Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania mjini Rome, Mh. Leonce Uwandameno(kushoto),afisa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. Salvator Mbilinyi (katikati), na kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Ndugu Andrew Chole Mhella


*************************************
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno pamoja na Katibu wake Ndg. Andrew Chole Mhella, leo asubuhi, tarehe 23 Juni 2010, waliwasilisha rasmi barua ya utambulisho wa Jumuiya ya Watanzania Roma kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Italy.

Viongozi hawa walipokelewa na afisa utawala wa ubalozi Mh. Salvator Mbilinyi. Itakumbukwa kuwa jumuiya hii ya Watanzania Roma, iliundwa rasmi mjini Rome tarehe 30 Januari 2010.

Moja ya malengo mengi ya uundwaji wa Jumuiya hii ni; kuwaunganisha watanzania wanaoishi Roma na sehemu zingine za Italy, ili kushikamana na kusaidiana panapo kuwa na furaha au tatizo la aina yoyote. Jumuiya inalenga kuhamasisha wanajumuiya ili waweze kuishi kwa malengo hapa ugenini na kupeleka maendeleo nchini Tanzania.

Jumuiya hii pia inalengo la kuwa chombo cha kuutangaza utamaduni na utalii wa nchi yetu hapa nchini Italia.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jumuiya ya Watanzania Roma.


Kwa matukio mbalimbali yanayotokea hapa Rome, mnakaribishwa kwenye official blog ya Jumuiya
www.watanzania-roma.blogspot.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    Haya ndio mambo tunayotyataka...Mbarikiwe sana huko Rome....

    Smart people do the smart things


    Mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2010

    Hao watu wa wawili kutoka kulia, wanaficha nini?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2010

    Haichekeshi... Watanzania tuwe serious jamani..Hawa ndugu wanafanya hahakati za kujenga taifa we ndugu unaleta utovu wa nidhamu..

    ReplyDelete
  4. MBONA JAMAA KAMA VILE WANAOGOPA?....SIJUI WANAOGOPA NINI...KUWENI NA CONFINDENCE JAMANI, NYINYI NI VIONGOZI...DUH

    ReplyDelete
  5. Mbona CHIBILITI NCHUMALI hayupo hapo?

    Amehama au amerudishwa Tanzania kwa kukosa MAKARATASI?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2010

    Mdau wa pili tar 24,June 04:33 nakuunga mkono kweli wanaficha nini hao makaka wawili?!Yule wa kwanza kushoto naye yuko kama anajihami.Basi alimradi wapo tu.Haya kila la kheri.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 25, 2010

    Mdau wa mwisho wacha ushamba na ukiritimba! Unga mkono vitu vya maendeleo na si vitu vya kipuuzi unavyosupport!! Unatakiwa ufurahi unapoona mtanzania mwenzako anajaribu kama si kufanya jambo la maana kwa Watanzania wenzake na kwa nchi yake. Get a lesson!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 25, 2010

    Mdau Jun25,10:00.What lesson have you given here??Nawaunga mkono wakati wote waTanzania wenzangu wenye kufanya vitu vya maendeleo kwa nchi,kama tuko realistic!Nina ishi Roma miaka kibao!!!And as far as lessons are concerned learn to be elastic,you should also have a bit of sense of humour!!!!Bado nauliza wanaficha nini?!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2010

    aah jamaa vipipi kibindoni!hahaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...