Dear Friends,
I would like to express my heartfelt gratitude for all your support.
Today we mark the start of a new journey.


This morning I submitted my nominations forms for re-election for the Kigoma North parliamentary seat ready to serve again the people of Kigoma North and my country TANZANIA.


In order to make it happen am humbly asking for your support; if you would like to see Zitto back in Parliament and serving our nation I ask for your support.
I am ready to serve you once again.

DONATE:
Help Zitto keep fighting for our future and our country.
Join the campaign by making a donation today.
Your contribution and support will help us in our campaign.
To donate please
Make a Deposit to Our Campaign Account:
NAME: ZITTO KABWE ZUBERI
BANK: CRDB BANK
ACCOUNT NUMBER: 01J2082022500
Contact Details:
Contact Person: Mhonga Ruhwanya
Mobile Number: +255 0758 000 111
E-mail Address: zitto2010@gmail.com
FACEBOOK: http://www.facebook.com/zittokabwe
Blog: http://www.zittokabwe.wordpress.com/
Follow me on my Twitter Account: http://www.twitter.com/zittokabwe
On FLICKER(PICTURES): http://www.flickr.com/photos/zittokabwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. JAMANI NYIE WAGOMBEA UBUNGE MLIOMALIZA KIPINDI KILICHOPITA ILE MIBULUNGUTU MLIYOPEWA HIVI KARIBUNI KAMA SIJUI NINI NDIO MMEMALIZA MIAKA YENU 5 HAITOSHI MPAKA TUWACHANGIE TENA KUTOKA MIFUKONI MWETU?

    MAGARI MNAYO, HIYO MIPESA YOTE MIMILIONI MNAITAKA YA NINI? HEBU TUPENI MCHANGANUO KWANZA!

    na mimi nakuwa kama wao ukiwaendea kuwaomba mkopo au msaada wanakwambia "kalete mchanganuo"

    ReplyDelete
  2. MTOA MAONI HAPO JUU UMENIWAHI!

    Na Mimi nilitaka kuuliza vivo hivo; kama ushaingia mjengoni, na unahitaji kupata re-election, inabidi ujipange kwa kutumia rasilimali ulizokuwa nazo tayari. AIDHA
    Hiyo michango ni ya nini? Kwani sheria ya uchaguzi hairuhusu mgombea kutumia fedha jimboni kwa wakati huu; kwa vile matumizi ya aina yoyote jimboni yanaweza kutafsiriwa kuwa rushwa; hivi mheshimiwa Kabwe amelizingatia hilo?

    MHESHIMIWA KABWE atapata wingi wa kura Jimboni mwake endapo aliwatumikia wapiga kura wake kwa mujibu wa matarajio yao, na atapata uchache wa kura ikiwa vyenginevyo.

    HATA hivyo, tunamtakia mheshimiwa Kabwe mafanikio kwenye azma yake ya kurudi mjengoni.

    Wadau - UPANGA DAr Es Salaam

    ReplyDelete
  3. Pat-MagazetiAugust 20, 2010

    Elimu kwa Watanzania,

    Kama unalipa kodi na wagombea viti vya ubunge na urais was chama Tawala kama awachangishi pesa. Sasa nani ana garamia uchaguzi wao?

    ReplyDelete
  4. Hapa karibuni tumekuwa tukimuona ZITTO kama si mtu wetu tena, Amekua anaonekana kama kashanunuliwa hivi, na amekua akitoa misaada ya kampeni kwa ''rafiki'' zake walio nje ya chama chake, sasa leo uniambie tena nikuchangie wewe wakati wewe unazo mpaka za kugawa vyama vingine!inaingia akilini kweli?wewe kama umeshapewa ''mabilioni'' na kututosa sisi watu tuliokutegemea sana kwanza ujue iyo ni laana kama umechukua, bora urudishe, pesa si kila kitu kaka, Dr Slaa anavyopambana kuifanya Tanzania kuwa mahali bora pa kuishi ni kutoka moyoni, furaha yake itakua kuona Tanzania inastawi, sasa wewe kama furaha yako ni pesa unakosea sana. Sasa unataka tukuchangie, hizo ulizopewa mpaka ukaanza kutuletea kiburi cha eti ''siasa haikua chaguo langu la kwanza'' ziko wapi?na kuanza kuleta jeuri kwa chama kiasi cha kutufanya vijana tuonekane ukiingia kwenye siasa ni umekosa kazi nyingine au unataka kuongeza mapato,na si nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.Kama ningekua na uamuzi nisingependa kukuona katika mafanikio ya kisiasa kwa sasa. Ningeshauri ukae katika uongozi wa chama tu ukue kwanza kichama, maana naona hizi sifa za kitaifa zinakupumbaza kaka, unaanza kujiona muhimu kuliko chama ambacho ndo msingi wa demokrasia ya kweli. Si kila mtanzania anatokea kigoma kaskazini, ila karibu kila mtanzania anataka kuona mabadiliko kwa taifa letu, sasa wewe mwenyewe huwezi kuleta hayo mabadiliko, ila chama, sasa unapoanza kuonekana kama mamluki unakwamisha sana maendeleo ya chama.
    Michu thanks, haya ni yangu maoni.

