Alikiba akiwapagawisha mashaki wake waliofika katika shoo yao iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Club Afrique
T.I.D akiwa na wacheza shoo wake stejini
T.I.D akifanya vitu vyake
Alikiba nae hakuwa nyuma kuwaburudisha mashabiki wake.
T.I.D na Alikiba

Alikiba na TID jana usiku waliwafurahisha wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jijini London, wanamuziki hayo walifanya tamasha katika ukumbi wa Club Afrique.

Wapenzi wengi walionyesha kufurahishwa na tamasha hilo lililowajumuisha wanamuziki hao wawili kwa pamoja.

Mwandishi wa Blog ya TZ-ONE Ally Muhdin alipomuhoji Christopher Chagula ambaye ni mpenzi wa muziki wa kizazi kipya kuhusiana na tamasha hilo alisema kuwa amefurahishwa na jinsi wanamuziki hao walivyoweza kufurahisha wapenzi wa muziki jijini London.

Wanamuziki hao watafanya onyesho lingine Reading siku ya jumapili katika ukumbi wa Face Club. Wanamuziki hao wamewahakikishia wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jijini Reading kuwa watafanya onyesho kabambe.

Mkurugenzi wa BongoDjs DJ Richie Richie amesema kuwa anawaomba wapenzi wa wanamuziki hao kufika mapema ili kuweza kufanikisha tamasha hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2010

    mwazo sikuzote mzuri!! nawaombea mungu muendelee hivi hivi Msije mkaja kutafutiana mchawi tu bure!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2010

    HAPO READING PAKOJE? MBONA NAPASIKIA SANA NA INAELEKEA KUNA WABONGO WENGI, NINATAMANI SANA KUJUA PALIVYO NA PENGINE IKO SIKU NINAWEZA KUFIKA. INAELEKEA NAPAPENDA PIA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2010

    najuta kwanini nilikwenda kwenye hii shoo. Too much u-wanna bee, yaani haina radha hata kidogo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 02, 2010

    SHSREHE ZA MEI MOSI ZILIFAFANYIKA SEHEMU MBILI MNAZI MMOJA NA UWANJA WA UHURU.

    BLOGO HII IMEONYESHA SURA YAKE HASA NA HII SI SAWA. NBC,NMB NA NSSF NI SAWA NA 08% YA WAFANYAKAZI TANZANIA. SEKTA ZOTE ZA UMMA ZAIDI YA 90% HAWAJARIPOTIWA NA BLOGO HII.

    MICHUZI BLOGO UNATUPA UJUMBE GANI?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 02, 2010

    Reading kama vile manzese au kariakoo.Wabongo wamezagaa wengi. wabongo wengi wako huko ukiwa town utasikia kiswahili unajisahau kama upo uk.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 02, 2010

    JAMANI NIELEZENI VIZURI HAPO READING KUKOJE? NAOMBA SIFA ZA HAPO, MBONA HUKU BONGO WATU WENGI WANAPAFAHAMU? PAKOJE ZAIDI YA KUWA KAMA MANZESE NA KARIAKOO?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 02, 2010

    Leave our Kariakoo alone!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 02, 2010

    hebu acheni upunguwani kwani manzese na kariakoo wanaishi nyani???hovyoooo,reading bomba tuu sema wabongo wapo nyomi wengiwao ni ex-students hakuna la ajabu zaidi wana makutano yao unatapata vyakula vyenye ladha ya kibongo.naona wanaopasagia watakuwa ni wale waliopigwa bomba aka deportation kwani wengi walitokea hapo-pana majungu balaa.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 02, 2010

    Aisee Reading pana majungu ile mbaya, wapiga box wakikutana ni majungu kwa kwenda mbele. Asikutishe mtu mdau wangu wa bongo, kama maisha yanakulipa huko baki huko hukooo. Reading kuna full kusota. watu na elimu zao wanafanya kazi za kipumbavu na no kuheshimika. Ukitaka u enjoy jiingize kwenye vijiwe vya jioni na wewe uanze umbeya kama wafanyavyo wengi, kama ni mwanamke haya tena

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 02, 2010

    Nakubaliana na huyo hapo sijafika hapo mahalai ila kuna ndugu yangu alikua anaishi hapo akahama kwa ajili ya majungu yaliyopo hapo. Anasema watu wengine ni umbeya saaana na sijui Mirungi inavyutwa sana tu hapo....

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 02, 2010

    Weye unasema ati watu wanaelimu zao wafanya kazi za kijinga. Nani wa kulaumu hapo? Kalaumu mafisadi walomeza nchi na Kikwete kuachia hili liendelee tu. Watu wako radhi wafanye kazi za kijinga kuliko kurudi bongo.

    Kila siku twawaona watu waja hapa kuomba tuwekeze huko bongo. Waomba misaada tusaidie sijui nini huko. Sijaona hata mmoja anayesisitiza watu wakimaliza maelimu yao warudi bongo..Pana ulaji hapa wameona hata waosha vyoo waweza kuweka kibanda huko kwao...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2010

    naungana na nyinyi wadau ni kweli jamani reading kuna majungu bin umbea yani nilipita hapo nikae wiki moja tu manake nilikuwa naendelea mbele kwa box la obama nikaona nipoe kwa bibi kwanza wee niliondoka baada ya siku mbili tuu! kwa kweli huko ni wambea sana manake nilisikia story za bongo hata mie nilikuwa sijazisikia na nilikuwa bongo yani niliblooo si msomee tu upaparazi manake mnayaweza mashushu si mashushu bali ni umbeaaaaa uliovuka mipaka mh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...