Balozi wa Jamhuri ya Djibouti, Saidi Amin Shamo akielezea machache juu ya sherehe hiyo ambayo alikuwa ameiandaa nyumbani kwake. Kulia ni Mshereheshaji wa sherehe hiyo Baby Kabaye ambaye pia ni mtangazaji wa Choice Fm 102.6 FM.
Baadhi ya Wanachama wa Unity of Women Friends (UWF) wakiwa katika picha ya pamoja usiku huu nyumbani kwa balozi wa Djibout.
Pichani kati ni Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti Bi. Mariam Shamo akiwa amepozi na wageni wake usiku huu,kushoto ni Prof. Faya mbaye ni mtaalamu wa magonjwa ya mifupa wa hospitali ya Aghakhan,jijini Dar pamoja na mwanae.
Mwanamuziki wa kimataifa ajulikanaye kwa jina la Ahmad Naji kutoka nchini Mogadishu akitumbuiza kwenye hafla hiyo usiku huu.
Mke wa Balozi wa Jamhuri ya Djibouti Bi. Mariam Shamo (katikati) akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga (kushoto) kwa wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo iliyofanyika nyumbani kwake usiku huu.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Alphonso E. Lenhardt (katikati) akimtambulisha mkewe kwa Balozi wa Uturuki Dk. Sander Gurbuz katika hafla iliyokuwa imeandaliwa na Balozi wa Djibout Bw. Shamo kwa ajili ya kumshukuru Mungu kufunga mwaka wa 2010 salama na kuukaribisha mwaka 2011. Pia ilihuhusu maadhimisho ya miaka 6 ya Universal TV yenye makao yake makuu nchini Uingereza.
Mithupu huyo mpiga gitaa anatoka nchi inayoitwa Mogadishu au Somalia? Maana kama bado nakumbuka mji mkuu wa Somalia ni Mogadishu. Sina hakika hiyo nchi ya Mogadishu ipo maeneo gani.
ReplyDeleteMwaka haujaisha huu!
ReplyDeleteKumbe kuna NCHI inaitwa MOGADISHU!!
Duh!
Hovyo! Mwandishi mzima? Eti nchi ya Mogadishu? Hovyo!
ReplyDeleteNaona Mwandishi anashambuliwa kwa kuwa eti ametaja kuwa kuna nchi ya "MOGADISHU", lakini mimi sijaona hilo jina Mogadishu kwenye habari hiyo, badala yake ninaona "JAMHURI YA DJIBOUTI". Hivi kuna matatizo ya uono na pengine usomaji kwa upande wangu au habari ilibadilika baadae?
ReplyDeleteMwenyeji wa Tanga- Ughaibuni
Absolutely positively Gorgeous Woman.I say this in a complimentary way
ReplyDeleteBongo kweli wiki kadhaa mbele yaani mmeshamaliza mwaka? na party za kumaliza mwaka mmeshazila?
ReplyDelete