Mkurugenzi wa kituo cha matangazo cha Radio One, Deogratius Rweyunga akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi wa upatikanaji wa habari za papo kwa papo (Breaking News) kupitia njia ya simu za mikononi.kushoto ni Mkurugenzi wa Infocomtechnologies,Finehasi Lema na Kulia ni Momose Cheyo wa OnPoint.

NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO

Mkurugenzi wa kituo cha matangazo cha Radio one Deogratius Rweyunga amesema kituo hicho kimezindua rasmi upatikanaji wa habari za papo kwa papo (BREAKING NEWS) kupitia simu za mkononi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Rweyunga amesema uzinduzi huo utawasaidia wananchi walio mbali na radio au ambao hawana kabisa kupata taarifa popote walipo hata kama wamebanwa na majukumu ya hapa na pale.

“Radio one tumeamua kuzindua huduma hii ya kuwafikishia taarifa wasikilizaji wetu kupitia simu zao za kiganjani ili tuweze kuwajuza nini kimetokea wapi na kwa muda gani”. Amebainisha Rweyunga.

Wananchi watakao hitaji huduma hii wale wanaotumia mtandao wa Vodacom, Tigo na Airtel. Namna ya kujiunga na huduma hii itakubidi kufungua ujumbe mpya katika simu yako kisha andika neno Radio one halafu tuma kwenda 15310.

Rweyunga amesema baada ya kumaliza hatua hiyo utapata ujumbe wa kukujulisha kuwa umeshaandikishwa kupata ujumbe mfupi wa maneno kila taarifa za hapo kwa papo zinapotokea popote pale nchini.

Akizungumzia suala la gharama Rweyunga amesema kila ujumbe utakaopokea utatozwa shilingi 150 tu na ukitaka kujitoa katika huduma hii itakubidi uandike neon Radio one –Stop kwenda namba 15310.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...