aadhi ya wanafunzi wa Vyuo vikuu vya IFM na Chuo cha Kiislam Morogoro, wakihamaki wakati walipokuwa nje ya Ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Msasani jijiji Dar es Salaam leo, walipofika kuulalamikia uongozi wa bodi hiyo kwa kutosimamia taratibu za ulipaji wa ada za wanafunzi na kupanda kiholela kwa ada kutoka Sh. milioni 1 hadi milioni 1.7, jambo linalowafanya baadhi ya wananfunzi kushindwa kulipa.
Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Machunda Lubambula. akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha IFM, wakati akitoa majibu kuhusu malalamiko yao, wakati walipofika kwenye ofisi hizo Msasani jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi hao wakiondoka eneo hili baada ya kutofikia muafaka na kuanza safari ya kuelekea Ofisini kwa Waziri wa Elimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. matatzi kama haya kama hayapatikani muafaka ndio pakupandishwa kwenye bunge ili lijadiliwe. serekali inafanya nini? hili ni tatizo na sio lakuzungumziwa nje ya bunge. kuna wakati rafiki yangu aliniambia jinsi hii bodi ya mikopo inavyowanyanyasa wanafunzi hata kupata mikopo.na sidhani kama kuna system ambayo iko effective ya wanafunzi kurudisha mikopo kama nchi za wenzetu.

    ReplyDelete
  2. ina maana bodi haiwasumbui UD, UDOM, SUA, DIT, n.k. inawasumbua hawa tuu?

    ReplyDelete
  3. nilijuwa tuu, mambo ya tangu ukoloni

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni hivi vyuo vya watu binafsi na baadhi ya taasisi kupandisha ada ovyo,.. bodi kama bodi ina kiwango chake cha kulipa ada,na sio kwamba kila mara chuo kinapo amua kupandisha ada basi na bodi nayo itakubaliana na mabadiliko hayo.
    ukiritimba wa vyuo kupandisha ada ovyo unapelekea usumbu na unatishwa mzigo mkubwa sana kwa wanafunzi na wazazi.

    wito, kwa sisi tulio someshwa na serikali kupitia mapango wa ukopeshwaji tujitokeze na kulipa madeni yetu ilikuiwezesha bodi kua na vyanzo mbadala vya mapato na sio kutegemea serikali peke yake, na hatimaye kuwezesha wanafunzi wengi kupewa mikopo na matatizo kama haya kupungua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...