Bratha Michu,
kama ujuavyo jumamosi ni pambano la watani wa jadi, hebu posti hii tukumbushane na wadau simba na yanga ya enzi hizo mimi nimejaribu kukumbuka festi eleven ya simba enzi hizo:
Mackenzie Ramadhani
Mavumbi Omari
Twaha Hamidu
Deo Njohole
George Masatu
Iddi selemani
Zamoyoni Mogella
Malota Soma"ball juggler"
Hamis Gaga "gagarino"
John Makelele
Malota Soma"ball juggler"
Hamis Gaga "gagarino"
John Makelele
Raphael Paul
mdau mwingine anisaidie kupanga vizuri
kaka umesahau. kipindi ambacho masatu alikuwa taifa kubwa basi na hussein aman masha alikuwepo coz walitoka wakati mmoja pamba ya mwanza wa tupwisa lindada mazembe. na masha alikuwa hawekeki benchi. so you should have included him
ReplyDeletenamkumbuka kipa P. mwangata alidondosha mchozi uwanjani baada ya kushindwa kudaka mpira.
ReplyDeleteliz
Kusema ukweli hilo Chama likuwa hatari ! Mtu kama Marehemu Gaga angeweza kuchezea timu yoyote duniani kama angekuwa na discipline ya mpira. Hivi wadau mchezaji kama Marehemu Method Mogela alitakiwa achezee timu kama Man au Liver Kutokana na kiwango chake.
ReplyDeleteMie mshabiki wa simba Kumbukumbu yangu nakumbuka GAGARINO alikosa Penalt Uwanja wa AMAAN,Zanzibar ilikuwa USIKU. GAGARINO alilia washabiki wa YANGA wakawa wanamtafuta alijificha Kilimanjaro Hotel. Ilikuwa KOmbe la Afrika mashariki na kati. Simba alikuwa Bingwa. Dogo.
ReplyDeleteDuh Enzi hizo hilo chama nakumbuka mie BW mdogo la Kwanza nikisikia SIMBA Sports Club Mtangazaji akisema The Champs nilikuwa najuwa ndio Jina lao la Timu Simba Sports Club The Champs. kumbe Mabingwa. Mwalimu.
ReplyDeleteWengi wa wachezaji uliowaweka hapo juu hawajawahi kucheza pamoja kwa wakati mmoja Simba.Mfano Malota Soma hajawahi kucheza na George Masatu.Ovyooo.Katafute kumbukumbu za soka la bongo halafu uje kurekebisha list
ReplyDeleteMie nafikiri TANZANIA wachezaji 3 hawa nafikiri wangecheza Mpira nje vizuri Kipindi ambacho wapo Method mogella(Mwenyezi amrehemu) na Hussein Masha na Rifat Said(mwenyezi Amrehemu) na Salvatory edward kama nimekosea jina lake niwekeni sawa wa Yanga. hata Thomas mashala wa Pan african.
ReplyDelete1Mohd Mwameja (TZ one wa ukweli)
ReplyDelete2. Kassongo othman
3. Deo Mkuki
4.Idd seleiman
5 Gorge Masatu
6 Juma Amir Maftah
7.Rashid Ramadhan (machine)
8.Hussein Aman Marsha
9 Edward Chumila (EDO BOY)
10 Madaraka suleima (Viminyio)
11 Duwa said
Kikosi ambacho sitoweza kukisahau tulimpiga Mecco bao 5-0 baada ya kuanza vibaya ligi mechi ya kwanza msimu 1990 baada ya kuponea kushuka daraja msimu uliopita kwa kuifunga yanga 2-1 mechi ya mwisho. Kikosi cha msimu huo kilikua hivi.
ReplyDeleteMackenzie Ramadhani/Patrick Mwangata,Mavumbi Omari,Twaha Hamidu,Deo Njohole OCD,Frank Kasanga Bwalya,Aston Pardon,Dan Mhoja/Method Mogella,Hamis Thobias Gaga "Gagarino",Malota Soma "BallJuggler",Zamoyoni Mogella "Golden Boy" anamalizia kushoto Edward Chumila "Sure Boy".
