Katibu mkuu wa ATSA akihesabu dola 1500 kutoka kwa mzee Rajabu kabla ya kuzikabidhi kwa mweka hadhina wa ATSA Omary Pindo, huku mkurugenzi wa elimu ya juu Prof. Abel akishuhudia. Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Alhaji Profesa Dihenga (wa tatu toka shoto) akisikiliza kwa makini risala ya wanafunzi (msomaji hayupo pichani). Baadhi ya wanafunzi walio hudhuria kikao cha katibu mkuu wakimsiliza kwa makini mh,pro.DIHENGA pindi walipokutana naye katika chuo kikuu cha Blida.
Mama kibaya alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu jinsi gani serikali inavyo wasaidia wanafunzi wanaosoma nje ya nchi pindi wanapopata na matatizo ya ugonjwa ikiwemo kuwarudisha nyumbani kwa matibabu.
Mh.Katibu mkuu akiwa ndani ya usafiri maalumu aliondaliwa na wenyeji wake.msafara wa katibu mkuu ulipewa ulinzi mkali ukisindikizwa na ving’ora vya polisi.
Mh.katibu mkuu na ujumbe wake wakiwa na viongozi wa jumuia ya wanafunzi wa tz wanaosoma Algeria (ATSA), toka shoto ni Seif Pepo(rais wa ATSA),pro.Dihenga(katibu mkuu),Habibu H.Ruhombo(makamu wa rais ATSA),prof.Abel (mkurugenzi wa elimu ya juu) na mwisho ni Mh..NYATEGA(mkurugenzi mtendaji wa bodi ya mikopo).

Jumuia ya wanafunzi watanzania nchini Algeria (ATSA) kwa mara nyingine tena wiki iliyopita ilipata kutembelewa na ujumbe mzito wa wizara ya elimu na ufundi ukiongozwa na mheshimiwa katibu mkuu wa wizara hiyo Mh. Alhaji Profesa Hamisi Dihenga akiambatana na mkurugenzi mkuu wa elimu ya juu Prof. Abel, Mkurugenzi mtendaji mkuu wa bodi Mh. Nyatega, pamoja na maafisa watendaji wakuu wa wizara Mama Kibaya na mzee Rajabu na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa mh. Flavian Komba.

Ziara hiyo ya siku 7, ilikuwa na lengo la kujua matatizo na maendeleo ya kielimu ya wanafunzi wakitanzania wanaosoma Algeria . Ujumbe huo uliweza kutembelea vyuo mbalimbali na pia kupata fursa ya kuongea na wanafunzi wa kitz nchini Algeria.

Wanafunzi hao walionesha furaha na shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuonesha kuwajali raia wake wanao soma nje ya nchi. Algeria inatoa scholarship sio tu kwa tz bali karibu nchi zote za Africa na baadhi ya nchi za Ulaya na Asia.

Pia ujumbe huo uliweza kukutana na waziri wa elimu ya juu, Sayansi na technologia, wizara ya Utalii na Mazingira. Katibu mkuu alifurahishwa na mapokezi mazuri aliyoyapata kutoka kwa serikali ya Algeria na wanafunzi watanzania wanao soma nchini humo. Serikali kwa ujumla imeridhika na ubora wa kiwango cha elimu ya juu inayotolewa nchini Algeria.
.
Katibu mkuu aliweza kuchangia chama cha wanafunzi hao (ATSA) dollar 1500 na mkurugenzi mkuu mtendaji wa bodi ya mikopo naye alitoa dollar 1000 kwa chama hicho, hapo awali chama kilipokea dollar 2000 kutoka kwa Mh. Membe Waziri wa Mambo ya nje pindi alivyotembelea nchi hiyo hivi karibuni.Ujumbe huo mzito tayari umesha rejea nyumbani

-Imetolewa na idara
ya mawasiliano ATSA.
Rais +21355433727,
mkm/rais+213551713920.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Jamani siku 7 Algeria????? Mimi sioni mantiki ya katibu mkuu kukaa siku 7 kwa pesa za walipa kodi eti kuangalia matatizo ya wanafunzi. Kweli nini vipaumbele vyetu kama taifa? Kwa mtazamo wangu, kama ni kufanya ziara ndefu hivyo basi angekwenda Ulaya Mashariki ambako mara kwa mara tunasikia malalamiko ya wanafunzi.

