Align CenterGodfrey Chinga akiwa mzigoni.
Picha na Peter Bennet


Chuo cha Muziki cha Nchi za Jahazi (Zanzibar) kikishirikiana na wahisani wa makampuni ya Vodacom, Mnarani Beach Cottages na Zanair, wameandaa onesho la muziki la aina yake kwa ajili ya kusherekea mafanikio ya Chuo katika mwaka 2010. Onesho hilo, ambalo kwa kawaida hufanyika kila mwaka na kujulikana kwa jina la URITHI CONCERT litafanyika katika kiwanja cha Muembe Kisonge, Michenzani mjini Zanzibar leo Ijumaa.

Mratibu wa onesho hilo, Mahsin Basalama, amewaahidi wapenzi wa muziki mjini hapa burdani mwanana kutoka kwa makundi mbali mbali ya Chuo ikiwemo Taarab, Ngoma za kiasili, Kidumbaki, Muziki wa Dansi pamoja na Jazz. Katika wasanii mashuhuri watakaotumbuiza ni pamoja na mpigaji Kidumbaki maarufu Makame Faki pamoja na wengine wengi. Onesho hilo litaanza saa mbili usiku na kutegemewa kufurika kwa wapenzi wa muziki kutoka sehemu mbali mbali za kisiwa cha Unguja.

Chuo cha DCMA kimekuwa kikiandaa Onesho la Urithi kila mwaka kwa dhamira ya kuyawasilisha mafanikio ya Chuo kwa jamii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwavutia vijana kufanya maamuzi ya kujifunza muziki kupitia kozi zinazotolewa hapo Chuoni.

DCMA ni taasisi isiyo ya kiserikali (NGO) inayoendesha mafunzo ya muziki yenye kuweka msisitizo katika ufundishaji wa muziki wa ala za muziki wa kimatuduni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...