Mechi ya kwanza tulifunga Yanga 1-0 Mavumbi alifunga kwa free kick. Mechi ya marudiano tukihitaji ushindi kutangaza ubingwa tulipigwa bao 3-1 baada ya penalti ya Gaga kuota mbawa.Weekend iliofuata tukaenda kuchukua ubingwa kwa African Sports Tanga. Msimu uliofuata mar Method, Deo Njohole waliondoka.LUNYASI FOR LIFE
Mbigiri Yanga Damu tuachie wenyewe Simba yetu. Malota kacheza na George Masatu kikosi kilichofika fainali ya CAF 1993 japo Malota alikua anarejea uwanjani baada ya kuugua kwa muda ila wamecheza pamoja Simba
ReplyDeleteWachezaji waliokua na viwango vya juu na hakika wangecheza timu yoyote duniani ni Hamis Gaga, Athuman China, Hussein Aman Marsha, Mohamed Mwameja,Issa Athumani, Fumo Felician bila kumsahau Yasin Abuu Napili. Walikua wamekamilika kila upande urefu,ubavu na control za kumwaga!
ReplyDeleteUmesahau kuongezea, John Makelele aka. ZIGZAG PAJERO....ilikuwa balaa..Yanga wenyewe walikuwa wanazima fegi.
ReplyDeleteMdau
Uholanzi.
Mdau uliyesema Gaga alikosa penati naona hiyo siyo kumbukumbu bali ni usahaulifu. Mechi hiyo aliyekosa penati alikuwa beki Mwakalebela (David?). Na huyo mdau aliyedai kuwa atiMasatu na Malota hawajawahi kucheza pamo wewe ndoi ukatafute kumbukumbu. Wakati simba inafika fainali za CAF 93 masatu alikuwa Simba na Malota alikuwemo sasa kama huko siyo kucheza pamoja sijui tuiteje.
ReplyDelete1.Idd Pazi 2.Deo Mkuki 3. Twaha Hamidi (noriega)4 Mustafa Hozza 5 George Magere Masatu 6.Hussein Aman Masha 7John Makelele 8Hamis Thobis Gaga 9.Zamoyoni Mogela 10.Malota Soma 11.Itutu kigi
ReplyDeleteMdau
Kisiju Pwani
Dah, Combination ya Mustafa hoza, george masatu na Hussein marsha ilikuwa sio mchezo, mbele kina Hamisi gaga, Zamoyoni mogella.
DeleteNamjibu Mbigiri-Yanga damu... Georege Masatu alishwai kucheza na Malota Soma. Kama unakumbuka Fainali ya kombe la CUF SIMBA VS STELA ABJAN Mwaka 1992 Masatu alisimama mkoba tisa Malota
ReplyDeleteMdau wa saa 6:38 , nakubalina na wewe ya kuwa Marehemu Method alikuwa na uwezo wa kucheza klabu yoyote kubwa kwani alikuwa na nguvu , spidi na zaidi alikuwa ni mtu wa kujituma. Masha i seriously doubt, the guy had talent but he was too slow ! Michuzi nadhani utakubali ya kuwa Marehemu Method angeweza kuchezea Liverpool . Ninependa sana kusikia maoni yako kuhusu hili...
ReplyDeleteWana SIMBA wenzangu je mnaikumbuka listi hii? 1 Mohammed Mwameja, 2 Kasongo Athumani ,3 Twaha Hamidu, 4Mustafa Hoza, 5 George Masatu, 6 Hussein Masha, 7 George Lucas, 8 Athumani China, 9 Madaraka Suleiman A.K.A. Kiminyio, 10 Ntheze John 11 Duwa Saidi. Hivi kocha mcheza Azizi nyoni yupo wapi?