    ReplyDelete
  5. Jamani tuache kukwamisha mtumishi wa bwana aliyejifisha kwa mgongo wa siasa, huyu ni kijana mwenzetu anaitaji support yetu ili atutengenezee njia.. Ni vijana wangapi wanapata nafasi zinazofanana na yake na wanafanya nini? kijana kaingia bungeni na ameleta mabadiliko kiasi kwamba hata wabunge wa chama tawala wameona ni kweli wengi wapi itapelekea taifa letu kuangamizwa na kikundi cha watu wachache.. Je? niwangapi wanajua matumizi ya mapesa tunayochanga kwenye sherehe? mbona hatuoji hilo.. Imani ndio msingi wa maendeleo. Tafakari kwanza anachoomba kijana halafu maamuzi unayo wewe mwenyewe kuchanga ama la.. ZZK keep it up we are together with u..GM

    ReplyDelete
  6. Kilimo kwanza!!!!!!

    ReplyDelete
  7. tatizo bw Zitto umekuwa hueleweki eleweki kabisa,mara siasa naacha,mara umerudi so tukuelewe vipi ndugu yetu?umekuwa kama vile kichwa kimekua ukaota pembe ukaanza kuringa, mapambano hayataki nyodo,ungetangaza nia tangu mwanzo ungeeleweka but sasa mmh umekaaa sana, well tutakuchangia kidogo,for umekumbuka blanket asubuhi kaka!

    ReplyDelete
  8. Acheni kujiongelesha
    Unatoa mada ya kwanza
    Then unatoa ya pili kujifanya "mtoa maoni hapo juu umeniwahi" ili kutilia uzito comment yako.
    Unajiongelesha mwenyewe.
    Zote 2 zinatoka pamoja. Ulijuaje kama wa juu atasema hivyo?

    ReplyDelete
  9. Ni vyema kutekeleza kauli zetu. Hivi si wewe Mh. Zitto ulisema sasa unapumzika na unataka kusoma kwanza? au ndo flip flop.

    Kama bado una hamu na siasa, nadhani ni wakati muafaka usione aibu vuka tu msitari kama wengine uje kwetu CCM tuendeleze chama chetu tawala.

    Pili ni ushauri tu. Wengi wetu Watz (mfano hata wa jimbo lako Kigoma) hatujafikia hii level ya kuanza kuchangishana kupitia mitandao (the Obama like style)!
    Chapisha tu fomu zitembezwe na wapambe wako unaowaamini kama vile unataka kuoa tena!

    ReplyDelete
  10. Mimi sifahamu Kiingereza. Nasubiri Tangazo la Kiswahili, au kwa anayeweza kutafsiri afanye hivyo...

    ReplyDelete
  11. Lugha gongana Mwheshimiwa! Hata wewe msomi unasema '......am humbly......' badala ya '......I am humbly......'? Aibu! Tunang'ang'ania cha nini kama kiinglishi hatukiwezi. Alafu ni nani huyo hasa asiyeelewa Kiswahili unayemuomba mchango kwa lugha ya kigeni?

    ReplyDelete
  12. usiwaulize nyani wanafanya nini kwenye shamba la mahindi

    ReplyDelete
  13. Dr. Slaa kasema mahela munayopata wabunge ni mengi sana sasa kwa nini hizo hela usizitumie kwa ajili ya kampeni?

    Kiinua mgongo chako baada ya kila miaka 5 nu kikubw akuliko hata profesa wa mlimani sasa mchango wa nini?

    Yaani kweli munataka na sisi wauza samaki na maandazi tuwachangie nyinyi munaoendesha mashangingi?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  14. sasa bwana mkubwa Nyepesi me sijakuelewa kitu kimoja,japokuwa sifungamani na chama chochote, ila
    wewe kwenye mikutano yako karibu yote huwa unazungumzia swala la umasikini. kwamba tanzania imezidi kudidimia kwenye lindi la umasikini.
    sasa leo masikini hao hao unawakamua tena eti wakuchangie ufanye kampeni,ha!!? sasa hiyo michango bwana mkubwa masikini thithi twaitoa wapi!? na tukishakukuchangia maendeeo kwa wote au kwa Kigoma Tu!?
    kama vipi kama alivyosema mwenzangu hapo chapisha vipeperushi uwatembezee wananchi wako wa kigoma bwana mkubwa cos sisi wenyewe tunahitaji kuchangiwa pia. Vilevile utaomba vipi Support kwa Lugha isiyo yetu!? watanzania walio wengi hasa hao wapiga kura unaowategemea lugha yao ni kiswahili, hivyo ni bora tu uongee lugha yetu me naona ndio utaeleweka haraka zaidi kuliko staili hii.Umenisoma Mh. Nyepesi!?

    Ni hayo tu

    ReplyDelete
  15. Ni jambo la maana kuomba msaada manake hata mchango wako bungeni umeonekana na hasa ile issue ya Buzwagi iliyokufanye upate suspension. Lakini kuna maneno ya chini kwa chini yanasema ushanunuliwa na CCM? Hebu mheshimiwa toa tamko hapo, lkn mime binafsi nitakuchangia kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...