Wanafunzi wa Chuo cha IFM,jijini Dar wakiwa wamekusanyika asubuhi hii kwenye moja ya sehemu ya wazi ya chuo hicho kwa madhumuni ya kuanzisha mgomo wa kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza.
Wanafunzi wa chuo cha IFM,wakiwa wamekusanyika leo asubuhi ndani ya uwanja wa chuo hicho,wakiwa na mgomo kwa kile walichodai kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwa sababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza

Aidha imeelezwa kwamba kutokana na kugoma kwa wanafunzi hao ni kupinga uonevu na mfumo mbovu unaofanywa na chuo hiko kwao wakati serikali ilishaweka wazi kuwa hakuna na marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vya umma kuzuiwa kufanya mitihani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Serikali natakiwa kutafuta suluhisho la matatizo haya, kuliko kila siku mugomo migomo,
    Au inaelekea serikali inapenda that why they keep on entertaining

    ReplyDelete
  2. serikali inatakiwa itatue matatizo ya wanafunzi kwa muda muafaka ili kuzuia migomo

    ReplyDelete
  3. tanzania inahitaji kuwekewa drip imekwisha kabisa!!!

    ReplyDelete
  4. Uongozi wa chuo ni wa kulaumu na inaonyesha jinsi wasivyokuwa na akili na ubabe wa kijinga,solution acha wanafunzi wafanye mitihani yao vizuri tuu lakini usiwape matokeo mpaka wamelipa fees yote....vitu vidogo lakini carelessness za hawa wajinga zinaleta chaos na kutia hasara kila mtu na kuvunja amani kwa jambo dogo kama hili...aibu sana!

    ReplyDelete
  5. Unaweza kuwa na elimu na bado isikusaidie. Management za vyuo zinatakiwa kuwa makini katika kusikiliza matatizo ya wanafunzi. kila siku matatizo ni hayo hayo, na maneno ya kashfa kutoka kwa viongozi ya management kwakweli tumechoshwa na tunahitaji haki zetu!!!! Wabadilike!!!

    ReplyDelete
  6. Mimi sieelewi migomo mingine na watu mnashangilia. Honesty unataka kusoma tafuta scholarship kama huna hela...Sioni kwanini watu wagome eti kwa vile wengine wameshindwa kulipa ada. Hata sisi tunashida lakini tunalipa kwa shida hivyo hivyo. Sasa hawa sijui ni ubabe...Sasa kila mtu asipolipa wafanyakazi watalipwaje? Kuna mambo ya kusupport lakini mengine tumezidi....Mimi nasoma kwa shida sana semester nisizoweza kulipa nachukua off....Degree nimefanya kwa miaka 6 ...sasa nyie mnadeeka tu hapa ...hakuna cha bure...

    ReplyDelete
  7. Hii ni ujinga tu...Kama mnataka sheria zibadilishwe mngefanya hayo mapema na kujadiliana na uongozi mapema. Ubabe wa kugoma saa hizi hausaidii kitu. Wakilegeza sheria kila mtu atakua anafanya hivyo hivyo kutokulipa ada on time...Wapi kuna cha bure? Na ukifanya mtihani usipopewa matokeo wapi utaajiriwa? Ni wangapi hawajalipa mpaka leo na walimaliza miaka sijui mingapi iliyopita na wamekuja huku kuendelea na masomo? Na wanafanya masters kwa kutumia vyeti vya mlimani na IFM wakatai sisi tunasotea degree za kwanza huku na kutoa jasho haswa..Tunawaona nyie nyie hapo mnajidai kusema sijui nini lakini mkimaliza hamlipi hela za watu.....

    Wengine hapo wanasindikiza tu kwa vile hawajasoma kwa ajili ya mitihani...Lipa usome sio mnagoma mwishoni ...Kwanini usigome kuingia darasani kama ulikua unajua hii sheria itakucost at the end....Life is not easy..Mimi hapa nalipa rent kwa shida sana na naenda shule kwa shida sana. Kazi hamna siku hizi lakini sigomi kulala nje ati nina nusu rent au nimelipa tuition fee half of the year...Lipeni hela au kopesha mahali ulipe kisha ukimaliza shule utapata kazi na kulipa......

    Haki gani mnayotafuta? Ya kusoma bure? Those who stand for nothing fall for anything...common now...

    ReplyDelete
  8. kama serikali inpesa ya kulipa DOWANS, kwanini wananchi wasisome bure? sio kila mtu anaweza kulipa ada, kuna familia nyingi zinashida lakini watoto wao wanapenda elimu / kusoma. kwahiyo kama mzazi hana uwezo mtoto wake akae nyumbani? dont be fools. Mbona mikopo ya elimu ya juu haiwafikii walengwa? unakuta hadi watoto wa mawaziri na vigogo wengine wanachukua mikopo kwa kufanyia starehe zao. We need to be serious with these things. Alternatively - elimu ya juu itolewe bure then we forget about mikobo but kila mzazi ampatie mwanae mahitaji muhimi ya kujikimu awapo chuoni. kwa watu wa part time walipe in full

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...