Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakihutubia jumuiya iliyofika katika hafla hiyo, Mheshimiwa Lema aliwahakikishia watoto hao watasoma na kupata matibabu bure na Mwenyekiti wa ArDF aliwahakikishiwa licha ya kupatiwa Ada na Matibabu pia watapatiwa Chakula kufuatia kampuni ya Arusha Mambo kuazima shamba lake lenye Ukubwa wa ekari 30 lilimwe na chakula kitakachopatikana kigawanywe katika shule za Kata na Vituo vya watoto yatima, hata hivyo aliomba jamii, mashirika na wadau mbalimbali kuendelea kuchangia Taasisi yao ili imudu kuwasomesha watoto hawa na kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Jonathan Lema na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini Elifuraha Paul Mtowe wakimpatia mmoja wa wazazi Cheti cha kuthibitisha kupatiwa msaada wa Ada na Matibabu kwa watoto wake kwa kipindi cha miaka minne.
Kati ya watoto wenye kuishi katika mazingira ya kati waliojitokeza kuwahamasisha watoto wenzao wenye kuishi katika mazingira magumu kuwa watashinda na siku moja wataishi katika Nchi yenye neema wakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini na mmoja wa mzazi aliyejitokeza kusaidia watoto wenye uhitaji baada ya kununua tshirt za ArDF kama mchango wao kwa watoto wenzao.
Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakiwasajili na kugawa Tshirt na Bendera za Taifa kwa Watoto waliofika katika hafya hiyo kabla hawajaimba wimbo wa Tanzania Nakupenda na baadae wimbo wa Taifa.
Baadhi ya Wazazi na Walezi waliojitokeza wakiwa katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya watoto wao kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kuendelea na kutimiza ndoto zao.
Baadhi ya Watoto kati ya watoto 400 watakaopatiwa msaada wa Ada na Kadi za Afya na Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Mjini kwa kupitia Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo, watoto hao waliojitokeza kwenye Ofisi ya Mbunge wa JImbo la Arusha Mjini kupokea Msaada huo wa Ada wenye thamani ya Shilingi Milioni 60 na kadi za bima ya Afya zilizopata udhamini kutoka Shirika lisilo la Kiserekali la Green Hope linalopata msaada kutoka Serekali ya Canada.
Baadhi ya watoto na Madiwani waliojitokeza katika picha ya Pamoja na Mbunge Pamoja na Mwenyekiti wa ArDF baada ya kupatiwa Ada, Kadi za Matibabu, Daftari na Kalama Ili kumudu mahitaji ya masomo yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hivyo ndivyo wananchi wanavyotaka, CCM acheni siasa za kutaka kushinda uchaguzi tu na sasa mnahangaika na mikakati ya ushindi 2015. Taifa letu bado changa lahitaji maendeleo. Big up sana LEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA! Hongera CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAA!

    ReplyDelete
  2. This Man is genius. We should all extend our hands and support him.

    ReplyDelete
  3. Mfano wa kuigwa..Sio wakishashinda hawaonekani tena mpaka miaka mitano ikishaanza kuisha..Au kutwa kucha kutembelea viwanda na mabiashara wakiishiwa sabuni, sukari na mafuta ya kupikia nyumbani kwao...wasaidieni watoto ada wende shule.....

    ReplyDelete
  4. haya ndio mambo sasa tunayoyataka safi sana mbunge wetu,sio wengine mikelele kutwa hakuna cha maana viongozi wengine igeni jaman sio mwajinufaisha wenyewe tuuu,chadema oyeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  5. Wonderful! It's so nice kuona kuna mtu/ watu wanajitokeza kuchangia Elimu na Matibabu kwa watoto wa kiTanzania. Watoto hao wanaishi kwenye mazingira magumu sana!

    ReplyDelete
  6. safiiiii mbunge wetu wa Arusha Lema endelea na moyo huo onyesha mfano maana kuna wengine viongozi bado wapo usingizini,baadhi yao wengine toka wamepata madaraka hawajawahi kufanya kitu kama hichi wao ni raha tuuuu na maneno mengi,chadema juuuu zaidi wenye wivu jilipueni,tunaipenda chadema

    ReplyDelete
  7. Taifa hili linahitaji watu wenye moyo safi ambao wako tayari kusaidia watoto ambao ndo taifa la kesho. I salute you Lema. God Bless you!!

