Mimi ni mpenzi mkubwa wa blog ya jamii. Nimesikiliza BBC leo asubuhi, wanasema nchini Rwanda kuna sehemu serikali imekataza sauti za kidini (Adhana kuwaita watu kwenda kumswalia Mola wao na nyimbo za injili) sauti zake zisitoke nje ya jengo ambako zinaadhiniwa au zinaimbwa, ni kelele kwa watu!
Nyumba hizo zinatakiwa zisitoe sauti kuwafikia watu walio nje kiasi kwamba Waislam wamesema watawanunulia kila Muislam redio, watumie radio ya Kiislam kuwaita watu badala ya vipaza sauti vilivyoko misikitini! Ninachoshindwa kuelewa ni kuwa, hao watu (serikali) inaona afadhali sauti za walevi, matusi, kelele za vyombo mbalimbali ndizo zisikike badala ya adhana? Hizi serikali zetu zinatupeleka wapi! Kama utaona inafaa, irushe kwenye blog yetu watu wachangie. Inasikitisha sana!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. I would like to comment on the article above. First you need to understand that, your religion is everyone else religion.
    Mwathana is woking up everyone else, even though they are not part of that religion. Do not impose your religion to everyone, keep it to your self - there are ways you can spread your religion but not by disturbing everyone in the morning just because you are calling people to pray. I dont thinks there is a bar that is allowed to play a music loud to be heard by everyon else. All the bars should have a sound proof building material.

    ReplyDelete
  2. Kwanza ningependa nikufahamishe kwamba mimi ni muislamu na naishi UK, Huku kwetu vilevile hairuhusiwi kufanya vitu kama hivyo siyo dini tu hata club music n.k unless is live band(show) nazo hufanyika mahala maalum.
    Sasa ndugu yangu muislamu sijajua tatizo liko wapi kwani waislamu wote inabidi tujue nyakati maalum za sala(swala) na wala tusitegemee mtu au kitu kutukumbusha kufanya hivyo,wenzetu zamani(enzi za mtume) hawakubahatika kuwa na SAA(CLOCK) kwa ajili ya kuangalia mida ya swala hivyo walitumia utaalamu wa kuangalia kivuli na kuambiana kwa Adhana kwani siyo kila mtu aliyeweza kusoma kivuli(hata babu yangu mungu amrehemu nilimkuta akitumia staili hiyo).

    Sasa kama serikali imegundua kwamba Kengere za kanisani na maspika ya msikitini yanaleta matatizo ktk jamii kama kuwashtua wagomjwa,watu waliolala au kuna baadhi ya watu ambao hawana dini wanabughudhika na kelele za vyombo hivyo sioni kwa nini wasikataze na kama ulivyo sema waislamu wameamua kumia redio ili kukumbushana....Thus good man, why do we have to use the same old way everyday???? LETS USE RADIO THEN TV TO COMMUNICATE NA WAUMINI WETU
    Usikasirike ndugu yangu hizo ni miongoni mwa changes ktk maisha na wala siyo CHUKI.
    Mdau.

    ReplyDelete
  3. Hii pia ingetakiwa kuwa sheria Tanzania ambapo sauti ziishie kanisani na misikitini tu. Inakuwa ni usumbufu mkubwa kwa wakazi wa maeneo na mji kama kuna kelele asubuhi au jioni huwezi hata kupumzika kwa amani. Bravo Kagame

    ReplyDelete
  4. Wewe unapoenda kubeba BOX kunamtu anakugongea mlango? au ni DINI tu ndio inasahaulika?

