Marehemu Swetu Ramadhani Fundikira

Inaniwia vigumu sana kutoa shukran kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi kutokana na ushiriki wenu kuanzia kujeruhiwa mpaka mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira. Basi pale nitakapokuwa nimekosea kwa kumsahau kumtaja mhusika naomba radhi.

Kwa niaba ya familia ya Mzee Ramadhan Said Fundikira na ukoo wa Fundikira kwa ujumla, tunapenda kutoa shukran za dhati kwa watu wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa ndugu yetu mpendwa.
Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini pia ningependa kutoa shukrani za pekee kwa uongozi na timu nzima ya Mango Garden Veteran Team kwa ushirikiano wanaoendelea kuutoa kwetu hata mpaka baada ya mazishi.
Shukrani pia ziende kwenye vyombo vya habari vyote kwa ujumla yakiwemo magazeti mbalimbali, mitandao (blogs), televisheni na radio zote walioshiriki katika kuupasha umma unyama aliofanyiwa ndugu yetu.
Naomba niishukuru sana Radio Clouds FM kwa kurusha mwenendo wote tangu mwanzo hadi mwisho wa mazishi,Uongozi wa ASSET Entertainment, Madaktari na wafanyakazi wa MOI, Vituo vya Polisi cha Salender Bridge na Oyster Bay, Mkuu wa kitengo cha maabara cha Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Masheikh wa Masjid Jamia Kinondoni na kila mmoja aliyeshiriki kwa hali na mali katika mchakato mzima wa mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Swetu Ramadhan Fundikira.

Sisi wana familia hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu atawalipa Inshaallah.
Inna Lillah wa Inna Illah Rajiun
Ismail R. Fundikira
Msemaji wa Familia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. DU UCHUNGU KWELI YANI MACHOZI YANANITOKA HUYU KAKA KAFA KIFO KIBAYA SANA HERI ANGEZAMA BAHARINI.OLE WAO WATOAO ROHO ZA WATU KIAMA CHAWASUBIRI.DU POLENISANA SHEMEJI ZANGU.WAJUE HATA WAO WATAKUFA TU KWANI PUA ZAO ZIMEANGALIA WAPI MBINGUNI AU ARDHINI NA WALLAANIWE MILELE

    ReplyDelete
  2. ati ndugu zao hao wauwaji wako busy wanatafuta malawyer utamu zaidi ni kwamba hawana hata hela wanafanya vikao kama vya arusi ati ili wachangishane wapate milioni kama 25 za kumpa lawyer ili awasaidie katika kesiyao ya mauaji na mtashaa hamtapa ng'oo hizo hela damu ya mtu haimwajigi bure hiyo itawaandama tu hamkuwa na huruma nyinyi kweli naomba kwa Mola mfungwe milele

    ReplyDelete
  3. Broda Michuzi mbona hutupi updates za huyo askari aliyetokomea kizani???Haiwezekani mpaka leo akawa hajakamatwa!!!!HIVI BONGO MKO SERIOUS NA KITU GANI???Maana kila kitu huwa kinaachwa bila kufikia mwisho wake!!!!!!!Richmond,EPA,TWIN TOWERS,Governor's house na sasa Swetu-RIP, na huko India - Imran mmmh nimekata tamaa na nchi yangu.

    ReplyDelete
  4. nimesikitika sana na bado najiuliza kwa nini yeye kakaangu rafiki yangu rafiki wa wote lakini nasubiri ukweli na mauwaji yanayofanywa na mapolisi na wanajeshi watanzania sasa serikali yetu inatuua mmoja mmoja na wote humu ndani mnaelewa na hata serikali haitujali lakini sasa tunataka kujua ukweli time imefika tanzania polisi na wanajeshi ni wauwaji na wote wanatumwa na serikali sitapumzika kakaangu mpendwa mpaka natakapo ona haki inafanyika na hao waliokuondoa machoni kwetu cha moto watakiona kuanzia duniani mimi niko na wewe kakaangu na kitabu nitaandika unyama na mauaji yanayofanywa na nchi yako unayoipenda. ROHO INANIUMA MACHOZI YANANITOKA . MUNGU ALAZE ROHO YA KAKAETU MPENDWA PEPONI DAIMA TUTAKUKUMBUKA NA TUMAMISS UPENDO WAKO.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Ismail. sisi sote tumepatwa na machungu hasa ikizingatiwa kuwa Al marhoum Swetu alikuwa mwenzetu uwanjani kusakata kabunbu. zama zilee za Moshi. Nakumbuka tulikupa jina Okalla kwa jinsi ulivyokuwa mahiri golini zama zile.
    Hakika kwa Mola sote tumetoka na kwake ni marejeo yetu sote.

    ReplyDelete
  6. Pole sana Ismaili na familia nzima ya Fundikira.....

    barnabas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...