    ReplyDelete
  8. Inapendeza haswa kuwa na Mbunge kama huyu. Vijana wanahitaji elimu ili kujikwamua katika lindi hili la umaskini linalotukabili anahitaji kuungwa mkono Mh.Lema ili aweze kuwafikia wengi zaidi wenye hitaji hili muhimu..TUMUUNGE MKONO ili na wengine nao waone aibu kwani toka tuwachague hatuwaoni sijui wamejificha wapi HONGERA MH.LEMA

    ReplyDelete
  9. Nafikiri CHADEMA ndio mfano wa kuigwa kwa vyama vya Upinzani nchini. Miaka ya nyuma tulizoea kuona wapinzani wakiibuka wakati wa Uchaguzi tu na hatimaye kutoweka pindi uchaguzi unapokwisha.

    Kwa mfano huu aliofanya Bwana Lema inadhihirisha wazi kwamba CHADEMA ni Chama chenye nia thabiti ya kuwakomboa watanzania.

    ReplyDelete
  10. This is wonderful....na huyu ndio aina ya kiongozi anaefaa na siyo wale wanaoendekeza kujali familia zao na marafiki zao wakiwa wameshikilia sehemu za uongozi katika nchi. Kiongozi lazima atambue shida na matatizo ya wananchi anaowaongoza na aonyeshe kwa vitendo jinsi ya kutatua kero hizo na siyo porojo tu.....

    ReplyDelete
  11. Kaka Mh. Lema hongera saaaana, the DREAM has started to be realized now, let the wisdom and will behind it receive the GODs grace and may HE guide it to its fullest achievement.

    ReplyDelete
  12. Chadema Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeee!! Safi sana CCM kamezeni mkasage chupa mle, mnywe, mkalie, au jinyongeni TUMEWACHOKA!!!! CHADEMA safiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  13. I see something in u Lema,u r real wonderful person at least wanaarusha wanaweza kuguess kuwa we ni kiongozi mteule toka kwa mungu sio wengine porojo tuuu. Arusha msije teleza tena kuweka watu wanaogawa pikipiki kipindi cha uchaguzi kwani badala ya kuwasaidia kimaendeleo watataka kurudisha fedha zao walizotumia kucampaign. And Lema Mungu yuko pamoja nawe kwani kichwa chako hakipumziki kusaidia watu wako, GOD BLESS U MR.Godbless

    ReplyDelete
  14. Kwa kweli ni jitihada za kuigwa na hao wengine wote wanaojiita "Viongozi". Tumechoka na porojo, tunataka vitendo. Achaneni na porojo CCM jamani fanyeni kazi, nyie kukaa na kuwapinga CHADEMA tuuuuuu kila kukicha, nyie hamna hata la maana mnalolifanya zaidi ya kukidhi maslahi yenu binafsi. Ufisadi kibao mnaukumbatia, basi msione wivu Chadema wakifanya! Hakika Watanzania wa leo wanataka kuona mabadiliko, siyo blabla zenu bwana! Hongera Lema, Mungu azidi kukutia nguvu. Hongera Chadema, kila kilicho chema kina baraka ya Mungu, wala msikate tamaa, siku ipo ya kuona mabadiliko ya kweli!

    ReplyDelete
  15. Nimejisikia vyema sana kuona haya unayotenda Kaka. This is more than beautiful. Hili ni jamba adimu na adhimu sana kwetu. Hatuna jinsi ya kuwapinga wanamaendeleo kama hawa. Najua Baba Ridhiwani akiona mambo kama haya ndio anachanganyikiwa na kuanza kuona kama CHADEMA ni jeshi. Big up sana kaka na bado tunasubiri kutoka kwa kaka Mnyika na dada Halima bila kumsahau mkuu Tundu Lissu.
    Barikiweni sana.

    ReplyDelete
  16. MIMI NIONAVYO, NA KWAKUWA NAMJUA BWAMDOGO WETU LEMA, TATIZO UBISHOOO! ANGEPUNGUZA UBISHOO ANGEKUWA MCHAPA KAZI MZURI, NASHANGAA HAPO SIJAONA VOGUE LAKE LA MCHORO lililoandikwa Lema 1 TOKA SAUZI HALIPO Mbele ya CAMERA tehteh! Ila asianze mpango wakugawa hela kama pipi, kinachotakiwa ni kwenda vijijini na kuhamasisha ujenzi wa shule, maji, barabara na kadhalika, sidhani utaratibu wa kugawa fedha utasaidia kwa kuwa wenye shida ni wengi na shida si pesa ni kuwezeshwa kujitegemea ndio njia sahihi, ukiwawezesha wazazi au walezi wa hao vijana waweze kufanya kazi na kujitegemea tatizo hilo litatoweka, wanasiasa tupunguze kukaa mbele ya camera.. twene tukalete maendeleo ya kweli na yatakayodumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...