    ReplyDelete
  5. Tatizo kubwa ni kuwa waafrika wa sasa tunakubali kutawaliwa na mabepari na kufundishwa kuwa kila kitu chao na kila wakisemacho ndo sahihi.wanatufundisha kuwa staili yao ya maisha ndo sahihi, vijana wetu wengi walio nje hawaishi kuponda nchi yao kila kukicha, tamaduni zetu zilizowalea mababu zetu leo zinaonekana ni potofu. tuache utumwa mamboleo. Adhana na kengele za kanisa zilikuwepo miaka nenda miaka rudi na hakuna aliyelalamika, ila leo hii kwa kuwa wazungu wanasema ni kelele, basi na sisi ndo tunaona ni kelele! mbona sisikii mkisema kuwa kuwa na mapadre mashoga si sawa? ni kwa kuwa mzungu kasema ni sawa nanyi mmeshaoshwa akili mnaona ni sawa! Afrika tunayoipenda inapotea hivi hivi! wajukuu zetu watakuja kutupiga wakipata historia ya mababu zetu then wangalie na hali tuliyowarithisha.Natamani kiyama kifike kabla ya kizazi kijacho. MUNGU BARIKI AFRIKA, MUNGU BARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  6. Kila kitu katika maisha kina utaratibu. Uchafu ni kitu chochote kilichokaa mahali ambapo si pake, hata dhahabu ikiwa ndani ya glass ya maji still ni uchafu. Vile vile sauti isiyo na mpangilio na utaratibu huitwa kelele. Kwa mtizamo wangu adhana Saudi Arabia, Kuwait, Iran na Iraq ni kitu ambacho ni sawa kabisa kwa sababu kinawafikia walengwa ambao ni zaidi ya asilimia 95. Tofauti na sehemu hizo au zinazoendana na hizo inakuwa ni fujo. Na kama kila kikundi fulani kikisema kipashane habari kwa njia kinachoona inafaa basi itakuwa ni fujo. Kwa misingi hiyo mimi binafsi naona hiyo ni hatua nzuri kuelekea kwenye ustaarabu wa kuheshimiana katika kuabudu na kupashana habari.

    Mpenda Amani

    ReplyDelete
  7. Jamani mbona hamkubali hata mabadiliko yanayojenga? Kwahiyo kama mtu umezaliwa kwenye mtaa wenye barabara za mashimo siku serikali ikija jenga barabara ya lami hautakubaliana na mpango huo mzuri mradi tu kwa kua umezaliwa mashimoni na mavumbini? Good Job Kagame.

    Mimi ni mwislamu swafi na nakubaliana na mpango huu. Ila mpango huu usiwe kwa waislam pekee. Hata wale akina Kakobe nao waweke lodspeakers zao ndani.

    ReplyDelete
  8. Mimi nadhani ni sawa tu maana sio wote humu duniani ni waisilamu/wakristu kuna watu hawana dini au wana dini nyinigine na adhana/nyimbo za injili zinakuwa kero kwao! Serikali haina dini na inataka kumpa haki y autulivu na amani kila mwananchi wake so BIG UP RWANDA! I wish hii kitu ingekuja Tanzania maana mtu umelala kwenye kiota chanko ghafla unasikia mayowe ya either adhana au mapambio kwakweli inachefua!

    ReplyDelete
  9. Kumekuwepo na kampeni hizi nchini Rwanda mara baada ya Vita na watu wa njia ya Msalaba wamekuwa mbele kupiga vita Adhana ambazo zilikuwepo kabla ya hawa watu wa njia ya Msalaba(Crusaders) kuwepo madarakani na watu wamekuwa hawana hata simanzi juu ya Adhana.Tatizo ni chuki za kidini na kama alivyowahi kusema Kagame kupinga kuzuiwa Adhana kuwa Adhana zinawasaidia watu waamke mapema kuwahi shughuli makazini na wanaaonekana kusumbuliwa na Adhana mara nyingi ni walevi na wavivu(hii ni kauli ya Kagame)
    Huyu mdau wa UK si Muisilamu , sijui mazingira ya Uingereza ila naambiwa kuna mahala Uingereza kama Barking kuna Kengere zinapigwa makanisani na anasahau kuwa Uingereza ni nchi ya kanisa tofauti na nchi zetu za Africa.Sidhani kama wewe ni Muisilamu ila unaonyesha kabisa wewe ni mkatonta na mwana Msalaba
    Hili ni suala la wanyarwanda

    ReplyDelete
  10. Sitaunga mkono wala kupinga maoni ya kuona mambo yanayohusiana na baadhi ya dini kama adhina na kengele kuwa 'kelele' katika jamii. Ningependa nikumbushe kwamba tusidhani wanaoona hali hizi ni kelele ni kwa sababu wameiga mambo ya kimagharibi na hivyo hawako sahihi katika kuiga kwao. Tukumbuke hata imani husika ni za kuiga kutoka Mashariki ya Kati. Kuiga hatujaanza leo. Tumeiga tukawasahau kina Kobelo.

