Ankal eeeh!
Sisi ni wananchi tunaoiishi maeneo ya Kwembe - mbezi ambayo kwa sasa kunafanywa mji endelevu, Tunamasikitiko makubwa na Serikali kwani tunaona kama tunaonewa.

Tulilipwa fidia ndogo mwaka 2008 ya sehemu yetu (fidia ya ardhi tu bila fidia ya nyumba zetu) ila tuliambiwa kuwa tungemilikishwa sehemu ya makazi kwaajili ya hizo nyumba tulizo nazo (sehemu tunazoishi) ili tuweze kuendelea kuishi na kwa vile tulikwisha jenga...sasa tumeitwa kuchukua invoice ya kumilikishwa ardhi ila kwakweli hatuoni kama tunatendewa haki, bei ya kiwanja ni kubwa sana yaani kwa kila square meter moja tunalipishwa sh elfu 6 (6,000) na vilevile unaweza kumilikishwa sehemu ambayo hakuna nyumba yako.

Sasa je hii nyumba yako ambayo umeijenga kihalali inaenda kuwa mali ya mtu mwingine kwa misingi ipi? na kama anamilikishwa mtu mwingine je Wizara ya Ardhi ina utaratibu wa kutoa fidia ya nyumba?

Vilevile je ni halali kwa Serikali kutoa kiwanja kwa kiasi kikubwa hivyo kwa wananchi wake ambao tumeishi hapo miaka yote?

naomba bwana Michuzi tufikishie kilio chetu kwa Wizara ya Ardhi, nyumba na maendelea ya makazi kwa kupitia blog yako..

wananchi wa Kwembe kati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nashukuru blog hii kwa taarifa mbali mbali. Mimi pia ni mhathirika wa kadhia hii. Lakini hata fidia sijalipwa wala nini walifika tu wao na polisi na kupima kwa mabavu. Nimeandika barua wizarani bila majibu. Naomba kama kuna mtu anayeweza kunipa nini la kufanya ili nichukue hatu.

    Strategy yangu kwa sasa ni kupambana na huyo atakayepewa kwa njia zote kama vile kumpeleka mahakamani na kumzuia kinguvu.

    ReplyDelete
  2. pole sana kaka. watu wa ardhi na serikali wanasumbua sana na kuzulumu.naelewa mnavopata shida. ila tafuta mtu wa ardhi mmpe kitu kidogo basi atakupandishia thamani ya vitu vyako na nyumba. maana hata sisi wazee walikuwa na eneo hapo kwembe , sasa serikali imesema inataka kujenga chuo kikuu cha muhimbili. hatukuwa na nyumba . mazo tu na shamba tumelipwa million 22. chakushangaza mtu wa ardhi analazimisha apewe million 5. ahaa. kwa kazi gani ndio rushwa za bongo kaka hizo. at the end tumempa lakini less amount. wezi sana hao kuwa mjanja. wahi nikuwahi hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...