SIKU YA IJUMAA 27 - 03 - 2010 MAJAMBAZI WALIVAMIA DUKA LA DHAHABU LA SAFARI LEWELLERS LILILOPO MTAA WA UDOE.
UWIZI HUO ULITOKEA KATI YA SAA NNE NA SAA TANO ASUBUHI. KWA YEYOTE MWENYE UWEZO WA KUTOA TAARIFA ZITAKAZOWESHA KUPATIKANA MZIGO ULIOBIWA ATAPATA ZAWADI YA SH. MILLION TANO.
TAFADHALI PIGA SIMU KITUO CHA POLISI KILICHO KARIBU NA PIA NAMBA ZIFUATAZO:
- 0713 40 22 43
- 0713 46 53 36
- 0716 11 11 74
UONGOZI WA SAFARI JEWELLERS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. JAMANI THIS IS TOO MUCH SASA... HIVI MBONA UJAMBAZI UNAONGEZEKA TENA KILA MWAKA WA UCHAGUZI? AU JAMAA WANADHANIA SERIKALI IPO BIZE NA KUPATA HELA YA UCHAGUZI... HALI INATISHA SASA INABIDI JESHI LA POLISI LIJIDHATITI KIKAMILIFU KUPAMBANA NA HAWA WATU. HALI ILITULIA KAMA MWAKA MMOJA ULIOPITA LAKINI SASA INATISHA HATA MTU KUWA BIASHARA YAKO INAYOINGIZA VIZURI UNAKUWA NA WASIWASI MUDA WOTE NA ROHO MKONONI... HUKU NI KUGAWANA UMASIKINI SASA.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  2. NI VIZURI KUSAIDIA ILA KWA TANZANIA YETU UKIENDA NA UKIJUWA UTAAMBIWA NA POLISI NA WEWE UMEHUSIKA BURE UKAOZELEA NDANI KISA ZAWADI YA MILLION 5. AU MNASEMAJE WADAU WACHA WAMALIZE UCHUNGUZI WAO WENYEWE NA WALINZI WAO KWANI SECURITY WA HIZO SEHEMU WANAKUWA WAPI NA MAPOLISI?.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...