    ReplyDelete
  11. KAMA NI UTAMADUNI, TUKISEMA UKWELI HIZI DINI ZOTE SI TAMADUNI ZETU TUMELETEWA NA WATU WALIOKUJA KUTUTAWALA HAPO ZAMANI, NA HATA HIVYO HATUKUWA TUNAFANYA ADHANA KWA VIPAZA SAUTI VYA KISASA, NI MTU NA KINYWA CHAKE KIKAVU ALIKUWA ANAADHINI SI VYA KISASA VYA UMEME, NCHI NYINGI SANA DUNIANI WANAKATAZA KELELE HADHARANI UNLESS IMEOMBEWA KIBALI NA KUKUBALIKA SI NA SERIKALI TU BALI NA WATU WA ENEO HUSIKA. RWANDA NI NCHI NA INASHERIA ZAKE WALA HAIFUNGAMANI NI DINI YOYOTE, IT IS A SECULAR STATE.

    ReplyDelete
  12. Kuna umuhimu wa kupunguza kelele katika jamii. Shughuli zote zinazoleta kelele zipigwe marufuku.

    Marufuku kupiga muziki kwa sauti mtaani (kama Uswahili wanavyofanya)
    Marufuku makanisa kupiga kengele
    Marufuku waazin kupiga kelele za "Swalaa! Swalaa!"
    , n.k.

    Kila mtu anatakiwa kujua muda wa sala ni saa ngapi. Ndio maana tuna saa na alarms.

    ReplyDelete
  13. Naungana mkono na Kagame.Huyu ni mwana Afrika halisi.Hizo kengele za makanisani na azana misikitini siyo utamadunu wa kiafrika.Hizo kelele zililetwa na Waarabu paoja na wazungu.Kumbukeni kuwa kabla hawa wageni hawajatutawala tulikuwa na dini zetu za asili bila kengele wala azana.Warabu walipokuja wakatulazimisha kufuta dini yao na wale waliyokataa wakaitwa makafiri.Na wale waliyokataa kufuata ukrisu uliyoletwa na wazungu waliitwa washenzi.Kwa maneno mengine wadau ni kuwa kama wewe ni muislamu basi pia ni mshenzi na kama ni mkristu basi wewe ni kafiri.Kwahiyo siyo tu kama walituletea makelele bali pia walitutukana.Wametupandikiza chuki kuwa Afrika ya leo kuna vita vya udini kati ya wakristu(makafiri) na waislamu (washenzi).Imefika wakati sasa makelele yabaki Mecca na Vatican watuachie total freedom.Kumbukeni kabla hawa wageni kufika Afrika kiwango cha maendeleo Afrika kilikuwa karibu sawa na Ulaya.Tuligundua maandishi Misri,tulikuwa na vyuo vikuu kule Tumbuktu,Gao Jene na Kataina.Tulikuwa na vikwangua anga pale Mwanamutapa kingdom ambapo waingereza wapofika wenyewe walibaki midomo wazi.Hongera sana Kagame,marais wengine igeni mfano huo.
    Toto Tundu - Upper Marlboro

    ReplyDelete
  14. Ndugu zangu nashangaa sana leo hii binadamu tunavyojisahau, kisa tu tuna mali ama tunajifanya tupo kimagharibi zaidi, Dini ni muhimu, Adhana ama kengele si makelele, Watu wengi haswa wenye kipato huwa wanachukulia dini kama kikwazo cha maendeleo yao, Kama ni suala la kelele MBONA KUNA MIKUTANO YA HADHARA? JE KWANI KILA MTU ANAPENDA SIASA?
    No one will live here forever, Chunga unachosema maana ni dhima kubwa, Kuna mtu anasema tunaiga wakati yeye hapo alipo kavaa suruali na c magome ya miti!
    Kuiga kilicho chema ni sahihi kabisa maana dini ni mfumo mzima wa maisha