ReplyDeleteSimba ilikuwa na kocha mchezaji mmoja tu, alikuwa Hassan Hafif
DeleteWanasimba wenzangu je mnakumbuka ma2kio haya? Hamisi Gaga Lino alipochana nyavu Simba vs Majimaji bao la 2ta yanga wakadai eti nyavu zilikuwa zimelowa. Mnakumbuka 2lipowafunga Atlatico Aviacao ya Angola Muhammed Jongo akawa anayangaza Simba wana2piwa mawe? Mnakumbuka 2lipoifunga El hillal ya Sudani 2lipigwa mpaka Ntwa Kiwhelu alikula nyuzi 3, Samola Saidi mdogo wake Duwa saidi alikula nyuzi 5 na kibadeni na mwenyekiti wa FAT walivunjika viuno. Mpaka Rais Mwinyi akai2mia barua viongozi wa mpira wa Sudan
ReplyDeletekipindi cha GM(George Masatu)kipa alikua 1 Mohamed Mwameja Tanzania one,2 Omary Mavumbi,3 Twaha Hamidu(Noriega)4 Hamza Maneno au Mustafa Hoza,5 George Masatu,6 Hussei Masha,7 Thoma Kipese(Uncle Tom)8 Marehemu Ramadhan Lenny(Abbega)9 Malota Soma,au alikua Damian Kimti,10 Gebbo Peter, 11 alikua Dua Said.Kama nimekosea, wapenzi wa Simba lunyasi nikosoeni.Mdau Seven sisters London
ReplyDeleteDu wadau tunakuwa tunakumbushana mbali,John Makelele(zig zaga)nimepiga nae kabumbu kule T.P.C pamoja na Abdalah Bori ambae amekipiga Pamba ya Mwanza.
ReplyDeleteBila kumsahau Salehe Sonda
Na hii je?
ReplyDelete-Sahau Kambi
-Minziro
-Ken Mkapa
-Godwin Aswile
-Salumu Kabunda
-Isa Athumani
-SAnifu Lazaro
-Athumani Abdala {China}
-Makumbi Juma
-Justine Mtekele
-Thomas Kipese.
Mdau fidel
LUNYASI FOR LIFE
ReplyDeleteyaani hapa.....
Mackenzie Ramadhani/Patrick Mwangata,Mavumbi Omari,Twaha Hamidu,Deo Njohole OCD,Frank Kasanga Bwalya,Aston Pardon,Dan Mhoja/Method Mogella,Hamis Thobias Gaga "Gagarino",Malota Soma "BallJuggler",Zamoyoni Mogella "Golden Boy" anamalizia kushoto Edward Chumila "Sure Boy".
ndo umenigusa.yaani hii ndo list niliyointend kuikukmbuka, nashukuru umeikukbuka tena nakumbuka tukapigwa 3-1 na yanga nilikuwa bwana mdogo tu enzi hizo lakini niliumia kweli.Thanks
Aaaah ww sasa na huku zenji small simba kulikuwa na
ReplyDeleteAlly bushiri/Ridhaa Khamis
Issa lambo
Rashid Tall
Karume Mussa
Innocent haule
Omar King
Omar marungu
Juma bakar 'kidishi'
wengine nmesahau nlikuwa bwamdogo kipindi hicho
Malindi:
Yassin Saleh
Mbegu Mohammed
Seif Bausi
Ally Nassor kibichwa'
Ally Shariff 'Adolph'
Hamad Hilika
Athanas Micheal
Shekha khamis
wengine ntarudi kukumbusheni baadae hao fasta fasta
mnayazitaka kumbe
ReplyDeletesigara nayo
1.nyalusi
2.abubakari kombo
3.azizi nyoni
4.peter lucas
5.iddi cheche
6.abunu issa
7.msamba
8.ladislaus shaha
9.mwakatika
10.michael bulton
11.shabani anania
coastal union
1.rifat said
2.said kollongo
3.deoglatius muhani
4.yasin napili
5.ruben mgaza
6.ally maumba
7.kingsley mwalilo
8.kassa mussa
9 juma mgunda
10 husein mwakuluzo
11.razak yusuf
mdau mussa salum
HAHAHAHAHA MIE MBAVU SINA HAYA WA IRINGA JE NA LIPULI? ISSA MICHUZI TAJA KIKOSI CHETU CHA PAN AFRICAN. SMALL SIMBA HIYO NDIO ILIKUWA INATISHA MIE SIMBA NAYOIJUWA
ReplyDeleteMohd Mwameja (TZ one wa ukweli)
2. Kassongo othman
3. Deo Mkuki
4.Idd seleiman
5 Gorge Masatu
6 Juma Amir Maftah
7.Rashid Ramadhan (machine)
8.Hussein Aman Marsha
9 Edward Chumila (EDO BOY)
10 Madaraka suleima (Viminyio)
11 Duwa said -- MUUWAJI WA YANGA
Bench Kuna Kimti muuwaji wa kuwamaliza watani.
