Afisa Ubalozi Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bibi Joyce Kafanabo (mwenye suti nyekudu), akiwa na baadhi ya wanafunzi kutoka shule kadhaa za sekondari za Jimbo la Califonia, Marekani. Wanafunzi hao wakiwa na walimu wao ambao hawapo pichani, waliutembelea Ubalozi wa Tanzania wakiwa katika ziara ya mafunzo ya kujifunza historia ya Tanzania, mila, desturi na tamaduni za watanzania, walitaka kujua pia mfumo wa siasa za Tanzania, Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii na pia mfumo wetu wa elimu. Maelezo hayo kwa wanafunzi hao yalitolewa na Bibi Kafanabo kwa niaba ya Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Baada ya maelezo ya kina pamoja na maswali na majibu, wanafunzi hao wamevutiwa na kuonyesha hamu kubwa na wamelezea nia yao ya kwenda Tanzania mwakani (2011).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...