    ReplyDelete
  15. safi sana kagame....kelele hazitakiwi katika utandawazi huu. hata wakristo makengele, manyimbo, vinanda na kwa waislamu adhana zimepitwa na wakati na isiwe tabu kwa wengine ambao hatuna dini na hatuamini Mungu. suala la dini ni lamtu mmoja personal. tumieni redio na majumba ya ibada yawekwe soundproof. hata Tanzania itakuja hiyo na hatutaki kusikia mtu analalamika lalamika hovyooooo....tupambane na maendelea na si kubishana masuala ya kitoto kama haya.

    ReplyDelete
  16. safi sana kagame....kelele hazitakiwi katika utandawazi huu. hata wakristo makengele, manyimbo, vinanda na kwa waislamu adhana zimepitwa na wakati na isiwe tabu kwa wengine ambao hatuna dini na hatuamini Mungu. suala la dini ni lamtu mmoja personal. tumieni redio na majumba ya ibada yawekwe soundproof. hata Tanzania itakuja hiyo na hatutaki kusikia mtu analalamika lalamika hovyooooo....tupambane na maendelea na si kubishana masuala ya kitoto kama haya.

    ReplyDelete
  17. Namuunga mkono Kagame na serikali yake kwa hilo. Kama hapa Bongo kwa sasa misikiti inashindana kunuanua spika kubwa kiasi kwamba huwezi kusikiliza kingingine chochote wakati wa adhana au mawaidha. Just imagine kwa mfano umekaa umepumzika saa mbili usiku na unashtuliwa na adhana kwa sauti kubwa mna kama hiyo haitoshi inafuatiwa na mawidha ambayo yatakufanya ushidwe hata kupumzika au kusikiliza hata habari.Ustaaraabu wa hivyo ukija hata huku bongo utasaidia sana.

    ReplyDelete
  18. Kama unahitaji kukumbushwa muda wa kuswali,bado hujania kuswali. Kama kila kanisa(roma. lutheran,TAG,EAG,kakobe,anglican etc) nalo liweke spika juu kukumbusha watu wao ibada itakuwaje? nyumba ya ibada zingine zipo katikati ya makaazi ya watu ambamo humo kuna wagonjwa au binadamu wasioihitaji kelele za jinsi hiyo. Hii iwe kwenye baa na kumbi za starehe zote.

    ReplyDelete
  19. Ndugu yangu ulietuma hoja hii kwa nini umekimbilia kuzungumzia zaidi upande wa dini moja. Kwa taarifa yako wanaongoza kupiga sana kelele hapa Rwanda ni makanisa na hii imelenga kwa dini zote mbili.Wamepiga marufuku adhana pamoja na mapambio kelele toka makanisani. Kuna utitiri wa makanisa umeibuka na mengine yako kwenye maeneo ya makazi ya watu inakua kelele kubwa sana.Tukumbuke zamani makanisa na misikiti na nyumba zingine za ibada zilikua zinatengewa maeneo yake. Sasa hivi wanakuja wamisionari wanapanga nyumba mtaani ghafla ni kanisa nadhani ukienda kuwauliza wakazi wa huo mtaa wote wataunga mkono hili tamko la kupiga marufuku.Kuabudu si kwamba kuwanyime utulivu wengine.

    ReplyDelete
  20. yaani i wish to embrance Kagame he is the most inteligent president in the world, he has sense and knows how to fit his ideas for positive change please wahusika take and act his idea. Nakupongeza kwani kelele sio za misikitini tu hata makanisani where i live nimezungukwa na msikiti na makanisa tofauti mawili you can imagine hizo kelele , na imani zetu tofauti unataka kupumzika wenzio wanasali basi tabu kweli kweli jamani ziwekewe bullet proof aaah sorry sound proof.