    ReplyDelete
  2. Hii ziara ina mkono wa mtu, kwa nini Algeria ndiyo iwe focus ya serikali nzima, maana hao wote wanakwenda huko either kwa shinikizo la mkubwa wao wa kazi

    Swali, mbona sisi wanafunzi wa Russia ambapo wapo wanafunzi wengi wa Tanzania tunakufa njaa na matatizo kibao hatutembelewi????????? Mbona India wanafunzi wa Tanzania mpaka wanapata vifo na manyanyaso lakini hawatembelewi?????? Mbona watanzania wapo nchi nyingi Ulaya mashariki hawatembelewi????????
    acheni ubaguzi, acheni siasa zenye mtizamo wa kidini au kwa kuwa Algeria ni nchi ya Kislamu.

    ReplyDelete
  3. WEWE UNAYEBWABWAJA NANI KAKWAMBIA ALGERIA KUNA WATOTO WA WAKUBWA?KWA TAARIFA YAKO HAO WA INDIA NDIYO WANAONGOZA KWA KULIPWA POSHO KUBWA!!ACHENI ITIKADI ZA WATU WASIO KUWA CIVILISED KABLA HUJABWABWAJA FANYA KWANZA RISERCH!KAKWAMBIA NANI NCHI YETU INAFATA UDINI? HAO WAKURUGENZI WOTE NI WAKRISTO SASA WATAMPENDELEA NANI KWA UDINI?WANAFUNZI ALGERIA WANAONGOZA KWA DISPLINE NA NDIYO MAANA KIONGOZI YEYOTE ANAPOKUJA KWA MISSION ZA SERIKALI NI LAZIMA AOMBE KUKUTANA NAO TOFAUTI NA NYINYI MNAOPIGA AMA KUTUKANA VIONGOZI HUKO MLIPO!!SISI NI WAZALENDO BABA ZETU WAKULIMA NA WAUZA MAGENGE!!NDIYO MAANA NA SISI NI WAZALENDO WA NCHI YETU!!TUNAIPENDA TANZANIA DAIMA!!TUNASUPPORT SERIKALI YETU TUNATAKA MAENDELEO!!WATOTO WA WAKUBWA WANASOMA MAREKANI NA UK SIO ALGERIA. ENDELEENI KUTUKANA VIONGOZI MTAKULA JEURI YENU

    ReplyDelete
  4. Russia hampatani na ubalozi wenu!!wanafunzi wa India mmezidisha umach know!!bahati mbaya pia mpo ktk nchi ya wabaguzi kuliko zote duniani poleni kwa kupigwa tupo pamoja tunawasaport!!hata nasisi huku algeria tunamatatizo mengi tu ya kiuchumi na sivyo kama mnavyodhani, serikali yetu inajal watanzania wote na sio kama mnavyoropoka.

    ReplyDelete
  5. MDAU WA ELIMUApril 18, 2010

    kwa ninavyojua mimi wanafunzi wewe shida na matatizo ni wanafunzi wa vyuo vyetu vya Ndani ya nchi.Algeria hawana matatizo ya kiasi cha kutembelewa kila siku na viongozi wa Bodi ya Mikipo na wizara yenye dhamana ya elimu.
    Kwanza Algeria wanapewa pesa nyingi sana na Bodi na vile vile nchi ya Algeria wanatoa pesa kwa wanafunzi wa Kitanzania na elimu ya Juu Algeria ni Bure,hivyo pesa nyingi inatumika kwa matumizi yasiyokusudiwa.
    Lakini kwa wanafunzi wa Ndani kwanza kuna madaraja na ni lazima kulipa ada,maisha kwa ujumla na gharama kweli zinaumiza kwa Tanzania kuliko hata huko Algeria.
    Me ningeomba viongozi wetu wawe makini katika ziara zao maana ziara zingine hazina umuhimu.
    Viongozi angalieni vyuo vyetu vya Ndani mazinngira yake ni magumu sana kuliko hata inavyoweza kuelezeka.Mabweni hayatoshi na hata uduma za vyoo na maji safi si za uhakika,nenda pale Udsm mlimani na Mabibo hali ya huduma hizo ni ngumu sana.
    me naona viongozi hawa wangeongea kwanza na wanafunzi wa ndani kisha ndo waende huko nje,maana ndani kuna shida nyingi sana hata kuliko nje.

