Kaimu balozi wa Tanzania Rome-Italy ,Mh Silvestri Mbilinyi akisaini kitabu cha wageni mara alipofika katika ofisi ya jumuiya ya Watanzania Italia kwa ajili ya sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania, pembeni ni mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy ndugu Abdulrahaman A.Alli na waliosimama ni katibu mkuu ndugu Kagutta N.Maulidi na mwakilishi wa jumuiya Padova & Venezia ndugu Zacharia Maggid Mhessa.
Viongozi wa jumuiya ya Watanzania Italy katika picha ya pamoja na kaimu balozi wa Tanzania Rome Mh.Silvestri Mbilinyi katika sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya uhuru wa Tanzania.
Mh.Mbilinyi kaimu Balozi wa Tanzania Rome-Italy akikata keki ya uhuru,katikati ni Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy ndugu Abdulrahaman A.Alli na pembeni ni katibu mkuu ndugu Kagutta N.Maulidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi naomba nitoe ushauri wa Bure kwa Kaimu Balozi Mbilinyi ili aweze kuishauri Jumuiya ya watanzania jambo lifuatalo:

    "mpangilio wa rangi za Bendera ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania...mkato huanzia chini kwenye nguzo kuelekea juu na siyo kama ilivyo katika nembo yao kwenye hiyo Meza"

    Nimeamua kumshauri Mbilinyi ili aishauri hiyo Jumuiya kwa kuwa yeye kama mwanaitifaki nafahamu vyema namna ya kuwasilisha ushauri kwa wahusika.
    Kaka michuzi nasikitika sana kuona watanzania wengi huko wakijumuika katika mambo mengi ya Kitaifa ili hali hawaijui hata bendera ya nchi yao ikoje. Ukikosea mpangilio wa Rangi za bendera yako au ukiiweka kinyume moja kwa moja inakuwa si bendera ya nchi tena bali ni kitu kingine...

    shukrani

    ReplyDelete
  2. Shukran mdau wa Thu Dec 16, 11:39:00 pm kwa kuiona dosari ya mchoro bendera katika nembo ya jumuiya ya wa-TZ Italia, hata hiyo bendera ndogo ya mezani picha ya kwanza pia imeshonwa kwa makosa (kinyume. Rangi ya bluu imeshonwa juu badala ya kuwa chini napia michirizi ya njano na kijani imeanzia juu ya mkamti kalikoshikilia bendera badala ya kuanzia chini ya kamti kalikoshikilia bendera. Inabidi kua waangalifu na alama za taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...