    ReplyDelete
  21. mi naunga mkono kabisaa hii kitu kuna mdau anasema ati tunaiga kwani enzi hizo mababu zetu walikuwa na hivyo vipaza sauti??? NATAKA NA PALE MUHIMBILI HOSIPITALI WAPIGE STOP HARAKA IWEZEKANAVYO! pale wagonjwa wa kila aina wapo na wengine wapo ICU hawahitaji makelele kabisaaaaaaaaaaa mgonjwa yeyote haitaji kelele bali mapumziko ni hayo tu mie naona redio ni bomba sana tena sio mkulima vile viredio vidooogo

    ReplyDelete
  22. Nafikiri afrika inahitaji wakina kagame kama sita au kumi hivi, au?

    ReplyDelete
  23. Kwasababu ni mambo ya dini, watu watakaopinga watakuwa wengi sana, hii ni hali ya kwaida, kwasababu wengi wanamuamini Mungu kwa midomo, lakini kimatendo ni ziro.
    Kuna kelele za ndege, kuna kelele za magari,music nk,hizi haziitwi makelele,lakini kelele za dini lazima zitatungiwa `walakini' Na hizi kelele za dini sio wakati wote ni wakati maalumu!
    Tujue sisi sote ni wapita njia, anayemiliki kila kitu, hata hiyo hali ya kuona hiki ni kelele au sikelele ni Muumba! Leo tuhalai nzuri yakuona hiki kinafaa, hiki hakifai, lakini.... Ina maana kila wanachopendekeza wenzetu wa mataifa makubwa ni sheria? Sijui

    ReplyDelete
  24. adhana haiwi kero isipokuwa kwa anaechukia, awe muislam au si muislam. Kuna mambo muhimu zaidi ya kuyazuia kwa manufaa ya jamii, kama vile kuenea kwa machangu kila kona katika miji mikubwa kama Kigali, hawa ndio carriers wa maambukizi na magonjwa mbali mbali ya zinaa, hawa ndio wenye kuvunja nyumba za watu na kusambaratisha familia za watu, hawa ndio wanaoitoa jamii aibu juu ya tendo la ndoa na likaonekana ni jambo la kawaida, hawa ndio wanaongeza idadi ya wagonjwa wa maradhi ya zinaa katika mahospitali yetu, hawa ndio nguvu kazi ya jamii iliyokataa kuwajibika kwa ajili ya jamii na wanaishia kuiboa jamii, hawa ndio wanaongoza katika kuyaporomoa maadili ya jamii, hawa ndio... list haina mwisho. Hivi hawa na sauti ya adhana ipi hasa ni kero zaidi kwa jamii na taifa kwa ujumla? Kwa kuendekeza chuki binafsi kwa dini za watu ndipo tunapoacha kushughulikia mambo muhimu zaidi na kung'ang'ania yasiyo muhimu.

    ReplyDelete
  25. Mdau mchangiaji namba mbili(from UK)...I would like to advice u, not to try to lament any thing in Islam without having appropriate knowledge of the matter, first go and study ur religion then come up with ideas carrying water..I'm feeling so pity to people like u..pls study first

    ReplyDelete
  26. Kelele (sauti) za spika za adhana inatakiwa zizuiwe,taasisi za kidini hazilipi kodi zozote yaani kuwepo kwake serikali haifaidiki kimapata(economic point) kwa unakuta hotel,guest,restaurents,au sehemu yoyote ambayo watu wenye heshimu wanaweza kupunzuka,kama hiyo sehemu ipo karibu na msikiti huwezi kupata wateja,hasa hotel,kwa hiyo uamuzi wa Rwanda naona muzuri sana kama ilivyo Ulaya
    ,

    ReplyDelete
  27. Nadhani watu tunapaswa kufahamu ni maana ya neno KELELE au MAKELELE sio kila sauti ya juu ni makelele. Pili nini maana ya Adhani na nani anahitaji zaidi, mgonjwa ambae yuko ICU anahitaji zaidi adhana kuliko...... NAWASHUKURU KAMA TUTATAFAKARI HILI

    ReplyDelete
  28. KAGAME IS FOR RWANDANS.. LONG LIVE COMREDE..