    ReplyDelete
  6. Katibu mkuu hakwenda Algeria kwa lengo la kutembelea wnafunzitu! lengo kuu la msafara huo lilikuwa ni kukutana na wadau wa serikali ya algeria kujadiliana mambo mbalimbali ambayo tanzania inaweza kufaidika through Algeria.ieleweke kuwa Algeria inatumia mfumo wa elimu wa mfaransa,ambao ni tofauti na mfumo wa elimu wa tanzania,hivyo msafara wa katibu mkuu umelenga kusoma mfumo wa elimu wa algeria na kujifunza mambo mengi ambayo ni wazi kuwa algeria imeendelea zaidi YA MARA 1000 kuliko tz:
    ieleweke pia,ujumbe wa wizara umetembelea nchi nyingi sana mfano:china 2005,hii ni mara ya kwanza wizara ya elimu kutembelea algeria ukiondoa mara1 ambayo mm kibaya alienda algeria kulipotokea tetemeko la ardhi wanafunzi wkalazmika kurudishwa tz kuepuka maafa:ww unaoingiza udini cjui ni msomi wa aina gani unaetumia feelings kuliko akili to make ur jugements!!! 2hell!

    ReplyDelete
  7. wanafunzi wa ndani ya nchi hawana shida yeyote wanataka pesa za kuendea disko na kuonga tu!!huyo mwanafunzi aliye nje akipatwa na shida hana pa kukimbilia mnataka wauze unga?na kujiuza kwa mabinti?wkt wewe uliye ndani ya nchi ukipatwa tatizo unakimbilia kwa baba!!yeye aende wapi?serikali inaongozwa na wasomi wanajua nini wanachofanya!!watoto wa vigogo wanasoma ndani ya nchi na nchi za mabepari tu

    ReplyDelete
  8. asilimia 98 ya wanafunzi wanaosoma algeria ni wakutoka vijijini watoto wa wakulima, yani wakuja kweli Dar transit!!na sio watoto wa wakumwa kama mnavyosema,pia huo udini unaongea kuhusu serikali inaonyesha undani wako jinsi ulivyo halisi!!kwamba wewe ndio mdini!maana usingekuwa hivyo usingeamsha suala ambalo halipo!!kwani kunawanafunzi wa dini mchanganyiko na algeria inasomesha nchi zisizo za kiislam pia africa nchiza, ulaya na Asia

    ReplyDelete
  9. mimi niko russia huku kuna matatizo kibao na pia ubaguzi wa rangi upo sanaaaaaaaaa, wewe kiongozi wa Algeria muongo siyo kweli hatupatani na balozi, isipokuwa Balozi anajitahidi sana ila serikali haitoi support kama nyie mnayopata,pia nina ndugu yangu yupo India kule wanafunzi wa TZ wanalalamika lakini hawasikilizi na wahindi ni wabaguzi kuliko hata Russia, tunaomba hao viongozi weje kutembelea Russia waone mfumo wa Elimu maana Russia ipo Juu mara 1000 kuliko Algeria usikia wewe jamaa wa Algeria unayejidai wewe mtoto wa mkulima.Kwa taarifa yako karibia sote tunaosoma nchi hizi za Russia, India, Ulaya mashariki , hizi nchi ni masikini watoto wa wakubwa hawaji huku, kwahiyo sote ni watoto wa wakulima, hatuna uwezo wa kusoma marekani, Uingereza wala Ulaya Magharibi, sote ni watoto wav kulima kama ndicho kigezo basi nasi mtufikilie. Swala la mtizamo wa kidini yawezekana siyo kweli lakini tunalichunguza, tumeweka kwenye record, if the trend persists, we will conclude.

    ReplyDelete
  10. Wewe anon wa 12:06:00 pm ndiye mdini mkubwa na roho ya giza la chuki. (1) Ujumbe huo haukwenda Algeria kwa ajili ya wanafunzi tu. TZ ina mikataba mingi ya ushirikiano na Algeria tangu enzi za Mwalimu. (2) Mbona Algeria ilitusaidia kwa silaha katika vita dhidi ya Idi Amin wakati wazungu wako "wakristo" walitusia. (3) neda kamuone psychologist udeal na issues yako badala ya kututapikia sumu yako ya chuki. AMANDLA!!!!!!

    ReplyDelete
  11. mimi nimekuwa nasoma maoni yenu sitaki kuingilia malumbano yenu, mimi niko katika nchi ya wastaarabu huku Finland, Elimu ni bure, kwa kweli huku ni kama hakuna ubaguzi kama ninavyosikia India. Swali langu, Mbona wahindi wapo wengi bongo na hawabaguliwi??????? Kwanza huku Finland wahindi hawana lolote, ni sawa na sisi tu, yaani hawana social status yeyote, Kwa nini sasa ni wabaguzi kihivyo huko india???????????sijui kwa nini??????mimi nawashauri Watanzania njoo msome huku Scandinavia yaani Finland,Sweden,Norway, Denmak achana na hao makobachori mtikila aliwaona, wanafikiri dunia ya sasa ni ya kujivunia rangi ya ngozi ya mtu, hawaoni Marekani pure black first lady, sasa nimeanza kuona kwa nini wahindi bongo hawajichanganyi na wabongo, Dawa yao ni viongozi kama Amini aliyewafukuza Uganda, kwa kweli mtu mbaguzi wa rangi ananikera muno tena muno ni shetani.

