Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, Naibu Gavana wa BOT, Lila Mkila, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mh. Mwanaidi Senare Maajar na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani,Grace Shangali, kwenye Mkutano wa Diaspora 2 unaondelea leo hapa London
wadau mbali mbali waliofika katika mkutano wa Diaspora 2 wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa awamu nyingine ya mkutano huo unaoendelea kufanyika hapa jijini London

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. mimi hii diaspora inaendelea lakini sijawaona diaspora orjino. Hebu pigeni picha ya pamoja ya hawa wataaramu na mtundike kwenye globu ya kamii ili tufahamu wazi kwamba hawa wakubwa wapo
    1. nabii mtakatifu yohana mashaka
    2. dakitari hideband shayo
    3. mdau (John)UK
    4. mbuzi us blogger
    hawa wakuu inabidi wapige picha ya pamoja uko dispora uingeleza. hii diapola ni batili kwa maana haisaidii chochote. ni forum tu ya mafisadi kuuza sura. kama hawa diaspora ni muhimu ana, mbona walioko nyumbani wasipate kazi na wale ni wazalendo orijino? hidebandi shayo anaishi huko rondon, naye nabii yohanna mashaka anaishi mtaa wa piri pale wostriti. au walikesha kwenye kubeba boxi ndo maana hawaonekani kwenye picha ya pamoja? jitahidi sana utuwakilishe mkuu

    ReplyDelete
  2. Candid ScopeMarch 27, 2010

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    Najiuliza maswali mengi kuhusu mkutano huo kwani naona pichani wajumbe ni watanzania. Kwenda kufanyia mkutano huo UK ni kutalii? Kuna umuhimu gani wa mkutano huo kiuchumi na maendeleo ya Tanzania na nani anagharamia huo mkutano.

    Huku nyumbani watu wanazidi kuteketea kwa malari, ajali barabarani, njaa, miundombinu dhaifu, udhalilishaji wa jinsia, matumizi mabaya ya pesa za umma, ufisadi nk. Je huo mkutano upo kwa malengo gani? Kama ni watanzania tu kwa nini usifanyike Tanzania ili kupunguza gharama zisizomuhimu? Gharama hizi za matanuzi kwa mwaka mzima hata kama zinafadhiliwa afadhali zingeelekezwa kuongeza barabara za jiji la Dar ili kupunguza msongamano wa magari. Au pesa hizo tungejenga barabara mpya ya Mpanda-Tabora, Mbeya-Tabora, Mwanza-Kagera, Kaliua-Kigoma, Bagamoyo-Tanga, kuboresha mbuga za utalii, kutoa mikopo ya wafanyabiashara ili kuanzisha viwanda vya uzindikaji vyakula kitaalam ili kuondokana na uuzaji wa vyakula holela visivyoandaliwa kitaaluma kwa ajili ya kujenga afya bora.

    Wenzetu walioendelea wamefikia hapa walipo kwa kutanguliza ya muhimu kwanza isiwe tunajenga historia ya kushindana au kuiga wakati tungali tunatambaa tunawaiga wanaokimbia mwendo wa kasi sisi tunawafuatia kwa kutambaa. Tupo UK hatujifunzi waliyonayo muhimu katika maendeleo na tutakaporudi bongo na kutafuta za walipa kodi kujaribu kuziba mifuko iliyotoboka.

    Nadhani maisha yangu yote ningeishi bongo tu nisingefunguka akili kuyaona kwa upana haya yanayoendelea, na nilichojifunza ni kutoka nje ili kujifunza yale yanayotufaa na kuyabeza yasioyotuletea maendeleo kwa nchi yetu.