    WA-TZ HIZI "KELELE" MNAZITAKA WENYEWE NDO MAANA MNACHANGIWA VINANDA, SPIKA, MAJENERETA, NK NA MAFISADI...

    ILA, HAKUNA LENYE MWANZO LISILOKUWA NA MWISHO..

    UHURU USIOKUWA NA MIPAKA NI UTUMWA!

    ReplyDelete
  29. Ninaipongeza serikali ya Kagame kwa kuchukua uamuzi huo. Ni wakati umefika ndugu zangu tuheshimiane na kuona kuwa ni muhimu kujali afya na mahitaji ya watu wengine. Ni kweli kuwa adhana, kengele za makanisa, misafara ya harusi, muziki kwenye mabaa na baadhi ya kumbi za starehe ni kero kubwa kwa wananchi wengine ambao hata hawahusiki nazo kwa namna yeyote ile. Chukulia kuwa tunahitaji kujipumzisha, kujisomea na wengine ni wagonjwa wanahitaji utulivu ili kuaccelerate kupona. Hakuna sababu yeyote ya kulazimishana kuabudu kwa kuwa, kwanza, kila mtu atahukumiwa kwa dhambi zake na atapata thawabu kwa kuomba kwake binafsi, si kwa kuombewa na mtu wala kwa kulazimishwa kwenda kanisani wala msikitini. Pili, kila mtu ana uhuru wa kuabudu au kuto abudu dini yeyote. Tatu, ni haki ya kila mmoja wetu kuheshimiwa na kuwa na amani bila kubugudhiwa. Nne,uisilamu na ukristu si utamaduni wetu wa kiafrika, hivyo wale wanatulazimisha tuone kuwa sisi waafrika tunapotea kwa kutofuata hizo dini mbili wao ndo wanatupoteza. Dini zote hizi ni za wakoloni na zipo kwa ajili ya kutufanya tushindwe kuendelea tuwe watu wakuona kuwa tunamakosa kila saa wakati si kweli. Waliobuni hizi tamaduni walikuwa na nia ya kujinufaisha kwa kutawala na mapato na kutufanya tujisikie wanyonge na tusioweza lolote hivyo iwe kwao rahisi kutuzungusha wanavyotaka.

    La muhimu ni kuwa, serikali yetu pia ipige marufuku, muziki kwenye mabaa uswahilini tunamokaa, kelele za misafara ya harusi, kengele za makanisani, adhana, matangazo ya magari ya promosheni, na kadhalika.
    Sisi wananchi tunahitaji, kupumzika bila kubugudhiwa. wote wanaohitaji kuamshwa asubuhi watumie alarm, wapigiane simu, au watumie teknolojia nyingine itakayoweza kuwafanya watimize malengo yao bila kusumbua wengine. Dini yenu, starehe zenu, harusi zenu, biashara zenu, na kadhalika ni vyenu ninyi na kwa faida yenu ninyi, hivyo viwasumbue ninyi na si sisi sote. Tumechoka kulazimishwa kufanya na kusikia tusiyoyataka.

    ReplyDelete
  30. - yule mwislam mchangiaji #2 kweli anatia shaka - arejee maana ya adhaan kwa mwislamu wa kweli..kuishi Ungereza ndo imemwia nongwa?!..Hata hizo kengele, hivi waweza ku-imagine London bila kengele Big Ben??..Niliwahi kuishi Lushoto, pembeni ya cathedral nzuuri na kengele iloashiria alfajir, adhuhuri na magharibi, hapakuwa kero!..maendeleo ya mashaka - watajafunga viwambo sauti 'silencers' hadi majogoo kuwika alfajiri!..KIWALACHO KI NGUONI MWENU!!..adhaan, what a beautiful call..done in a beautiful sound..a reminder to the true believers..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...