mpanda mlima France John akiwa na mgeni wake,Rausi Gerald wakiwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro.
njia itumikayo kupita katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
muonekano wa barafu katika kilelele cha mlima Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Asante Mdau na Bro michuzi kwa kuturushia hizi taswiraz, This is kind of pictures and information we would like to see in this "advanced" Blog. Our mountain is beautiful, real!! unfortunately barafu ndo inazidi kupungua....

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa pic michuzi na wale wambea wa global warming wanaosema eti mlima kili hauna barafu, na hiyo hapo ni nini? theluji au?

    ReplyDelete
  3. Hilo bango hapo kileleni mbona haliendani na hadhi ya mlima wenyewe? Mamlaka husika, mliona ni sawa kabisa kuweka kituko kama hicho juu ya utajiri na alama yetu muhimu ya kujivunia? Nawashauri mliondoe bango hilo na kuweka linaloendana na hadhi ya huu mlima, bila kuingiza ufisadi. Toeni tenda kwa wabunifu (kwa uwazi na bila upendeleo) muone watakachopendekeza.

    ReplyDelete
  4. bwana michuzi asante sana kwa hizi picha. siku nyingi nimeona documentaries juu ya huu mlima wetu mzuri lakini sikujua kumbe kuna vibarabara kama hivyo. jamani kuna mtu anajua hivyo vibarabara ni watu wanasukuma snow pembeni au ni kwasababu watu wanapita hapo mara kwa mara. sisi huku niliko huwa tuna shovel snow kutengene njia ya kupita. hata hivyo nina fikiri kusukuma snow juu ya mlima itakua ngumu sana especially ukifikiria kuwa hewa ya huko ni very thin na hakuna oxygen ya kutosha.

    ReplyDelete
  5. Congrats!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  6. HICHO KIBAO NI AIBU KWAKWELI. NADHANI NDO MAANA SHAMSHA MWANGUNGA AMEUKOSA UWAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KWA KUBWAGA UBUNGE NDANI YA CCM, KUTOKANA NA KUSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAKE VIKIWEMO VITU VIDOGO KAMA HIVI. BANGO GANI HILO???????? SHAME!! TUNAWAPA WAHUSIKA WIKI 5 WALIONDOE LASIVYO TUTAANDAMANA HUKU MOSHI

    ReplyDelete
  7. NASHUKURU SANA KWA PICHA HIZO. MIMI NI MMOJA WA WATANZANIA WACHACHE WALIOWAHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO INGAWA NI ZAMANI KIDOGO MWAKA 1997 NASHUKURU NILIPATA FURSA HIYO NA NAOMBA WATANZANIA WAJITOKEZE ZAIDI GHARAMA NI NAFUU MNO KWA WATANZANIA, WAKATI HUO NILILIPA SHILINGI 40,000 TU KWA SIKU ZOTE TANO ZA KUPANDA MPAKA CHAKULA, ILA KUFIKA KILELENI PIA INAHITAJI NIA HASA, UKIWA NA MIJIGUVU LAKINI KAMA HUNA NIA NA HUFUATI USHAURI WA KASI YA KUPANDA NA CHAKULA UNACHOTAKIWA KULA KWA MUDA HUO HUFIKI MBALI.

    GLOBAL WARMING NI KWELI IMEANZA KUUATHIRI MLIMA INGAWA SIO KWELI KWAMBA IMEPOTEA ILA MLIMA UMESHAPOTEZA ASILIMIA ZAIDI YA 50 YA BARAFU YAKE KWA KINA NA KUTAPAKAA KWAKE.

    MDAU ULIYETOA WAZO KUSEMA BAO HALIENDANI NA HADHI, TULIPATA MAELEZO WAKATI FULANI TUKIWA KATIKA ZOEZI LA UPANDAJI MLIMA KWAMBA MATERIAL INAYOWEKWA HAPO NI ILE INAYOWEZA KUHIMILI HALI MBAYA SANA YA HEWA KWA SABABU KILELENI HAPO PANA UPEPO MKALI SANA NA PRESSURE IKO CHINI SANA, NA HATA BENDERA ZA TAIFA ZINAZOWEKWA KILELENI HAPO ZA KITAMBAA, ZIKISHAPACHIKWA TU, BAADA YA MUDA MFUPI SANA (MASAA)HAKUNA KINACHOBAKI, KITAMBAA KINAKUWA KIMESHACHANIKA.

    WITO: TUSHIRIKI KWA PAMOJA KUBORESHA MAZINGIRA DUNIANI KOTE KWANI UHARIBIFU WA MAZINGIRA HAUNA MIPAKA, TUPANDE MITI TUKISHINDWA HATA MAUA JAMANI MAJUMBANI MWETU ILI KUONGEZA HEWA SAFI, TUEPUKE KUACHA CARBON PRINTS ZETU (TUSIZALISHE CARBONDIOXIDE) TUANZE NA MMOJA MMOJA KWA SABABU ONE IS MANY.

    ReplyDelete
  8. WEKENI BANGO LA DHAHABU JAMA! SI TUNAYOOOO? TATIZO LIKOWAPI? MWAGIA ZEGE LA NGUVU HAKUNA MTU ATANYAKUA,NINI KUJIAIBISHA HIVYO? WEKENI KITU WATANZANIA KURINGIE WENGINE JAMANI! NA WATOTO WETU WARINGE HUKO MASHULENI, BADALA YA KUONEKANA WAMETOKA KWENYE CAVES!!

    ReplyDelete
  9. ni kweli taswira ziko juu ila kusema ukweli kwa sie tuliopanda mlima miaka ya nyuma kama 99 ni kweli barafu imepungua, wakati sie tunapanda kulikuwa hakuna hata njia katikati ya barafu manake ilikuwa ni nyingi mno kama miamba, natamani kupanda tena nikaone hayo mabadiliko ila yataka moyo si mchezo, hilo winter niliaapa kutorudi tena

    ReplyDelete
  10. Hiki kibao ni safi kabisa...imeshakua alama ya kilele cha mlima Kili. Anyway hata fulana ya Michuzi ni poa tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...