    Kwa hakika tunahitaji kizazi kipya cha sasa chenye uchu wa kuleta mabadiliko ya kweli kimaendeleo, maisha, na upevu wa kuchambua ya muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.
    Naipenda nchi yangu na watu wake. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

    ReplyDelete
  3. Umakini wa kuandika habari hii vipi tena? Michuzi - hebu rekebisha jina la Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.... Sio Hally bali ni Harry

    ReplyDelete
  4. Mkutano mzuri wenye malengo mazuri (angalau unapoangalia makusudio ya baadae katika maandishi). Maoni yangu ni kwamba: Hii mikutano ni ya muhimu sana na ni ya kuigwa katika kila nchi huku ughaibuni. Kila mtu anayeishi ughaibuni (kwa kadri nijuavyo) anachangia maendeleo ya nchini kwao (informally) kwa kuwajali watu wa familia zao. Mfano: Kusomesha wadogo zetu, kujenga vibanda vyetu, kufungua vi-biashara vidogovidogo na misaada midogo katika vijiji vyetu....Somalia na Eritrea ni moja ya mifano bora niijuayo ambapo wananchi wake wanaamua kujenga nchi zao kwa kuchanga pamoja. Nadhani kuwa Diaspora tunaweza kufanikiwa hapo baadae ikiwa misingi hii ya leo itatiliwa maanani. Lakini, nasema Lakini; Ushirikiano wa uaminifu unahitajika ili tufikie maendeleo tunayotarajia. Tuendelee kupendana na kujengana na kuwa na mawazo chanya (positive attitude) ambayo huushinda ufisadi hata kama upo kwa uwingi. Mungu awabariki wote wenye mawazo ya kuijenga Tanzania.

    ReplyDelete
  5. @ANYNY wa kwanza. Haujatulia kabisa, umenicheksha sana ndo maana naipenda hii blogu ya jamii. Mashaka siyo Diaspora. Diaspora ni watanzania wanaoishi nje ya nchi. Na pia Dr. Shayo yupo Tanzania, na mashaka anaishi Marekani, na sidhani kama aliudhuria huo mkutano. yaani umenichekesha sana

    ReplyDelete
  6. Mimi sioni faida ya hii mikutano. Kuengeza gharama na kutafuta vyeo visivyo na msingi. Ni nini manufaa yatu sisi kwa kuwa na huu mkutano kweli. Kama huu ni wa pili wakwanza ulileta manufaa gani kwa watu?

    Na gharama za huu mkutano ni nani kagharamia?

    Wanawasaidiaje watu bongo sana sana hao wanaomaliza vyuo vikuu kufanikisha maelendeo au kutumia elimu yao katika maisha yao?

    Baada ya mimi kusota na maisha na mwishoe kufanikiwa kukopesha hela kuja kujisomesha na kutafuta maisha (majority of us is what we do) Mnatufuata huku sasa na kutuona kuwa tunafaa sasa kukaa na nyie kwa mikutano....je mlikua wapi tulivyokua tunasota bongo? Kwa nini sasa hivi mnatufuata na kufanya mikutano huku?

    Honesty I don't see the point zaidi ya wachache wanaotaka uongozi na kuandaa hii mikutano ili wakirudi bongo wagombee kazi serikalini kupitia migongo ya watu.

    That is just me

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi,
    Mimi sipingi hii mikutano ya diaspora kabisa. Ila ninapinga kuhamisha wakuu wa serikali na taasisi eti kwenda nje kutoa blabla kwa wananchi. Hizi ni kazi za Mabalozi wa Tanzania na maofisa wao huko nje. Ndiyo maana serikali ilifungua hizo balozi na kupeleka wataalamu huko ili wao wawe ndio wawakilishi wa serikali na asasi zake huko.
    Sasa huu utaratibu wa kuhamisha mawaziri, viongozi wa taasisi za serikali kwa kutumia fedha nyingi za walipakodi ili hali Serikali ina hali mbaya sana ya kifedha mimi sioni mantiki yake.
    Kwa mfano hiyo Wizara ya Mambo ya Nje imeshindwa kutekeleza hata Sera ya Nchi ya Mambo ya nje katika eneo la Diplomasia ya Uchumi. Wizara imeshindwa kuzihudumia Balozi zake ipasavyo kiasi cha kufikia hatua ya kufungiwa huduma muhimu kama maji, umeme, na hata kutishiwa kufukuzwa wafanyakazi wake. Sasa unampeleka Waziri na timu yake UK kufanya nini. hii timu ingeacha kwenda huko tungepata fedha za kulipia kodi za Ofisi na nyumba za watumishi kule Brazil, Ethiopia, Uswis,Sweden, Marekani, Italia na kweningineko ambako kuna hali mbaya sana.
    Napenda kuungana na watoa maoni wengine kuwa si la zima kupeleka timu lukuki huko nje kwa fedha nyingi za walipakodi ilihali hali ya serikali kifedha ni mbaya sana...Sasa wanapata wapi fedha za kusafiria wakati hakuna za kutoa huduma muhimu kama kulipia kodi za ofisi na nyumba za wafanyakazi wake wa ubalozi, kujenga barabara, kununua vyandarua, na mambo kibao tu...