Mnakumbuka NONDA NA KIMANDA walivyokuja SIMBA ILIMLA YANGA 4-1.
WEKA KIKOSI CHA PAN AFRICAN MICHUZI. MSWAZI KWA MANGARA.
Mie nawakumbuka hawa.
ReplyDeleteMACHUPA,MASAMAKI,MANYANYA,KACHUMBARI, ALI MAYAI,MAVUMBI, HAWA walikuwa nawasikia Sana KUTOKA RADIO MBAO mpaka MACHUPA NIMEKUJA KUMSIKIA RADIO PLASTIC. PANYA BUKU.
Kuna wadau wanasema Athuman China angeweza kucheza popote. Mnasahau alipata nafasi ya kucheza Reading (hii hii iliyokuwa ligi kuu miaka michache iliyopita huko England) akachemsha mwenyewe. Kuna mdau amemchezesha China Simba. Kumbukumbu zangu zimefuta hicho kitu.
ReplyDeleteKikosi burudani kilikuwa cha Tukuyu Stars cha kina Aston Pardon.
pan Africa hiyo
ReplyDelete1.sadik kalokola
2.said kollongo
3.nuldin kasabalala
4.idd cheche
5.abibu kondo
6.idrissa ngulungu
7.Ally yusuph tigana
8.ladislaus shaha
9.julias kalambo
10.Abdallah msamba
11.Thomas Mashalla
unataka ipi
mdau mussa salum
wadau nimepeda sana comment zenu nzuri sana za kukumbushana mambo yaliyopita pale kwetu husussani mpira wa miguu na wachezaji wote mliowataja walikuwa ni faraja kwetu,lakini mmetaja wote mume msahau mmoja RAMADHANI LENNY hunu vipi mbona hamumuongelei
ReplyDeleteHswaaaaaaaaaaaaaa hii ndio nimeitaka mie ya Pan african Bench kakosekana Akida makuda. Mussa Salum ahsante sana Nurdin Kasabalala Rafiki Jamaa huyu yupo magomeni. Kalokola si mburundi? alikuja na kina Kamanda na nonda au? kama si mburundi ni mtu wa Congo.
ReplyDeleteKosi hili huwa silisahau:
ReplyDelete1.Idd Pazi "Father"
2.Mussa Kiwelu
3.Daud Salum "Bruce lee"
4.Deo Njohole "OCD'
5.Athuman Maulid "Big man"
6.Ramadhani Lenny "Theophill Abega"
7.Sunde Juma "Pikipiki"
8.Ezekiel Greyson "Jujuman"
9.Malota soma "Ball Juggler"
10.Zamoyoni Mogella "Golden Boy"
11. Ibrahim Marekano
Kwangu mimi vifaa ambavyo vingeweza kutuwakilisha vizuri nchi za nje enzi hizo. Kuna Method Mogella"fundi", Salvatory Edward"mtaalam", Yusuf Macho"musso", Deo Njohole"ocd".
ReplyDelete