Mjane wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere (Mama wa Taifa) akizungumza na waandishi nyumbani kwake Msasani Dar es Salaam leo, kuhusiana na tuzo aliyoipokea Mapema mwezi huu kutoka kwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa inayotambua Mchango wa baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere katika ukombozi wa bara la Afrika,shoto ni Makongoro Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Watoto wa Taifa nao ni kina Madaraka na Makongoro Nyerere?Kina Kinjekitile mbona hawamo kwenye Hisotria?Walimwaga damu zao kwa nchi yao..Kina Abushiri au tunadanganywa kuwa walikuwa Waarabu na wauza watumwa?Kina mwana wa mwana wako wapi?wengi hawawajui na harakati zao zilikuwa zipi?Damu zao zimesahaulika Hawa ndio mababana mamama wa Taifa

    ReplyDelete
  2. wewe Anonymous wa Mon Sep 28, 11:07:00 PM
    uwe na nidhamu,
    mbona kuna watoto wa taifa waliojazana BOT na kwenye nyadhifa nyeti huwasemi? yani huyu bibi wa watu na wanae ambao walishirikiana na baba yao kuongoza ujenzi wa taifa hamuoni mchango wao hadi uwatukne hivyo?
    hivi huyu mama kaiba nini hadi sasahivi kwa urais wa miaka 25 wa mumewe? hebu angalia kina mama wengine ambao waume zao walikuwa marais wa nchi hii waangalie walivyovuna utafikiri paka kaona maziwa!
    angalia na wana wao walivyouchangamkia urais wa baba zao kujinufaisha na kujipatia mali za ufisadi!
    kuna watu safi kwenye familia za marais waliotangulia zaidi ya hii ya mwalimu?
    kama kuna mwenye hoja tofauti alete na kueleza rais mmoja mmoja na usafi wake unaomzidi mwalimu Nyerere

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...