WACHAGGA NA KULE BIHARAMURO.

    MWANAKIJIJI AU BENEDICT MWAKYANJALA ALISHASEMA KUWA CHADEMA WATASHINDA KWA ASILIMIA SITINI,

    NADHANI ANATUMIA NJIA YA KUPIGANA VITA YA WAMAREKANI AMBAO WALIPIGANA VITA NA IRAQ KWENYE COMPUTER WAKASEMA VITA ITACHUKUA MIEZI SITA LEO MWAKA WA SITA.

    CHADEMA WANAPIGA KAMPENI KWENYE JAMII FORUMS NA KUJIPA USHINDI WAKATI HAKUNA MTU WA BUSANDA ANAYEINGIA KWENYE JAMII FORUM ILIYOKUWA JAMBO FORUM KABLA YA KUIBA BRAND YA MICHUZI YAANI JAMII BLOG.
    YAANI WACHAGGA WAMEIBA EPA HAITOSHI HADI JINA LA BLOG MNAIBA?

    MDAU MSWAHILI.
    NILIYEKUWA MEMBER JAMII FORUMS LAKINI BAADA YA KUONA KUNAJADILIWA MAJUNGU NA KUUSIFU UCHAGGA NA CHADEMA NIMEACHA KUCHANGIA INAJIITA JF NADHANI TAFSIRI YAKE NI JUNGU FORUMS-JF.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2009

    Nakubalana na CUF kwamba adui namba moja wa demokrasia Tanzania ni CCM haiingii akilini hata kidogo hata kwa mtoto mdogo eti waliojiandikisha walikua takribani 130000 halafu waliopiga kura ni 53000 yaani 40% ya waliojiandikisha ndio waliopiga kura mimi sijakubali hata kidogo na hapa ndio CCM wanapoonesha uwezo wao katika kuiua demokrasia ya Tanzania kwa tamaa ya madaraka.CCm kumbukeni wizi wa kura ni hatari kwa amani ya nchi yetu kwani ipo siku twaweza kuona mambo yaliyotokea Kenya yakatokea na hapa Tanzania. Kamwe tusijidnganye kwamba wanajeshi na FFU wanaweza kuilinda amani ya Tanzania bali uhuru na haki ndivyo pekee vinavyoweza kulinda amani ya nchi hii.
    Ukiona comment inakukera bwana Michuzi we iweke kapuni

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2009

    Ha ha ha ha ha,I love politics!Just watching the game and not get involved.
    Yaani hilo wese loote la helkopta walilochoma jamaa lakini wapi.Ha ha ha ha ha,wallah hata ningekua mie ndo Mbowe lazima ningekataa matokeo kwa uchungu wa kuunguza wese.Ha ha ha ha ha!!We fikiria ukiingia sheli halafu ukute jamaa wameongeza bei hata shiling 10 utakavyoisikilizia.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2009

    Kwanza: Hongera CCM kwa Ushindi.

    Demokrasia gani hii sasa, Mbunge anachaguliwa na 41% ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura.

    Kwa nini hao wengine hawakupiga kura?

    1. Hawana imani na uchaguzi?

    2. Vituo vya kupiga kura vilikuwa mbali mno na maeneo wanayoishi?

    3. Hawataki/hawakubaliana na sera za vyama vyote au wagombea walioshiriki?

    4. Wananchi waliwekewa vitisho, wakaogoba kupiga kura?

    5. Takwimu inayoonyesha jumla ya waliojiandikisha (135,163) sio sahihi?

    Bado tuna safari ndefu.

    Hongera pia kwa CHADEMA, kura 22,799 maeneo ya Vijijini sio kazi ndogo; wamepiga hatua.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2009

    Jamani,haya ni maoni yangu tu.Hilo jicho alilitoa mwenyekiti hapo wakati anapewa brief, linonyesha hulka,husuda,jazba na munkari wa kukosa huo mnofu wa uongozi katika hilo jimbo.
    Kana kwamba haitoshi,hilo jicho lina element ya dictatorship as well.We cheki jamaa anavyojieleza kwa mwenyekiti hapo.
    Hii inatufundisha nini mtu kama huyu akishika nchi?????
    Jiulize halafu usinipe jibu.Huu unabaki kuwa ni mtazamo wangu tafadhali na sina ushabiki wowote na "si-hasa",ila ninapenda kuiona Tanzania ikibaki kuwa shwari.

