JK akimtunuku katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bwana George Yambesi Nishani ya Utumishi Mrefu na maadili mema Daraja la Kwanza katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mjini Dodoma leo.nishani zilizotolewa leo ni pamoja na Nishani ya Utumishi mrefu na Maadili mema daraja la kwanza kwa watumishi wawili na nishani ya utumishi mrefu na Maadili mema daraja la pili iliyotolewa kwa watumishi nane.
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2010

    Hapo mwake, nimekubali, mnyonge mnyongeni haki yake apewe. Namkubali Mzee Yambesi anastahili. Inapendeza sana kuona kuwa utumishi wa mtu unatambuliwa. Hongereni wote hapo wote mnatendeana haki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2010

    nakupa hongera sana Katibu Mkuu tunajua juhudi zako kubwa za kuendeleza utumishi wa Umma. tunaomba muangalie WIZARA YA MAMBO YA NJE KWA MAKINI, imeoza uchafu mtupu, hawataki pandisha watu vyeo. Idara ya utawala haifai kabisa irekebishwe yote maana atujui DAP ni Asia dachi au Mnubi. tusaidie kwa hilo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2010

    Mimi pia nampa nishani yangu ya utumishi bora Bw. Yambesi. This guy is serious na Wizara yake pia. We need watu kama hawa. japokuwa hapo Ikulu mlishaanza kuvuruga mipango ya Utumishi wa Umma hasa katika ajira ila naona mko on track. safi sana.

    Sasa hapo kwa mtoa maoni wa pili naona hilo swala linahitaji kufanyiwa kazi. Unajua hiyo Wizara ya Mambo ya Nje mimi huwa hata siielewi. Haiko serious kabisa. Pamoja na watumishi kupandishwa au kutopandishwa vyeo kuna tatizo kubwa la ajira zao. Vimemo kutoka kwa wajomba na mashangazi, baba mdogo sijui na nani na hasa kutoka kwa Mawaziri na hapo Ikulu vimetawala muda mrefu ajira za hapo. kama hilo halitarekebishwa mapema basi hiyo Wizara inaelekea kuoza zaidi.
    Wafanyakazi wako bize na safari tuuu kama mabosi wao na usishangae kuona wafanyakazi hawajui hata basic work.

    Nadhani ni Muda wa Yambesi na Katibu Mkuu mpa Bw. Saula kupapiga msasa hapo Mambo ya Nje.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2010

    Kweli George Yambesi anastahili TUZO hiyo ni watanzania wachache sana wenye moyo wa uzalendo uvumilivu na upendo kwa nchi YAO kama yeye
    big up EVEN NORMAL PEOPLE RECONGNIZE YOUR WORK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...