Mazungumzo baina ya Ali Saleh wa BBC akizungumza na Bimkubwa Said Abdallah, mama mzazi wa Ahmed Ghailani, Mtanzania wa asili ya Zanzibar aliyekutikana na hatia katika kosa moja la kuhusika katika mipango ya kuushambulia Ubalozi wa Marekani katika nchi za Tanzania na Kenya.

Mashambulizi hayo yaliyotokea nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998 ambapo katika shambulio hilo, watu 11 walifariki mjini Dar Es Salaam, Tanzania na zaidi ya 200 mjini Nairobi, Kenya huku maelfu wakiachwa na athari za moja kwa moja au za kuondokewa na ndugu, jamaa, rafiki na wafanyakazi wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwa nini umesita hapo tu ungeliendela kuwa ni mtanzania asili ya zanzibar, kikwajuni, majumba ya mjerumani, block number xyz na kadhalika.

    ReplyDelete
  2. Mkuu,

    Leo kama sikoseo ndio mara ya kwanza kukuona unaandika kutumia "mtanzania mwenye asili ya Zanzibar". Kama umewahi kutumia kama context nyengine basi samahani. Lakini kama hii ni mara ya kwanza nataka kujua kama umesema hivi kwasababu huyu jamaa anashtakiwa kwa kosa hili au una sababu nyengine. Jee kuna siku utaweza kusema mtanzania mwenye asili ya bara au Tanganyika? Ni katika mazingira gani utaweza kusema kama hivi?

    ReplyDelete
  3. A. aslaykum

    lah, ndio kwanz nisikie nione matumizi ya lugha namna hii, yenye mwelekeo wa kuleta tofauti kwa watanzania. Pengine kulikuwa na haja ya kuandika hivyo. Naomba muhusika kidogo atufafanulie madhumuni hasa ya kutumia lugha husika- mtanzania mwenye asili ya Zanzibar.

    Ni mimi Mtanzania halisi

    ReplyDelete
  4. Katika mahakama ya nyani, mshtaki nyani na jaji nyani hukumu ya haki itakwenda vipi hapo?

    Mungu amsaidie huyo Ghailani maana hatutaujua ukweli halisi.

    ReplyDelete
  5. In JESUS name aliye HAI......MUNGU WANGU.....mbona hayo mabomu hayakuwagusa wamarekani ambao ndiyo waajiriwa wa balozi hizo?....kama kweli huyu malaika ndiye aliyehusika basi pamoja na knowledge ndogo ya physics niliyonayo...nitakubaliana na dhana kwamba YALE MAJENGO PACHA IMARA KABISA...yaliyeyushwa na TU-NDEGE........SIKU ZOTE WAJINGA NDIO WALIWAO NA MUOGOPE MWENYE PESA!.......mbuzi wa kafara ni muhimu ili kuficha aibu!....kudadadeki!

    ReplyDelete
  6. Wewe mda hapo, walio kufa wengi walikua nje ya jengo na ndani ya uzio, na bumu hilo halikuja na nguvu kubw akama liliopigwa nairobi ambalo liliua pia wamarekani na dhani 8 walikua .

    Hakuna cha mbuzi wa kafara hapo, Wamarekani hawawezi mshaikilia mtu asiye na hatia wakati wakijua Alqaida wako na wana wacheka kuwa wana kamata watu wasio na hatia, unadhani wamkamate na kumfunga huyu kumdanganya Bin ladin kua wao wana nguvu wakati Binladini siatakua anawaona wajinga tuu. huyu kaishapatikana na hatia afungwe maika mia . Kwanz akanini alikimbilia south Africa mnanyama huyu asiye na Utu.

    Na nyie waZnz leo mnajifanya kuupenda utanzania, siku zote ooh mimi Mzanzibari, siku mnatatizo ooh mimi Mtanzania, ok tuna mkubali huyu ni Mtanzania mwenzetu ambaye ni wachache kama yeye walio na roho ya mauaji,tena kwa tamaa ya pesa, maana kmaangekua ni kachakachuliwa akilia basi angejilipua ila yeye akashiriki na kukimbia nchini.

    ReplyDelete
  7. @ anon 6
    huyu katenda kosa na sio kuwatwika mzigo wazenji wote,je wao wakisema wale watangyika wote malaya kwa kuwa kuna malaya wakibongo kule nungwi ,je hii ni haki ? jambo la pili wazenji wana fahari na jina lao liwe liwalo ila jambo likienda kombo waandishi wa bara husema wazenji lakini likiwa zuri basi huwa watanzania.....hili ndio watu wasilolitaka lisemwe moja tu aidha Zanzibar au Tanzania (kwa bara) kwa Zanzibar wao lao ni moja tu Zanzibar

    ReplyDelete
  8. Wewe mdau wa 01:22:00 PM uko very naive kuhusu Wamarekani. Hebu soma hasa mikenge ya CIA halafu uone kama kweli wanaweza kubambika kesi kwa wasio na hatia au hawawezi.

    Mfano mmoja tu ni Saddam Husein wa Irak ambaye hakuua Mmarekani lakini akaambiwa anazo silaha za maangamizi. Silaha hizo hazikuonekana mpaka leo.

    Huko Afghanistan wanafanya nini kama sio kuwahukumu raia wa vijijini wasio na hatia kwa kuwapiga mabomu?

    MICHUZI TAFADHALI TUWEKEE NUMBERING SYSTEM KWENYE HIZI COMMENTS ILI IWE RAHISI KUINUKUU.

    ASANTE

    ReplyDelete
  9. tanzania without zanzibar is tanganyika and tanzania without tanganyika is zanzibar

    ReplyDelete
  10. ....Hawa jamaa...(Wamarekani) mie wananishangaza na kunihuzunisha pale wanapoingia mikataba na Nchi mbalimbali kuzuia au kulazimisha kwa nguvu, raia wao(wamarekani) wasishitakiwe na nchi husika........kuwa mmarekani soo precious!!! jamaani.

    ReplyDelete
  11. At least now you guys comes to senses....Huko Iraq kaishia kupachafua mpaka inasikitisha....ALIKUWA ANATAFUTA NINI?.....kweli vita ni tamu ukiipigania kwa mwenzako na siyo kwako.....haya wamepata nini....wanaiambia nini dunia.....CHINA Hiyoooo inanyanyuka.....nayo waitengenezee sababu za kuiangusha....sijui wataanza na kupiga mmabomu ubalozi wao wa hapa TZ (ofcourse BUDGET ya renovation always inakuwa imeandaliwa before)...then waseme bomu lilitengenezwa CHINA!.....Jamani such bloody strategies hata kwenye vitabu vitakatifu zimetabiriwa kwamba zitakuja KUANGUKA KWA KISHINDO!.........BWANA YESU ASIFIWE SANA NA ATUPITISHE MBALI NA IBILISI HUYU.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...