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2009

    anoni wa 12:44 una akili sana. naomba niandikie email yangu ni tukae2000@hotmail.co.uk. tafadhali niandikie kama hutajali.
    Ahsante.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2009

    HIVI CHADEMA KUWA NA MAKENGEZA NI URITHI KWANI MWENYEKITI MSTAAFU MZEE MTEI AMBAYE NI BABA MKWE WA MBOWE NAE NI MAKENGEZA.KUULIZA SI UJINGA.
    MDAU MSWAHILI.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2009

    Hongera chama kubwa CCM kwa ushindi mlioupata.

    CHADEMA huu ni wakati mwingine tena wa kuelewa kwamba CCM walikuwa wanajidhihirishia kuwa Busanda ni jimbo lao kama walivyofanya Mbeya Vijijini na nyie mlivyofanya Tarime.

    Kubalini matokeo wananchi wameamua iwe hivyo

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2009

    mie ni ccm piga ua. lakini kwa matokeo ya busanda, naona aibu. wingi wa kula za chadema ni ishara za wananchi kuchoka na hadithi zilizotukuka za ufisadi. na pia nashawishika kuamini kwamba safari hii, tumeiba!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2009

    SAFARI YA DEMOKRASIA BADO NDEFU. NAPENDEKEZA YAFUATAYO:
    1. KUUNDWE TUME HURU YA UCHAGUZI
    2. VIONGOZI WA SERIKALI WAACHE KUTUMIA RASILIMALI NA VYOMBO VYA UMMA KWA MASILAHI YA VYAMA VYA SIASA.
    3. VIONGOZI WAACHE KUCHANGANYA NYADHIFA ZA KICHAMA NA KISERIKALI WAKATI WA KAMPENI ZA SIASA. ILI HILI LIWEZEKANE, JK AACHE UTARATIBU WA KUWAVIKA KOFIA ZA KICHAMA NA KISERIKALI WASAIDIZI WAKE.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2009

    CHADEMA NDIYO MPINZANI WA WAPINZANI ANGALIA MATOKEO YA CUF 2005. CHADEMA ILIKUWA YA TATU SASA KWA NINI CHADEMA WALIWAUNGE MKONO VUF BADALA YAKE WAMEKUJA KUCHUKUA WAPIGA KURA WA CUF, NINAVYOJUA MIMI WAPIGA KURA WA CCM HAWAKUAMA NDIYO MAANA WAMEIBUKA WASHINDI.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2009

    Tatizo lao wanamsikiliza mwanakijiji. Mlalost vie.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2009

    ina mana walioiba EPA wote ni wachaga?acha hizo wewe..kwahiyo kagoda ni ya wachaga? na bado mtaona wivu kwa wachaga hadi mkome. wachaga wanajali sana maendeleo ndio mana sehemu kama machame, marangu ni kama ulaya ndogo. Hata kama wanaiba lakini maendeleo tunayaona. CCM ni wezi hiyo haina kificho. lakini dawa ipo mwaka 2010 watakiona cha moto. sasa wewe unayewaonea wivu Wachaga kajinyonge? lakini bado wako juu babake. HABARI NDIO HIYO

    ReplyDelete
  14. Mdau, SoharMay 26, 2009

    Wizi mtupu!!! Aki narudi bongo nikajiunge na Chukua Chako Mapema (CCM) nigombee ubunge maana ndo lililobaki sasa, kuwaibia wananchi tu!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 26, 2009

    Bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, wasimamizi huru na system nzima ya uchaguzi kuwa huru haiwezekani demokrasia ikawepo. Wahusika wote ktk uchaguzi wanapokea amri kutoka kwa serikali ambayo ndio viongozi wa CCM, mnategemea nini? Pale wanapoona kuwa ni vigumu wapiga kura kukubali uongo (kama tarime) ndipo wanapoamua kuiachia demokrasia itawale. Kwa kujua hili ndio maana watu wengi hawapigi kura.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2009