    ReplyDelete
  12. RECORD GANI HIYO MTAKAYOWEKA NYINYI HUKO!!HIYO NDIYO KAZI YENU UTISHIA NYAU WATU WAZIMA!!HUKO NYUMA MLISHAWAHI KUMTISHIA BALOZI WENU HUKO RUSSIA!!MKAWAFUNGIA MLANGO MKAJIKUTA BAADHI YENU SHULE HAKUNA!!HIVI MTU MWENYE AKILI TIMAMU HAPA KTK HILI SUALA UDINI UMEANZIA WAPI?KAMA NYINYI SIO WADINI KWNZA?MAANA ATLEAST HUKO RUSSIA MNAUBALOZI LKN HAPA ALGERIA UBALOZI HAKUNA!!NA SERIKALI INAKWEPA KUFUNGUA UBALOZI NA ALGERIA NI MOJA YA NCHI MUHIMU SANA KWA TANZANIA!!INATUSAIDIA KTK SECTOR NYINGI MNO!!TOKEA ENZI ZA NYERERE!!SASA KAMA HUO UDINI BABA YENU NYERERE NDIYE MDINI!
    HIVI MNAFAHAMU KUWA RUSSIA INAWANAFUNZI ALGERIA?WANAFUNZI WAKIRUSSI MPAKA WAKICHINA WAPO WANASOMA ALGERIA.

    ReplyDelete
  13. HII NI HAKI YENU VIJANA WALA MSIJIHISI MMEPENDELEWA, HAKUNA UPENDELEO KTK HILO!!KWANZA ILIBIDI MUWE MNATEMBELEWA ATLEAST MARA MOJA KILA MWAKA!!NA HAYO NDIYO MATUMIZI YA PESA ZA SERIKALI!!KUMJALI HASA MWANANCHI WAKE NA HASA MWANAFUNZI KWANI HUYU AMETUMWA NA NCHI.
    JE MNATAKA HIZO PESA ZA SERIKALI ZITUMIKE KUPELEKEA VIMADA SALOON?
    KUHUSU UJIO WA BODI NA WAKAGUZI WA SERIKALI WALIFIKA KOTE HUKO INDIA, CHINA, CANADA, USWIZI, UFARANSA RUSSIA N.K.
    ILA WALIKATAA KUONANA NA WANAFUNZI KWA RECORD YAO MBOVU YA KUPIGA NA KUTUKANA VIONGOZI,LKN WALIPOFIKA ALGERIA WALIPOKELEWA VIZURI NA WANAFUNZI NA SIO SERIKALI!!HII INAJENGA LOVE NA UZALENDO KWA RAIA NA NDIYO MAANA WALIKUBALI KUKUTANA NA WANAFUNZI NA KAMA MLIVYOONA FAIR PLAY ILICHEZEKA WAKAPIGA PICHA ZA PAMOJA!!SOTE TULIONA PICHA ZA WAKAGUZI NA WATU WA BODI KWENYE VYOMBO VYA HABARI!!INABIDI NA NYINYI MJIFUNZE ADABU NA UKARIMU NDIYO MILA HALISI YA MSWAHILI MTANZANIA NA SIO USHENZI,NA UJUAJI, CHUKI NA UJANJA WA KIZAMANI WA KUTISHIA WATU WAZIMA MENDE.
    mtanzania bwana yani mmeshaanza kuoneana wivu mpaka kwenye haki zenu,roho za kwanini hizo

    ReplyDelete
  14. Poleni kwa kupigwa huko India!!hapo suala sio kutembelewa bali serikali inatakiwa kulinda haki za raia wake popote pale duniani, muhindi ni mnyama na sio binadamu!!hivi mnajua huko kwao wenyewe wanabaguana itakuwa waishi na mtu mwengine?muhindi hata akiwa maskini vipi jeuri ndiyo asili yake sasa mlikubali vipi kwenda kusoma kwa washenzi hao?
    rudini nyumbani wenyewe walio wengi ni maskini wa kutupwa kuliko sisi.
    msikubali kunyanyasika na wanyama hao wasio na hata maji safi ya kuoga na kunywa na sehemu za kulala hawana. kwahiyo wakimuona mwanafunzi na vijisenti vyake wanataka kumtoa roho.
    poleni ndugu zetu,rudini nyumbani na sisi tuwatimulie mbali kwetu