    ReplyDelete
  8. Kwa hesabu zangu za haraka haraka tulizopatiwa na mtaalamu wetu hapa UK anatuambia kuwa uongozi wa serikali na asasi zake kutoka tanzania umegarimu kama milioni 56 hivi fedha za kitanzania kwa ajili ya tiketi za ndege nyingi zikiwa daraja la kwanza na biashara pamoja na posho zao wao wanaita pa-diem. Hizo fedha hazijumuishi maandalizi ambayo tunatafuta gharama zake bado.

    ReplyDelete
  9. florian rweyemamuMarch 28, 2010

    wandugu zangu, nchi iliyo makini uwapenda na kuwakumbatia wananchi wake kama wadau wa muhimu sana katika maendeleo ya nchi husika. Tanzania ni masikini sana. Tujiulize swali la msingi
    Ni faida gani anayoipata mtu aliyepo Msamvu kutokana na mkutano huu wa Diospora?

    Nionavyo mimi hii sera ya diosporalism imeanzishwa na wachache wenye nguvu ya ku 'lobby' au wenye ushawishi katika dola ili kutekeleza matakwa yao. 'Powerful lobby groups' siyo jambo geni ulimwenguni. Hata leo huko Ulaya na Marekani wakulima wachache wakubwa na wenye pesa nyingi wana lobby serikali zao zitoe ruzuku kubwa kubwa ili kulinda soko la chakula wanachozalisha na hivyo kuwaondoa sokoni wakulima kutoka nchi masikini kama zetu.

    Vile vile watanzania walioko ughaibuni naweza kuwalinganisha na wakulima wa kizungu wenye ushawishi wa ku lobby washikaji wao waliopo serikalini.

    Kama serikali yetu ingekuwa makini basi ingetenga kiasi cha pesa na kuwaunga mkono wawekezaji wa kiuhakika wa kitanzania walioko diospora ili kuwekeza kweli kweli katika sekta mbali mbali ili kuleta kweli maisha bora kwa kila mtanzania.

    Ili kuwa 'fair' nawaunga mkono wana diospora kwa kuanzisha jumuiya wa watanzania walioko UK. Kinachotakiwa na kuunganisha nguvu za watanzania walioko siyo tu UK bali baadaye hata ughaibuni kote ili muunde kitu kama kampuni yenye nguvu ya kuwekeza kwenye miradi ya maana huko nyumbani kwenu.

    Ila kwa sasa watanzania waliopo ughaibuni wanaishi mmoja mmoja tu na hamna nguvu ya kuwekeza katika miradi yenye tija kwa Taifa letu.

    Kinachotakiwa kufanyika sasa siyo kwa watanzania ( viongozi) kwenda kuuza sura huko ulaya na kukwangua vidola vichache tulivyonavyo huku bali ni kwa balozi zetu zilizopo ughaibuni kutekelea diplomasia ya kiuchumi zaidi na kuwaunganisha watanzania kikawa kitu kimoja chenye nguvu ( taasisi) inayoweza kuwekeza katika miradi mbalimbali huku kwetu. Hapo mtakapokuwa mna act kama kitu kimoja ndipo mkutano wa diospora utafanyika na siyo ulaya bali hao madiospora itabidi wenye nyumbani kuchezea ngoma huku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...