    Tanzania bado tunasafari ndefu ya kuufikia `upinzani wa kisiasa' kawasababu bado vichwa vyetu vimetawaliwa na kasumba ya ukabila, udini ,ubinafsi na woga.
    Mtu kabla hajachagua ataangalia huyu ni kabila lake, ni dini yake au ni mwenzetu ambaye atalinda maslahi yetu.
    Sasa wenzangu na mimi ambao ni waumiaji tunafuata mkumbo, kama bendera. Tukipewa vikofia, khanga na vihela vichache na huko kijijini wakipewa `pombe' aah, apite.
    Lakini baya zaidi ni propoganda potofu, kuwa upinzani ni vita, upinzani hauwezi, hii ni hatari. Vitawezaji bila kupewa nafasi, Kunahitajika darasa, la kufuta hulka ya `chama kimoja' na hii itachukua muda sana.
    Kwa mfano hai angalieni makapuni kama ya simu jinsi yanavyoboresha huduma zao,hii ni kwasababu ya `ushindani', angalia kampuni kama Tanesco, halina mshindani, angalieni nini wanachokifanya. Bila ushindani(upinzani) hatuwezi kufikia malengo ya hali ya juu. Kidogo tu wamewaonyesha jinsi mafisadi wanavyofisidi, hamuoni hilo!
    Hayeni, wachagueni wazidi kujiimarisha, kujijenga na nyie kalagabahwe.
    M3

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 26, 2009

    hivi kama kweli ccm walishinda mbona walikataa kulinganisha form za matokeo yao na waliyokuwa nayo wasimamizi wa uchaguzi wa vyama
    pili na kama kweli ccm imeshinda itabidi twende vijijini tukawatoe tongotongo na utando wa masikio kwa sababu kelele zote hizo za ufisad hawazisikii na ukienda kijijini ndo watu wa kwanza kuomba misaada,
    kuhusu uchaga chadema hio ni propaganda za ccm tu watu walioenda shule wanajua,ingekuwa cuf ccm wangesema udini, wala hatuishangai na ingekuwa udp ingesemwa ukabila,ndio ,kuhusu makengeza ya mbowe mi naamni haihusini kabisa na uwezo mbona hatukuuliza upara wa mkapa,au kikwete kuvaa miwani ni kuwa haoni vizuri ,tuache kujadili mambo yasiyo kuwa na msingi

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2009

    sio makengeza. anaangalia pembeni au huangalii vizuri hiyo picha?? he!! we mwana CCM vipi!!!??

    ReplyDelete
  19. jamani ccm mnatupeleka wapi Watanzania? yaani watu zaidi ya 80,000 hawajatokea kupiga kura?
    kwa nini hawajatokea? ni wazi wameogopa idadi kubwa ya Police na magari ya mabomu ya machozi, gari la maji ya pili pili.

    ndio uchaguzi gani huo nyie ccm?
    jamani wangalizi wa nje oneni uchaguzi huru na haki wa Tanzania, nyie haya tu. iko siku

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 26, 2009

    CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!
    UPINZANI TANZANIA NI BADO MCHANGA SANA. HAUWEZI KUMCHUKUA DJ NA KUMPA URAISI...JAMANI WAKATI MWINGINE TUJARIBU KUKAA CHINI TUFIKIRIE.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 26, 2009

    Kusema ukweli inashangaza na ukifikiria sana inatia hasira, yaani 41% ya waliojiandikisha ndo wamepiga kura halafu unatangaza mshindi kweli? Tanzania!!!!??? siasa!!! demokrasia????? twashilaga. Noya

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 26, 2009

    chadema aona mwisho wenu ndo unakaribia,maana mnazidi kukopa na madeni yanazidi ya helikopta na bado hamshindi,angalieni sana 2010 karatu na moshi mjini,ccm watawapeleka kubaya,jaribuni kupiga kampeni za kisasa kama cuf,wanatumia hela ndogo sana na bado wanawafuasi wengi.

    ReplyDelete
  23. david villaMay 26, 2009

    Anon 12.44AM na 1.34AM mna akili sana.Comments zenu zimenigusa sana.Tuwasiliane kwenye atyini@yahoo.com.CCM wanajaribu kuzuia mafuriko kwa mikono lakini 2020 hawavuki.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 26, 2009

    matokeo yamenitoa machozi

    ndo maana walimwaga polisi kama walivyowafanyaia wazenji wakijua watayotenda.
    ccm angalieni sana 2010 hii itafunika kenya wananchi wamechoka,africa na uchu wa madaraka ndo maana hatuendelei japokua tuna kila kitu, viongozi mjue sote duniani ni wapita njia na idadi ya makahaba na mashoga inazidi kuongezeka mitaani sijui mtajibu nini mbele ya muumba?
    okay chadema tupeni matokeo yenu

    ReplyDelete
  25. Inasikitisha kuona waliopiga kura hawajafika ata nusu ya waliojiandikisha. CCM wana maoni gani juu ya hili? najua walipeleka mtandao mzima Busanda na CHADEMA kushinda ingekuwa miujiza lkn kwa takwimu izi kuna utata, je wale makada wa CCM waliokuwa wakinunua shahada ayo ndio matokeo yake? au watu wamelipwa wasiende kupiga kura? ebu angalieni kura zilizo alibika 2,069???
    Nilipenda CCM washinde lkn si kwa staili hii? ni aibu?
    Wapinzani punguzeni tamaa, mkiona hamuuziki majimbo ungeni mkono wale wanaokubalika, CUF na UDP mmeshindwa ata kupeleka mawakala, kama sio umamluki ni nini?

