mwendeshaji wa kipindi kipya cha TV katika TBC1 Maria Shaba akiongea na mwakilishi toka ubalozi wa Uingereza nchini pamoja na prodyuza Dk. Martin Mhando na msanii Vitalis Maembe, Rose Haji wa MISA-Tan na Mh. John Mnyika wa CHADEMA baada ya kukamilisha kurekodi sehemu ya kwanza ya kipindi cha 'Kitimtim' kitachoanza kurushwa hivi karibunik ikiwa ni kuamsha na kuelimisha wananchi kuhusu wajibu na haki katika uchaguzi mkuu. Fungua dimba ni mada ya Ushiriki na utendaji wa vyombo vya habari katika uchaguzi mkuu
Home
Unlabelled
TBC yaandaa kitimtim cha uchaguzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nakupongeza Mama Maria Shaba,zidisha juhudi na maarifa zakutuelimisha kwani wengi wetu bado hatujui wajibu na haki za chaguzi zetu kitaifa
ReplyDeleteMpili
Ikiwezekana wakati wa kampeni ukifika mtuandalie mdahalo tujue wagombea urais watatufanyia nini na watafanyaje kufikia malengo hayo. Uchaguzi uliopita ulipita kimya kimya basi hata malengo ya rais hatukuyajua wala jinsi atakavyoyafikia. Lengo pekee lililokuwa wazi ni la kutengeneza ajira milioni moja. Haukutolewa ufafanuzi kwamba wanaohitaji ajira watakuwa wameongezeka kwa kiasi gani. Tumeambiwa malengo yametimia kwa kiasi kikubwa kupitia sekta isiyo rasmi lakini inakuwa vigumu kutofautisha walichokuwa wanakifanya kabla na ajira zao mpya.
ReplyDelete