    ReplyDelete
  15. Hao wanafunzi wa ndani kila siku wanakutana na viongozi na kutatuliwa shida zao!!wanauwezo wa kugoma lkn huyu aliye nje ya nje agome aibishe nchi?jamani tumieni akili mwanafunzi wa nje hana pa kukimbilia akipatwa na tatizo

    ReplyDelete
  16. KWANZA KABISA NINGEPENDA KUWAULIZA HAO WANAOHOJI SAFARI YA KATIBU MKUU NA UJUMBE WAKE NCHINI ALGERIA JE MBONA HAWAKUHOJI SAFARI YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA UJUMBE WAKE WALIPOKWENDA ALGERIA NA SAFARI YA WAKAGUZI WA SERIKALI PAMOJA NA MHASIBU MKUU WA BODI WALIPOKWENDA NCHI HIYO HIYO;
    PILI HIVI NI WASOMI GANI NINYI MNAOPANDIKIZANA FITNA ZA CHUKI NA ZA KIDINI MIONGONI MWENU HIVI HIYO ELIMU YENU IMEWAOKOA NN AU NDIO HIYO ELIMU YA KUKARIRI NA WIZI WA MITIHANI NDIO UMEWAFIKISHA HAPO MLIPO KWELI TAIFA LINAELEKEA KULA HASARA HIVI MKIJAPEWA OFISI SIO MTABAGUANA KWA UDINI NA SEHEMU MTU ALIYOSOMA KUWA KAMA ANATOKA ALGERIA NA MM NIMESOMA RUSSIA NA NDIO HR MANAGER SIMPI KAZI.
    TATU VYOMBO VINGI VYA HABARI TZ VINAZUNGUMZIA NIDHAMU MBOVU KWA WANAFUNZI WA RUSHIA KWA KUWATUKANA VIONGOZI WA SERIKALI MABALOZI ULEVI NA UMALAYA KWA BAADHI YENU ILA HATA SIKU MOJA HATUJASIKIA HILO SUALA KWA NCHI KAMA ALGERIA;
    NNE VIONGOZI WANAPOKWENDA ALGERIA WANAAPLICIATE MCHANGO WA WANAFUNZI KTK MAPOKEZI MPAKA VYONI WAKUU WA VYUO WANAWASIFIA WANAFUNZI WA TZ NI WATULIVU NA WENYE NIDHAMU SIO NJE TU HATA MADARASANI NA AKILI ZAO ZIMETULIA NA PERFOMANCE YAO NI KUBWA UKILINGANISHA NA WANAFUNZI WENGINE HILO HATUJASIKIA RUSSIA
    TANO BODI ILIKUBALI KUONGEA NA WANAFUNZI KWA SABABU WANAFUNZI WOTE SI NDANI WALA SI NJE WAMEJENGA CHUKI NA BODI KUWA WANAKULA HELA ZAO NA KUCHELEWESHA ILA SIO ALGERIA AMBAPO WAMEPEWA UKWELI NA UWAZI NI KWA NN HELA ZINACHELEWA NA KUANZIA SIKU HIYO WANAFUNZI WANA IMANI NA BODI WIZARA PAMOJA NA SERIKALI KWA HIYO NINYI MTAKULA JEURI YENU NA UHUNI MNAOFANYA INAELEKEA VICHWANI MWENU HAKUNA KITU NDIO MAANA MNAJUDGE MAMBO BILA DATA NA KUENDEKEZA UDINI AU NDIO NINYI MNAOFAULU MITIHANI KWA KUKARIRI NA KUIBA MITIHANI TUNAWATILIA SHAKA;
    SS NI WASOMI HEBU TUHUKUMU JAMBO KISOMI NA SI UBISHI WA KWENYE KAHAWA AU MASKANI;

    ReplyDelete
  17. India walio wengi ni wanasoma watoto wa vigogo na mafisadi, tunajua watoto wengi wa vigogo mfano wajukuu wa Nyerere, mawaziri na wakurugenzi wengi watoto zao wanasoma India na Malesia, data tunazo!!maskini hawezi soma India maisha ni magumu mno kama hauna kitu!!kuthibitisha kuwa kuna watoto wa vigogo hata posho wanayopewa na bodi ni kubwa mno!!na ndiyo inayowapa wazimu na kufanya wahindi wazitolee macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...