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 26, 2009

    mnaotoa maoni humu wanafiki tu ikishinda ccm hakuna demokrasia wakishinda wengine mnasema kuna demokrasia. mnakuwa kama ligi ya uingereza manchester akichukua ubingwa, liverpool, arsenal na chelsea wanasema subiri msimu ujao, refa kapendelea sababu kibao. mlikuwa mnasema subiri 2010 ccm wataona mnaanza kuona maji marefu imekuwa subiri 2020. mtakufa mnasema subiri na ccm itaendelea kutawala. kama watu wameamua kutopiga kura mtawalazimisha rejeeni kura za urais hata milion 10 kasheshe tanzania ina watu milioni 34 ina hao milioni 24 walikuwa under 18? kama mna wasiwasi kuna daftari la wapiga kura nendeni mkakague. michuzi usikasirike mimi ni liver damu ila nasema ukweli.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 26, 2009

    Idadi ya wapiga kura siku zote huwa ni ndogo. Vyama vya siasa ndio vinatakiwa viwe makini kwenye zoezi la kuandikisha wanachama wake wapige kura.

    Pia vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha hao waliojiandikisha wanajitokeza kupiga kura.

    Badala ya viongozi wa CHADEMA kuzunguka na helikopta, wangetakiwa kuandaa mabasi ya kuwachukua wapiga kura wao na kuwapeleka kwenye vituo vya kupiga kura.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 26, 2009

    CCM walinunua kadi za kupiga kura kipindi walipokuwa wanagawa vyandarua na mchele. Thamani ya Mtanzania ni chandarua, nguo na mchele! Ee Mungu tusamehe kwa kile CCM wanachotutenda

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 26, 2009

    Watanzania wengi hawajasoma na ndiyo maana CCM itaendelea kutawala milele mpaka watanzania wengi watakapopewa elimu.

    ReplyDelete
  30. Advocate JashaMay 26, 2009

    Huu nashindwa kuita ushindi na nia aibu kwa CCM ianaonekana zoezi la kununua shahada za kupiga kura kwa CCM limefanikiwa ndiyo ilikua njia pekee kwa CCM kuinusuru Kwanza ukiangalia idadi ya wapiga kura na waliojiandikisha kwa mtu mwenyeakiri timamuananaweza kupiga mahesabu.Pili ukiangalia CCM amabacho ni chama tawala kilitumia kila mbinu kuhakikisha kinashida kwa mbinu yoyote ile karibia baraza la mawaziri na viongozi wote wa CCM walikuepo Busanda Je uchaguzi wa Rais 2010 iabidi iwalike Obama,Mandela,Ghadafi,Mseveni,Kibaki, n.k ili CCM ishinde.Kwa jitihada walizozitumia CCM na matokeo ni wendawazimu kushabikia ya kua wameshinda na badala yake wanapashwa kujiuliza kwa kiasi gani imani ya wananchi hawaridhiki na uongozi wa CCM hiyo ni taa ya njano nyekundu inakuja.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 26, 2009

    Wadau wengi wanaotoa maoni yao hapa wanadhani ushindi huwa unapatikana bila ya mikakati na mbinu za hali ya juu. CHADEMA watake wasitake ni lazima wakubali kuwa bado ni wachanga katika siasa za bongo. CCM kwa kutumia uzoefu wake ilikuwa n auhakika kabisa wa kushinda jimbo la Busanda kwanza, tayari wana ngome ya kutosha kuwapa ushindi. Pili, walikuwa wanajua wapiga kura wao wako wapi, kwa hiyom walichofanya ni kuwafikia tu.
    Kwa staili hii CHADEMA watakuwa na kazi ya ziada katika uchaguzi mkuu ujao kwani bado hajawajua jinsi ya kuwachomoa wapiga kura wa CCM.
    CHADEMA itakuwa na kazi ngumu majimboni kwani wabunge wanashikilia majimbo yao sasa hivi wengi ni machachari na wanajua jinsi ya kuendesha kampeni zao hasa katika kuwafikia wapiga kura wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...